Ningekuwa na mamlaka Simba ningewafukuza Masoud na Manara

upakoo

Senior Member
Joined
Mar 30, 2018
Posts
101
Reaction score
70
Kiukweli nakereka sana kwa namna soka la TZ linavyovurugwa na washenzi wachache wanaojitia wanajua soka, uswahili wa masoud na manara ni tatizo kwa soka letu ni watu wapuuzi mnoo hawafai kabisa ila wanalazimisha waonekane wapo vizuri,hawana lolote zaidi ya usaka tonge
 
Nakuunga mkono mkuu, hasa huyo Manara. Anatuvurugia team na kujiona mkubwa zaidi ya team iliyompa huo ukubwa anaojivunia. Namwambia: NJE YA SIMBA HANA UMAARUFU ANAODHANI ANAO. Atulize akili, afanye kazi anayopaswa kufanya na si kujenga makundi na vijembe vya kitoto mitandaoni. Kuna haja ya kukifumua na kuliunda upya kitengo cha habari na mawasiliano maana hiki ndo Image ya Club, hakiwezi kuwa na mtu wa ovyo ovyo.
 
Manara na huyo mshenzi masoud wanatuchezea ngoma ya sindimba hawana lolote
 
Wakuu tatizo la "De Le Boss" Manara ni lipi haswaa??
Kazi ya De Le Boss ni afisa habari na mawasiliano, na moja ya jukumu lake kuu ni kuhakikisha habari za timu zinawafikia walengwa kwa wakati muafaka. Na hapa anafanya vyema sana.
Kuhusu vijembe anavyotoa katika mitandao ya kijamii mi naona ni sawa tu kwa sababu anayafanya yote hayo katika page zake na si za timu.

NB: Alafu Simba SC ni Brand kubwa.. Inahitaji kua na Afisa habari mwenye makeke kama De Le Boss, Manara na si aliyepooza kama wa Ndala.
 

Brand kubwa inaitaji kitengo cha mawasiliano kilichotulia hili kilinde brand ya timu.
 
Manara keshasema Washabiki Wa Simba hamjui mpira Bali mmejazana tu kwenye magroup ya Whatsap sahizi naona mmehamia na JF mnajadili mambo ya mpira msiyoyajua. Jamaa akipaniki huwa anaongea ukweli
Aisee mkuu jifunze soka acha taarabu
 
Haji Manara kafanya kazi kubwa pia kuamsha hamasa ya mashabiki kuependa timu yao na ndo mana hivi sasa.. Kila Mnyama akiingia uwanjani, uwanja lazima ujae hadi pomoni, na hii ni kazi ambayo aliifanya kwa misimu miwili au mitatu iliyopita. Tumpe heshima yake.

Alafu timu hizi kubwa (Simba na 'mdogo wake' Ndala) zinahitaji maafisa habari wa kariba ya De Le Boss, Manara. Angalia Ndala baada ya kuondoka Muro, morali imeshuka miongoni mwa mashabiki. Just imagine Lipuli ikicheza inaingiza mashabiki wengi kuliko Ndala, kwa kifupi li timu la Ndala lipo lipo tu, halieleweki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…