Ningekuwa mimi, Azam FC ningetimua Wachezaji wote na benchi la ufundi

Atanandi

JF-Expert Member
Joined
Jul 16, 2023
Posts
341
Reaction score
483
Amini nakwambia! Unatumia pesa nyingi sana katika timu hii Wachezaji wanalipwa Kwa wakati wanakula

Ila sasa wanacheza ovyo ovyo, yaani mchezaji hana nguvu za kukimbia uwanjani ndo nini

Fukuza, anza maisha mapya
 
Wafukuzwe kwenda wapi tena! Miaka yote tunafahamu Azam Fc ni timu inayowasaidia wachezaji wake kulea miili, na pia kuota vitambi.

Hata utimue wachezaji wote na benchi lao la ufundi! Bado Azam Fc itabakia kuwa ni ile ile tu. Timu isiyo malengo! Inayocheza kwa kukamia baadhi ya mechi, nk.
 
Azam wamefanya usajili mzuri wa wachezaji ila tatizo nadhani lipo kwa benchi la ufundi. Yule kocha ni mzuri ila kwa Azam bado hatoshi. Naona ana ufaza mwingi na anashindwa kutoa hamasa kwa wachezaji wake.

Tatizo lingine ni kwa uongozi nadhani katika sajili wanazofanya wameshindwa kushughulikia nafasi ya beki wa kati na pembeni. Wanahitaji mabeki wazuri na bora zaidi ya hawa waliopo sasa. Beki la kuanzisha mashambulizi, kupiga pass ndefu na fupi, kuruka n.k
 
Mnawapa presha bure tu,kweye kila nchi lazima iwepo timu namba 3..misri kuna pyramid,morroco kuna far rabat,south kuna kina amazulu,tunisia kuna kina clube african sjui,na tz ndo kuna azam.
 
Ukweli hii Timu Bahir Dar Kama ingekutana na Utopolo pia Ingesumbua....hawafanani kbs na ASAS
 
Kocha ndio fala, Kwa sasa Fei toto hana namba kwenye hiyo timu ila yeye anamuanzisha.
 
mshaulini ostaz yusuf baresa aachane na timu pale azam komplex watengeneze gesti kuuubwa ya kimataifa afrika mashariki na kati
 
Bakhresa bora aendeleze Tanzania ya viwanda tu, kwenye mpira amefeli
 
Fei toto anastahili kuanza kwenye timu ya Azam ila kwasasa uwezowake ni dk 60 tu. Bado mwili wake unamafuta anatakiwa apunguze weight atengeze misuli.
Alitakiwa aingie Mbobo acheze 9 na Dube arudi 10.
Sopu baada ya kutoa assist ya goli akapotea alitakiwa kipindi cha pili aingie Lyanga au Kipre substution ilichelewa.
Kwa ujumla timu ya Azam wachezaji walichoka kabla ya jukumu kwisha.
Fitness lever kimataifa ipo chini.
 
Idris mbombo karidhika mpaka kitambi kimemtoka!

Feisal nae kanenepa vibaya kawa mzito sana

Jibril silla ni garasa la karne hta jama mba ana afadhali.
 
Tatizo la azam sio kocha wala viongozi ni wachezaji kuridhika na kuona tayari walishafikia mafanikio
 
Amini nakwambia! Unatumia pesa nyingi sana katika timu hii Wachezaji wanalipwa Kwa wakati wanakula

Ila sasa wanacheza ovyo ovyo, yaani mchezaji hana nguvu za kukimbia uwanjani ndo nini

Fukuza, anza maisha mapya
Anza kutimua wachezaji na benchi la ufundi la simba.
 
Amini nakwambia! Unatumia pesa nyingi sana katika timu hii Wachezaji wanalipwa Kwa wakati wanakula

Ila sasa wanacheza ovyo ovyo, yaani mchezaji hana nguvu za kukimbia uwanjani ndo nini

Fukuza, anza maisha mapya
Hata Fei Toto na Bangala ungewafukuza? Acha Masikhara ndugu yangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…