Ningekuwa mimi, Azam FC ningetimua Wachezaji wote na benchi la ufundi

Ningekuwa mimi, Azam FC ningetimua Wachezaji wote na benchi la ufundi

Azam wangeachana na mpira wa kimashindano huko wameshashindwa, ni bora wakarudi kwenye ule mfumo wao wa kukuza vipaji na kuwauza nje kama hapo awali,
 
Amini nakwambia! Unatumia pesa nyingi sana katika timu hii Wachezaji wanalipwa Kwa wakati wanakula

Ila sasa wanacheza ovyo ovyo, yaani mchezaji hana nguvu za kukimbia uwanjani ndo nini

Fukuza, anza maisha mapya
Pale Kuna ufadha na uislamu ndio tatizo kubwa...

Dogo mmoja alitoka biharamulo akaja kufanya trial akatafuta connection akapata azam team C tena akapewa jina la ki islamu......................

Kwenye mguu wangu wa kushoto Mungu aliweka kipaji murua na adhimu aliweka engine na akili ambayo nilikua naweza kufanya nilivyo penda...uli itaji macho na sekunde kadhaa mpira ukiwa mguuni kwangu....

Ila mm nili udharau mpira wa miguu Ile NDIO sehemu pekee ningepata mafanikio bla jasho
 
Azam na timu nyingine kubwa usajili wao ni mbwembwe hauna uhalisia wowote. Wachezaji wanasajiliwa kwa hela nyingi zinazotangazwa lakini uhalisia huwa hakuna hela inayotumika ni kidogo. Nyingine ni dili za watu. Hata mishahara wanatangaziwa hao wachezaji huwa ni hewa. Inaishia mifukoni mwa watu.
Hebu jiulizeni. Kwa nini mchezaji anayelipwa dola 6,000 hizo timu kubwa akitoka wala hajishughulishi kwenda timu nyingine kubwa ya nje ya nchi kutafuta maslahi. Anahamia timu ndogo ya kwenye ligi na kulipwa dola 1200? Ina maana anajua thamani yake sio dola 6,000. Na hawezi kwenda popote zaidi ya kuzunguka humu humu.
Tunasajili wachezaji wa nje ambao hawaitwi timu zao za taifa.
Tuache mbwembwe za usajili na dili zake.
 
Back
Top Bottom