Azam na timu nyingine kubwa usajili wao ni mbwembwe hauna uhalisia wowote. Wachezaji wanasajiliwa kwa hela nyingi zinazotangazwa lakini uhalisia huwa hakuna hela inayotumika ni kidogo. Nyingine ni dili za watu. Hata mishahara wanatangaziwa hao wachezaji huwa ni hewa. Inaishia mifukoni mwa watu.
Hebu jiulizeni. Kwa nini mchezaji anayelipwa dola 6,000 hizo timu kubwa akitoka wala hajishughulishi kwenda timu nyingine kubwa ya nje ya nchi kutafuta maslahi. Anahamia timu ndogo ya kwenye ligi na kulipwa dola 1200? Ina maana anajua thamani yake sio dola 6,000. Na hawezi kwenda popote zaidi ya kuzunguka humu humu.
Tunasajili wachezaji wa nje ambao hawaitwi timu zao za taifa.
Tuache mbwembwe za usajili na dili zake.