Ningekuwa na dhamana, nyumba za Magomeni Kota wangeishi wafanyakazi wa Hospitali ya Muhimbili na Magomeni

Ningekuwa na dhamana, nyumba za Magomeni Kota wangeishi wafanyakazi wa Hospitali ya Muhimbili na Magomeni

Unamaslah napo muhimbili ndo hospital pekee??? Au na ww n mfanyakazi wa hapo???? Vp kuhusu magereza??? Polisi??? Walimu????
 
Serikali imejitahidi sana kuboresha huduma za afya Nchini, kuna huduma za kibingwa zinazotolewa hapa nchini, ambapo miaka 10 nyuma ilikuwa ni ndoto, reffferal za kwenda kutibiwa nje ya Nchi kwa sasa zimepungua sana. miundombinu ya Afya katika Hospitali zetu imeimarika sana, japo bado kunachangamoto ndogo ndogo ambazo zinazidi kupatiwa ufumbuzi.

Changamoto bado ipo kwenye maslahi duni kwa watoa huduma wa Afya, kweli suala la makazi kwa watoa huduma wa Afya bado ni changamoto, wengi wao wanaishi pembezoni mwa miji, na ikitokea dharura (Emergence) hasa nyakati za usiku inakuwa tabu sana kwa mtoa huduma kuwahi kufika Hospitali kumuhudumia mgonjwa kutokakana na umbali.

Nadhani imefika kipindi serikali kuwajengea Nyumba watumishi wa idara ya afya zitakazo kuwa maeneo ya karibu na maeneo yao ya kazi kama inavyofanya kwa kada nyingine , wapewe motisha kuwapunguzia ugumu wa maisha, ili huduma wanazotoa ziwe zenye tija kwa Taifa,
Ukienda Nchi za wenzetu, maslahi ya watu wa Afya wameyapa kipaumbele sana, mtoa huduma anatoa huduma hana stress yoyote ya Maisha.

Kuna utafiti mdogo nimeufanya hapa hapa Nchini, Hospitali zile zinazowajali watumishi wake kwenye suala la maslahi, ndio zinaongoza kutoa huduma nzuri ukilinganisha na zile zisizowajali watumishi wake,
Nchi jirani zimeanza kuleta wagonjwa wao kutibiwa Nchini kwetu kutokana na kuhimarika kwa huduma za Afya Nchini. Tukiwekeza vya kutosha kwenye sekta ya Afya miaka ijayo na sisi tunaweza tukawa kama India kwenye sekta ya Afya.

Miaka ya nyuma Hospitali zilikuwa na makazi ya watoa huduma, sio vibaya ukaanza utaratibu wa kuwajengea makazi watumishi wa Afya,

kwa kufanya hivyo kutawapunguzia kazia wanazokumbana nazo kutokana na umbali, wanaweza wakatumia utaratibu wa kuwakata kwenye mishahara yao kodi za nyumba, kama mdau alivyo shauri hapo juu.

Nchi nyingi za Afrika miundombinu ya Afya iko duni, tutumie hii fursa tunaweza tukaongeza Pato la Taifa kupitia sekta ya Afya, tukichanga vizuri karata tunaweza tukawa tunapokea wagonjwa kutoka katika hizo Nchi.

Serikali iendelee kuwaendeleza watumishi wetu wawe na ubobezi kwenye Huduma za kibingwa. Oparesheni za Moyo sasaivi haina haja ya kwenda india, Upandikizaji wa Figo, Uroto, nk zinafanyika nchini kwetu, huduma za Kutibu kansa kwa kutumia mionzi zinapatika nchini tena bure, haya yote yaendane sambamba na uboreshwaji wa Maisha ya watumishi wa afya

Mkuu Sijui Nchi gani za ulaya unazungumzia. Ni ngumu sana wa watoto wa kijerumani kusomea unurse na Hospital nyingi zina watu wa nje (Ausländer) na wanasema kuwa kazi nyingi zisizoendana na kipato.

Msipende kufanya comparison tu, kwanza anzeni kushauri njia za mapato. Bajeti kubwa inategemea ufadhili Unawezaje kuwa na mishahara mikubwa. Ni rahisi kufanya projects kwa kuwa sio Life Time Engagement. Tanzania ni third world country Jamani. Hizi internet zisiwafanye mjione Sawa na Marekani.
 
Mwambie mama ajenge zingine.
Issue sio kujenga nyingine bali kujenga nyingine karibu na hospitali. Kama kule ngorongoro wamasai wanahamishwa kupisha tembo na nguruwe pori wakae kwanini wakazi wa Magomeni hawakuhamishiwa sehemu nyingine ili kupisha watumishi wa taasisi za umma wakae karibu na maeneo ya utoaji huduma ili kuimarisha ubora wa utoaji huduma kwenye taasisi zetu? Mfanyakazi anatoka nyumbani usiku kuwahi kazini na anafika nyumbani usiku kutoka kazini kila siku. Hii nayo inahitaji elimu kubwa kiasi gani kuifikiria?
 
Lipa Kodi
Hata wakoloni wametushinda kufikiria na kupanga, hizo nyuma zilikuwa za watumishi wakati wa mkoloni Leo hii baada ya miaka 60 ya Uhuru nyumba hizohizo wanapewa watu wa kawaida mtaani na kuwaacha watumishi kila mmoja ajijue mwenyewe, nadhani tumewahi mno kudai uhuru kabla ya kujiandaa. Mzee karume miaka 60 iliyopita alifikiria sio kuwapatia watumishi makazi bali kuwapatia watu wake wote makazi . Angeishi hadi Leo yule Mzee Zanzibar isingekamatika.
 
Issue sio kujenga nyingine bali kujenga nyingine karibu na hospitali. Kama kule ngorongoro wamasai wanahamishwa kupisha tembo na nguruwe pori wakae kwanini wakazi wa Magomeni hawakuhamishiwa sehemu nyingine ili kupisha watumishi wa taasisi za umma wakae karibu na maeneo ya utoaji huduma ili kuimarisha ubora wa utoaji huduma kwenye taasisi zetu? Mfanyakazi anatoka nyumbani usiku kuwahi kazini na anafika nyumbani usiku kutoka kazini kila siku. Hii nayo inahitaji elimu kubwa kiasi gani kuifikiria?
Hayo ni mawazo mgando.Kama tukiwa na mawazo Kama ya kwako,tutafika tumechoka.Pale Muhimbili Kuna nyumba za wafanyakazi .Kama hazitoshi nyumba nyingine ,Kama kukiwa na nafasi zaweza kujengwa sehemu yeyote Dsm.Kuna miundo mbinu ya kutosha ,Kama usafiri ambao unaweza kuwasaidia kufika kazini mapema.
 
Unapotamani mfanyakazi wa hospitali a-smile kwa mgonjwa kuna mambo mengi sana lazima afanyiwe kabla ya kukutana na wagonjwa. Miongoni mwa mambo hayo ni mahali pa kuishi karibu na hospitali.

Wafanyakazi kazi wa Muhimbili pale wanaishi mbali sana, wanatoka na kurudi usiku sana kutoka na kufika na nyumbani na hospitali respectively. Nguvu na tabasabu zao zote zinaishia barabarani wakati wa kwenda na kurudi kazini.

Kwanini serikali isingefikiria kuwapa nyumba zile au kuwajengea watumishi wa afya nyumba kama zile karibu na hospitali? Tumeona maghorofa kwaajili ya askari, watumishi wa afya je?

Mtumishi wa afya anatoka chanika kwenda Muhimbili kila siku, utategemea nini anaokutana na mgonjwa? Amechoka, anasinzia na ana njaa.

vipaumbe vyetu vyote vimekaa kisiasasiasa na kiuchaguzichaguzi, tutachelewa sana.
Vipi kuhusu walimu?
 
Unamaslah napo muhimbili ndo hospital pekee??? Au na ww n mfanyakazi wa hapo???? Vp kuhusu magereza??? Polisi??? Walimu????
Wewe na Mimi wote ni wadau wa Muhimbili National Hospital. Hii ndiyo hospital kuu ya watu wote tunaenda huko kutibiwa. Kuhudumiwa na mfanyakazi ambae hajui anafikaje na kurudije kazini ni hatari sana. Unaposikia mgonjwa wa kichwa kapasuliwa mguu na yule wa mguu kafanyiwa upasuaji wa kichwa ni mambo kama haya. Unanunua MRI sawa lakini anaeiendesha MRI huna habari nae.
 
Waambie wanaoishi upanga waondokrbwaache kupanga, au sema kupanga kusizidi miaka 20 NHC.upanga wote wamepanga zaidi ya miaka 50 akiwemo akina ......
 
kavulata una interest binafsi temeke , mwananyamala , mbagala , mloganzila katila hospital hizo zote hakuna wanaofanya opareshen??? Bugando?? Kcmc?? Na nyingnezo nying
 
kavulata una interest binafsi temeke , mwananyamala , mbagala , mloganzila katila hospital hizo zote hakuna wanaofanya opareshen??? Bugando?? Kcmc?? Na nyingnezo nying
Bugando, kcmc Wana nyumba nyingi sana za wafanyakazi.
 
Mi nauliza swali hao wananchi wa Magomeni wamepewa bure hayo magorofa au wanalipa kodi kila mwezi?
 
Wasemee na wewe. Nafahamu wale wa hospital kwakuwa huwa Wana zamu za usiku pia, pia wanaweza kujitajika kazini kwa dharura wakati wowote.
Kila mfanyakazi ana umuhimu wake kutokana na taaluma yake chief,na kuna Nyumba nyingi tu Tanzania zimetengwa kwa ajiri ya madaktari,hilo la kuwa na zamu usiku madaktari ni sehemu ya ratiba ya kazi zao na wala haiwezi kuwa justification ya wao kuonewa huruma ya kupewa hizo nyumba za Magomeni.
 
Watu wote ni sawa lakini heshima ya mtu kwenye jamii haitatokana na kufanana kwake na binadamu, umri wake, jinsia yake, elimu wala chama Cha siasa chake, bali heshima yake itatokana na aina ya huduma yake kwa jamii na namna anavyoihudumia jamii.

Kwa watu ambao jamii inatarajia iwaone na kuwakuta ni Wasafi, wacheshi, Wana afya, wanachekea, wanafariji, wanaponya, wanaokoa na kuhifadhi faragha zao muda wote siku zote na milele lazima mambo fulani lazima wapewe. Matamanio hayo lazima Yana gharama zake.

Zile nyumba pale wamepewa kuishi hata vibaka, makahaba na wachekeshaji ambao kazi zao hazihitaji mambo mengi sana. Wengine ni kuamka na kunywa kahawa na wengine wanalala mchana usiku wanaenda kukaba watu.

Naungana na mama Samia kuwa watu wale hawakustahili kukaa mule kutokana na vipato na akili zao ndogo, watatwangia visamvu na kupikia kuni, wengine wameshaanza kulalamika kuwa hawakuwekewa kamabati ya kuweka matambara Yao.
Tumia tena akili kufikili usimbague mtu kwa ajiri ya elimu yake na wadhifa wake
 
Tumia tena akili kufikili usimbague mtu kwa ajiri ya elimu yake na wadhifa wake
Kwahiyo kule ngorongoro kuwaondoa baadhi ya watu kupisha uhifadhi ni kubagua watu na kutukuza wanyama au ni vipaumbele TU vya taifa? Wangepewa eneo lingine ili lile la Magomeni kota kwasababu za kijiogorafia wapewe watumishi wa Muhimbili, Magomeni na mwananyamala.
 
Kama wewe ni mtu wa maendeleo basi tafuta fikra zingine za kimaendeleo na sio kizoba zoba ebo!

Yaani ujenge kanisa and then likiisha isha unasema bora waswalie baniani? kwanini usijenge nyumba za watumishi wa hospital huko huko kwenye maeno ya Hospital Muhimbili nakumbuka zipo nyumba za wafanyakazi labda hazitoshi... Ingekuwa labda hizo Hospital hazizalishi na ni za wito tu labda kahuruma kangekuwepo... and pale Buguruni kuna maflati ya wafanyakazi wa Muhimbili pia
 
zile nyumba kuishi mule utaratibu upo vp wakuu
 
zile nyumba kuishi mule utaratibu upo vp wakuu
Utaratibu unaomba kwa kujaza fomu manispaa na tayari zilishajaa miezi 3 ya nyuma ila kama ulikuwa mkazi wa pale kabla ya zile ghorofa hazijajengwa unapewa apartment ambayo wameambiwa mwenye uwezo aanze kulipia ili ainunue .changamoto kubwa pale kwa sasa kwenye yale maghorofa itakayowakabili wakazi wa takaoishi mule ndani itawalazimu kuchangia operation cost ambayo ni lift, umeme,mlinzi na mengineyo kitu ambacho wengi watashindwa na wameambiwa ukishindwa hutakiwi kupangisha rudisha funguo nafikiri hii ni janja ya kuwaondoa kisayansi au kiuchumi ukizingatia wakazi wengi wa asili walishafariki na wengine wameshachoka kimaisha kutokanana uzee au ukwamo wa kiuchumi.
 
MSHAANZA CHOKOCHOKO ACHA WANANCHI WA KAWAIDA NAO WAFAIDI KUKAA GOROFANI.
HAO WATUMISHI WAKAISHI NHC PALE WAWATOE WAHINDI
Pale penyewe wahindi walisha tunyanganya kwa kupitia waziri Tibaijuka kosa magufur kutumia ubabe Leo hii Manji pangekuwa kwake
 
Back
Top Bottom