Ningekuwa na dhamana, nyumba za Magomeni Kota wangeishi wafanyakazi wa Hospitali ya Muhimbili na Magomeni

Usidhani kila mtu anapenda maisha ya magorofani ushindwe kupata hata kimvuli cha mti na kupanda tembeke lako na mabanda ya kuku.
Ile jamii haiwezi kumudu kuishi kwenye majengo kama Yale, nakwambia wengi wao watapangisha na watawauzia wenye hela, serikali haijafanya utafiti wa kutosha. Wale watu wengi wao wanapika kwa vifuu, Kuni, mabaki ya mbao. Wengi wao wanaishi kwa kisamvu na dagaa. Tembelea yale majengo baada ya miezi 6 utasonya hadi basii

Utakachokuta mule bàada ya miezi 6 ni amoja na
1. Masizi kila Kona
2. Uchafu kila Kona
3. Vyoo vimeziba watu wametumbukiza mapedi vyooni
4. Watu wamechukuliana wake na mabwana.
5. Watu wanatuhumiana wizi wa mboga na chumvi
6. Kanga za mipasho zinavakiwa sana
7. Ukimwi unaenea kwa Kasi kwa wakazi wote.
8. Watoto kulawitiana.
8. Watu watapangisha vyumba vyao na kwenda kuishi tandale uswahilini wakapike kwa vifuu.
 
Akili za ubinafsi tu.
Badala ya kuomba wajengewe nyumba zao unataka wapewe za watu waliokwisha ahidiwa kabla ya ujenzi.
Kumbuka wale waliopewa walikuwa wanaishi pale kabla ya ujenzi.
Omba nyumba mpya mradi utakaowahusu watumishi wa kada ulizosema.
 
Inabidi wavunje na kota za kinondoni manyanya pia wazijenge kama magomeni
Kota zile ni uchafu mtupu

Ova
 
Hivi maza alimaanisha 'kisamvu' gani, alitaja kwa msisitizo sana.!
Mother aliwapa nyumba ili kukwepa kikombe kile kimueouke, lakiñi alifahamu akili na kipato Cha wale watu pale sio Cha nyumba zile.
 
Akili za ubinafsi tu.
Badala ya kuomba wajengewe nyumba zao unataka wapewe za watu waliokwisha ahidiwa kabla ya ujenzi.
Kumbuka wale waliopewa walikuwa wanaishi pale kabla ya ujenzi.
Omba nyumba mpya mradi utakaowahusu watumishi wa kada ulizosema.
Logic TU inatosha kuona serikali imekosea kuanza na wale watu kuwapa makazi sehemu ambayo Iko karibu na hospitali za Muhimbili, mwananyamala na Magomeni health center. Halafu unadai huduma Bora itolewe hospitali. Hivi sisi tuna nini? Our think tank is leaking.

Wafanyakazi 644 wa hospitali wangekaa pale wangekuwa na uhakika wa kufika na kutoka kazini Muhimbili, Magomeni na mwananyamala kwa urahisi kabisa na kuhudumia wagongwa muda wote kwa urahisi kabisa badala ya ilivyo Sasa watu wanatoka kibaha, bagamoyo, mbagala, kigamboni kwenda Muhimbili kuhudumia wagonjwa.
 
Akili za ubinafsi tu.
Badala ya kuomba wajengewe nyumba zao unataka wapewe za watu waliokwisha ahidiwa kabla ya ujenzi.
Kumbuka wale waliopewa walikuwa wanaishi pale kabla ya ujenzi.
Omba nyumba mpya mradi utakaowahusu watumishi wa kada ulizosema.
Nakwambia wale waliokusudiwa kuishi mule wengi wao hawawezi kuishi nyumba za vile, hawa ni watu ambao walikuwa na Bata na Kuku wao, mbwa wao, bustani zao, wachoma vitumbua, na kila kitu Cha mtanzania maskini kabisa. Huko juu itakuwaje? Hawa wanahitaji nyumba za chini kila mmoja afuge Kuku wake na njia akipenda.

Kwanini hawakufikiriwa watumishi ambao kazi zao zina maswali kama mbona umechelewa, mbona unasinsia? Mbona hutabasamu kwa mteja? Mbona umeondoka kabla mtu wa kupokea zamu hajafika? Nk.
 
Hoja yako naiunga mkono kwa 100%
Sawa mkuu, tuliowakabidhi nyadhifa wameamua hivyo, hawakuwa na uwezo wa kufikiria kuwa Muhimbili, Magomeni, mwananyamala au Palestine hospitals hazihami pale milele lakini wale wakazi wa waliopewa pale wangeweza kujengewa nyumba nyingine magwepande bila kuadhiri kitu chochote.
 
Temeke nako kota zilivunjwa mbona waliohamishwa hawajajengewa maghorofa?
 
Serikali imejitahidi sana kuboresha huduma za afya Nchini, kuna huduma za kibingwa zinazotolewa hapa nchini, ambapo miaka 10 nyuma ilikuwa ni ndoto, reffferal za kwenda kutibiwa nje ya Nchi kwa sasa zimepungua sana. miundombinu ya Afya katika Hospitali zetu imeimarika sana, japo bado kunachangamoto ndogo ndogo ambazo zinazidi kupatiwa ufumbuzi.

Changamoto bado ipo kwenye maslahi duni kwa watoa huduma wa Afya, kweli suala la makazi kwa watoa huduma wa Afya bado ni changamoto, wengi wao wanaishi pembezoni mwa miji, na ikitokea dharura (Emergence) hasa nyakati za usiku inakuwa tabu sana kwa mtoa huduma kuwahi kufika Hospitali kumuhudumia mgonjwa kutokakana na umbali.

Nadhani imefika kipindi serikali kuwajengea Nyumba watumishi wa idara ya afya zitakazo kuwa maeneo ya karibu na maeneo yao ya kazi kama inavyofanya kwa kada nyingine , wapewe motisha kuwapunguzia ugumu wa maisha, ili huduma wanazotoa ziwe zenye tija kwa Taifa,
Ukienda Nchi za wenzetu, maslahi ya watu wa Afya wameyapa kipaumbele sana, mtoa huduma anatoa huduma hana stress yoyote ya Maisha.

Kuna utafiti mdogo nimeufanya hapa hapa Nchini, Hospitali zile zinazowajali watumishi wake kwenye suala la maslahi, ndio zinaongoza kutoa huduma nzuri ukilinganisha na zile zisizowajali watumishi wake,
Nchi jirani zimeanza kuleta wagonjwa wao kutibiwa Nchini kwetu kutokana na kuhimarika kwa huduma za Afya Nchini. Tukiwekeza vya kutosha kwenye sekta ya Afya miaka ijayo na sisi tunaweza tukawa kama India kwenye sekta ya Afya.

Miaka ya nyuma Hospitali zilikuwa na makazi ya watoa huduma, sio vibaya ukaanza utaratibu wa kuwajengea makazi watumishi wa Afya,

kwa kufanya hivyo kutawapunguzia kazia wanazokumbana nazo kutokana na umbali, wanaweza wakatumia utaratibu wa kuwakata kwenye mishahara yao kodi za nyumba, kama mdau alivyo shauri hapo juu.

Nchi nyingi za Afrika miundombinu ya Afya iko duni, tutumie hii fursa tunaweza tukaongeza Pato la Taifa kupitia sekta ya Afya, tukichanga vizuri karata tunaweza tukawa tunapokea wagonjwa kutoka katika hizo Nchi.

Serikali iendelee kuwaendeleza watumishi wetu wawe na ubobezi kwenye Huduma za kibingwa. Oparesheni za Moyo sasaivi haina haja ya kwenda india, Upandikizaji wa Figo, Uroto, nk zinafanyika nchini kwetu, huduma za Kutibu kansa kwa kutumia mionzi zinapatika nchini tena bure, haya yote yaendane sambamba na uboreshwaji wa Maisha ya watumishi wa afya



"Healthy nation is a wealthy nation"
 
Kwani kuwa mfanyakazi wa hospital ndio nini hasa?
 
Mwambie mama ajenge zingine.
 
Wanawaza biashara, watumishi wa umma ilifaa wapate makazi Ili akili zao zitulie ndo walichofanya wakoloni.
 

Lipa Kodi
 
Sekretari wa TRA au Benki Kuu ana maisha mazuri kwa maana ya marupurupu na mshahara mzuri kuliko daktari bingwa wa upasuaji wa hospitali ya Mkoa wa Kagera... hahahahaha!
 
Ubora wa yale majengo sijui
Zimelipuliwa
Siasa inazimaliza sana nchi za Africa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…