Serikali imejitahidi sana kuboresha huduma za afya Nchini, kuna huduma za kibingwa zinazotolewa hapa nchini, ambapo miaka 10 nyuma ilikuwa ni ndoto, reffferal za kwenda kutibiwa nje ya Nchi kwa sasa zimepungua sana. miundombinu ya Afya katika Hospitali zetu imeimarika sana, japo bado kunachangamoto ndogo ndogo ambazo zinazidi kupatiwa ufumbuzi.
Changamoto bado ipo kwenye maslahi duni kwa watoa huduma wa Afya, kweli suala la makazi kwa watoa huduma wa Afya bado ni changamoto, wengi wao wanaishi pembezoni mwa miji, na ikitokea dharura (Emergence) hasa nyakati za usiku inakuwa tabu sana kwa mtoa huduma kuwahi kufika Hospitali kumuhudumia mgonjwa kutokakana na umbali.
Nadhani imefika kipindi serikali kuwajengea Nyumba watumishi wa idara ya afya zitakazo kuwa maeneo ya karibu na maeneo yao ya kazi kama inavyofanya kwa kada nyingine , wapewe motisha kuwapunguzia ugumu wa maisha, ili huduma wanazotoa ziwe zenye tija kwa Taifa,
Ukienda Nchi za wenzetu, maslahi ya watu wa Afya wameyapa kipaumbele sana, mtoa huduma anatoa huduma hana stress yoyote ya Maisha.
Kuna utafiti mdogo nimeufanya hapa hapa Nchini, Hospitali zile zinazowajali watumishi wake kwenye suala la maslahi, ndio zinaongoza kutoa huduma nzuri ukilinganisha na zile zisizowajali watumishi wake,
Nchi jirani zimeanza kuleta wagonjwa wao kutibiwa Nchini kwetu kutokana na kuhimarika kwa huduma za Afya Nchini. Tukiwekeza vya kutosha kwenye sekta ya Afya miaka ijayo na sisi tunaweza tukawa kama India kwenye sekta ya Afya.
Miaka ya nyuma Hospitali zilikuwa na makazi ya watoa huduma, sio vibaya ukaanza utaratibu wa kuwajengea makazi watumishi wa Afya,
kwa kufanya hivyo kutawapunguzia kazia wanazokumbana nazo kutokana na umbali, wanaweza wakatumia utaratibu wa kuwakata kwenye mishahara yao kodi za nyumba, kama mdau alivyo shauri hapo juu.
Nchi nyingi za Afrika miundombinu ya Afya iko duni, tutumie hii fursa tunaweza tukaongeza Pato la Taifa kupitia sekta ya Afya, tukichanga vizuri karata tunaweza tukawa tunapokea wagonjwa kutoka katika hizo Nchi.
Serikali iendelee kuwaendeleza watumishi wetu wawe na ubobezi kwenye Huduma za kibingwa. Oparesheni za Moyo sasaivi haina haja ya kwenda india, Upandikizaji wa Figo, Uroto, nk zinafanyika nchini kwetu, huduma za Kutibu kansa kwa kutumia mionzi zinapatika nchini tena bure, haya yote yaendane sambamba na uboreshwaji wa Maisha ya watumishi wa afya
"Healthy nation is a wealthy nation"