Ningekuwa na dhamana, nyumba za Magomeni Kota wangeishi wafanyakazi wa Hospitali ya Muhimbili na Magomeni

Umesahau kuwa imejenga Kodi yetu sio nyie mliojenga hizo nyuma. Kodi yetu ingetumika vizuri kama watumishi kama hospital na wengine wangekaa hapo ili watuhudumie sisi vizuri, yaani Kodi yetu ingeturudia sisi sote kwa kupata huduma Bora. Sasa hivi ni kama Kodi yetu inahudumia wahunii wachache kwa manufaa Yao.
 
Pale penyewe wahindi walisha tunyanganya kwa kupitia waziri Tibaijuka kosa magufur kutumia ubabe Leo hii Manji pangekuwa kwake
Zile nyumba za NHC zilijengwa na wahindi, ni zao tuliwanyang'anya kimabavu. Badala ya kuboresha makazi ya wananchi sisi rukawa bize na kukumboa Bara la Afrika.
 
Kwa cost ya kukaa pale
Wale wenzangu na mie
Watajichekecha wenyewe

Ova
 
Tatizo siyo kujenga, shida inakuja nyumba walizojengewa wafanyakazi wa mashirika
Zinauzwa kinyemela

Ova
 
Waje na kota za kinondoni manyanya pale
Wavunje yale mauchafu wasimamishe uyogaa tu

Ova
 
Unamaslah napo muhimbili ndo hospital pekee??? Au na ww n mfanyakazi wa hapo???? Vp kuhusu magereza??? Polisi??? Walimu????
Sina shida kama zingepewa watumishi wa aina yoyote bila kujali fani yao. Lakini zile pale zilikuwa ni nyumba za watumishi basi zingeendelea kuwa nyumba za watumishi wa taasisi ambazo ziko karibu na eneo lile. Mtu anaweza kuhama lakini taasisi hazihami, huwezi kuuza nyumba au eneo lililo karibu na taasisi ya kudumu kama Muhimbili, Mwananyamala, Magomeni Health Center, Jangwani Sekondari, nk
 
Zile nyumba za NHC zilijengwa na wahindi, ni zao tuliwanyang'anya kimabavu. Badala ya kuboresha makazi ya wananchi sisi rukawa bize na kukumboa Bara la Afrika.

Kwa kweli kwenye kukomboa Africa tulipoteza sana kama Taifa, halafu mwisho wake anatukuzwa Mandela.!
 
Kule ngorongoro wale wavamizi inabidi waondolewe waachwe wenyeji
 
Muhimbili kwanini wasijenge?
 
Tanzania ni maskini sana hatuna luxury ya kutumia kodi za wananchi kujengea nyumba watu wa kawaida kama wale wa magomeni kota wakati watoa huduma kama wa afya, elimu, polisi, jeshi, zimamoto ambao wanatakiwa kuhudumia watanzania wenzao 24 h hawana nyumba wala usafiri wa haraka wa kuwafikisha sehemu ya kazi kwa wakati. Kuna mtu ninamfahamu anaamka saa 9 usiku ili aanze safari ya kwenda kazini saa 10.30 ili afike Muhimbili saa 1 asubuhi na anafika nyumbani saa 3 usiku kila siku kutoka kazini. Mtu kama huyu ukimwambia atabasamu kwa mteja ni kumuonea tu.
 
wananchi wakawaida nao wanastahiki kula keki ya taifa. SIo kila kitu kipaumbele kiwe kwa viongozi na watumishi wa serekali tu.
 
wananchi wakawaida nao wanastahiki kula keki ya taifa. SIo kila kitu kipaumbele kiwe kwa viongozi na watumishi wa serekali tu.
Shida ya mtumishi ni kwamba wewe unahitaji akuhudumie wewe vizuri na kwa wakati. Hutakubali jino linakuuma sana halafu unaambiwa dk wa meno hajafika kazini. Au mwanamke kashikwa na uchungu wa kuzaa usiku halafu mkunga Yuko mbali na hospitali. Hii ni tofauti na machinga, mkulima, mfugaji au mvuvi baharini hata kama hajaenda kuvua hakuna atakae kulaumu Wala kuathirika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…