Ningekuwa na dhamana, nyumba za Magomeni Kota wangeishi wafanyakazi wa Hospitali ya Muhimbili na Magomeni

Ningekuwa na dhamana, nyumba za Magomeni Kota wangeishi wafanyakazi wa Hospitali ya Muhimbili na Magomeni

Kama wewe ni mtu wa maendeleo basi tafuta fikra zingine za kimaendeleo na sio kizoba zoba ebo!

Yaani ujenge kanisa and then likiisha isha unasema bora waswalie baniani? kwanini usijenge nyumba za watumishi wa hospital huko huko kwenye maeno ya Hospital Muhimbili nakumbuka zipo nyumba za wafanyakazi labda hazitoshi... Ingekuwa labda hizo Hospital hazizalishi na ni za wito tu labda kahuruma kangekuwepo... and pale Buguruni kuna maflati ya wafanyakazi wa Muhimbili pia
Umesahau kuwa imejenga Kodi yetu sio nyie mliojenga hizo nyuma. Kodi yetu ingetumika vizuri kama watumishi kama hospital na wengine wangekaa hapo ili watuhudumie sisi vizuri, yaani Kodi yetu ingeturudia sisi sote kwa kupata huduma Bora. Sasa hivi ni kama Kodi yetu inahudumia wahunii wachache kwa manufaa Yao.
 
Pale penyewe wahindi walisha tunyanganya kwa kupitia waziri Tibaijuka kosa magufur kutumia ubabe Leo hii Manji pangekuwa kwake
Zile nyumba za NHC zilijengwa na wahindi, ni zao tuliwanyang'anya kimabavu. Badala ya kuboresha makazi ya wananchi sisi rukawa bize na kukumboa Bara la Afrika.
 
Utaratibu unaomba kwa kujaza fomu manispaa na tayari zilishajaa miezi 3 ya nyuma ila kama ulikuwa mkazi wa pale kabla ya zile ghorofa hazijajengwa unapewa apartment ambayo wameambiwa mwenye uwezo aanze kulipia ili ainunue .changamoto kubwa pale kwa sasa kwenye yale maghorofa itakayowakabili wakazi wa takaoishi mule ndani itawalazimu kuchangia operation cost ambayo ni lift, umeme,mlinzi na mengineyo kitu ambacho wengi watashindwa na wameambiwa ukishindwa hutakiwi kupangisha rudisha funguo nafikiri hii ni janja ya kuwaondoa kisayansi au kiuchumi ukizingatia wakazi wengi wa asili walishafariki na wengine wameshachoka kimaisha kutokanana uzee au ukwamo wa kiuchumi.
Kwa cost ya kukaa pale
Wale wenzangu na mie
Watajichekecha wenyewe

Ova
 
Kama wewe ni mtu wa maendeleo basi tafuta fikra zingine za kimaendeleo na sio kizoba zoba ebo!

Yaani ujenge kanisa and then likiisha isha unasema bora waswalie baniani? kwanini usijenge nyumba za watumishi wa hospital huko huko kwenye maeno ya Hospital Muhimbili nakumbuka zipo nyumba za wafanyakazi labda hazitoshi... Ingekuwa labda hizo Hospital hazizalishi na ni za wito tu labda kahuruma kangekuwepo... and pale Buguruni kuna maflati ya wafanyakazi wa Muhimbili pia
Tatizo siyo kujenga, shida inakuja nyumba walizojengewa wafanyakazi wa mashirika
Zinauzwa kinyemela

Ova
 
Waje na kota za kinondoni manyanya pale
Wavunje yale mauchafu wasimamishe uyogaa tu

Ova
 
Unamaslah napo muhimbili ndo hospital pekee??? Au na ww n mfanyakazi wa hapo???? Vp kuhusu magereza??? Polisi??? Walimu????
Sina shida kama zingepewa watumishi wa aina yoyote bila kujali fani yao. Lakini zile pale zilikuwa ni nyumba za watumishi basi zingeendelea kuwa nyumba za watumishi wa taasisi ambazo ziko karibu na eneo lile. Mtu anaweza kuhama lakini taasisi hazihami, huwezi kuuza nyumba au eneo lililo karibu na taasisi ya kudumu kama Muhimbili, Mwananyamala, Magomeni Health Center, Jangwani Sekondari, nk
 
Zile nyumba za NHC zilijengwa na wahindi, ni zao tuliwanyang'anya kimabavu. Badala ya kuboresha makazi ya wananchi sisi rukawa bize na kukumboa Bara la Afrika.

Kwa kweli kwenye kukomboa Africa tulipoteza sana kama Taifa, halafu mwisho wake anatukuzwa Mandela.!
 
Kwahiyo kule ngorongoro kuwaondoa baadhi ya watu kupisha uhifadhi ni kubagua watu na kutukuza wanyama au ni vipaumbele TU vya taifa? Wangepewa eneo lingine ili lile la Magomeni kota kwasababu za kijiogorafia wapewe watumishi wa Muhimbili, Magomeni na mwananyamala.
Kule ngorongoro wale wavamizi inabidi waondolewe waachwe wenyeji
 
Unapotamani mfanyakazi wa hospitali a-smile kwa mgonjwa kuna mambo mengi sana lazima afanyiwe kabla ya kukutana na wagonjwa. Miongoni mwa mambo hayo ni mahali pa kuishi karibu na hospitali.

Wafanyakazi kazi wa Muhimbili pale wanaishi mbali sana, wanatoka na kurudi usiku sana kutoka na kufika na nyumbani na hospitali respectively. Nguvu na tabasabu zao zote zinaishia barabarani wakati wa kwenda na kurudi kazini.

Kwanini serikali isingefikiria kuwapa nyumba zile au kuwajengea watumishi wa afya nyumba kama zile karibu na hospitali? Tumeona maghorofa kwaajili ya askari, watumishi wa afya je?

Mtumishi wa afya anatoka Chanika kwenda Muhimbili kila siku, utategemea nini anapokutana na mgonjwa? Amechoka, anasinzia na ana njaa.

Vipaumbe vyetu vyote vimekaa kisiasasiasa na kiuchaguzichaguzi, tutachelewa sana.
Muhimbili kwanini wasijenge?
 
Tanzania ni maskini sana hatuna luxury ya kutumia kodi za wananchi kujengea nyumba watu wa kawaida kama wale wa magomeni kota wakati watoa huduma kama wa afya, elimu, polisi, jeshi, zimamoto ambao wanatakiwa kuhudumia watanzania wenzao 24 h hawana nyumba wala usafiri wa haraka wa kuwafikisha sehemu ya kazi kwa wakati. Kuna mtu ninamfahamu anaamka saa 9 usiku ili aanze safari ya kwenda kazini saa 10.30 ili afike Muhimbili saa 1 asubuhi na anafika nyumbani saa 3 usiku kila siku kutoka kazini. Mtu kama huyu ukimwambia atabasamu kwa mteja ni kumuonea tu.
 
wananchi wakawaida nao wanastahiki kula keki ya taifa. SIo kila kitu kipaumbele kiwe kwa viongozi na watumishi wa serekali tu.
 
wananchi wakawaida nao wanastahiki kula keki ya taifa. SIo kila kitu kipaumbele kiwe kwa viongozi na watumishi wa serekali tu.
Shida ya mtumishi ni kwamba wewe unahitaji akuhudumie wewe vizuri na kwa wakati. Hutakubali jino linakuuma sana halafu unaambiwa dk wa meno hajafika kazini. Au mwanamke kashikwa na uchungu wa kuzaa usiku halafu mkunga Yuko mbali na hospitali. Hii ni tofauti na machinga, mkulima, mfugaji au mvuvi baharini hata kama hajaenda kuvua hakuna atakae kulaumu Wala kuathirika
 
Back
Top Bottom