Ningekuwa na mamlaka Simba ningewafukuza Masoud na Manara

Hizi timu kwa sababu ni za kiswahili swahili hazina budi kuwa na wasemaji kama manala,maneno mengi vitendo sifuri
 
ahaahaaa mkuu nimecheka kwa sauti sana
Yaani mkuu hizi timu bila wasemaji wa namna hiyo hatufiki maana waswahili tunapenda maneno,na manara analijua hilo ndiyo maana ni miongoni mwa wasemaji waliokaa muda mrefu msimbazi pia ni mhamasishaji yaani ni pr mzuri sana,kitendo cha kujaza uwanja sio mchezo
 
Unamfukuzaje manara anayekuingizia zaidi ya milioni 200 kwa mechi moja refer mechi ya simba day msimu uliopita na msimu huu mdomo wake umechangia sana kuingiza fedha hizo,manara anaangushwa na wachezaji pia na uongozi ila kiuhalisia kipaji chake kikitumika kwa manufaa ya klabu nadhani hata kauwanja ka mazoezi katajengwa
 
wewe ndiye Manara mwenyewe ndio maana unatetea ugali wako!!!
 
Umelieleza vyema sana hili suala.. Nadhani limeeleweka.
 
wewe ndiye Manara mwenyewe ndio maana unatetea ugali wako!!!
Mkuu, unataka kusema wanachama wote wa Simba hawamtaki Manara? Kama, jibu ni hapana.. kwanini mimi nisiwe mmoja wapo nayekubali anachokifanya?
 
Umeshindwa hata kutaja makosa yao. Kwa sisi tusioona shida kwao tusaidie kujua. Masoud ana kosa gani?Haji anakosa gani?tukisema una chuki binafsi. Anayepanga kikosi ni kocha. Wajinga wachache wanasema Haji ana-overrate timu,huu ni usenge mbichi. Unataka Haji aseme timu yetu mbovu au ya kawaida?si wehu huu,taja kiongozi anaye underrate timu yake,hats kama ni ya Ndondo
 
Mourinho
 
Wewe kaa kimya hujui historia ya hizi timu. Yaani huna habari wala kutambua kuwa Simba fc ni ubavu was Yanga sport club kama ilivyo kwa Hawa alivyo ubavu was Adam, na Mke alivyo ubavu was Mwanaume. Nimejaribu kukujuza ili ujue we we na Simba yako mlitokea wapi.
 
Manara keshasema Washabiki Wa Simba hamjui mpira Bali mmejazana tu kwenye magroup ya Whatsap sahizi naona mmehamia na JF mnajadili mambo ya mpira msiyoyajua. Jamaa akipaniki huwa anaongea ukweli
Hahahaha Kwa hiyo huo ndio ukweli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…