MAMBO MUHIMU KWA UJUMLA
1. Punguza kodi na kodi zijulikane wazi: Mlipa kodi yeyote hatakiwi kusubiri mpaka mzigo ufike bandarini kujua ni kodi gani alipe. Hii inapunguza biashara, inapunguza idadai ya watu kuleta vitu n ahata inapunguza upelekaji wa vitu nje. Kodi inabidi ziwe rahisi sana kujulikana na kusiwe na tabia ya makisio ya kodi. Kodi itokane na receipt kama wenzetu hii inaongeza ushindani kama nimepata gari kwa bei rahisi haina maana wote tena tulipe kodi sawa maana kodi inatakiwa kutokana na kiasi nilicholipa. Hii inachochoe ushindani.
Vilevile kodi zipo juu sana hivyo angalieni vitu ambavyo vina add value mfano gari ikiingia moja kuna kodi nyingine nyingi itachangia mafuta, matairi, spare, road tax….. hivyo kupunguza kodi ya magari inafaida kubwa kwa miaka mingi kuliko kukosa kodi au kupata mara moja kubwa kwa magari machache
2. Rahisisha kufungua biashara. Haitakiwi mtu anafungua biashara kwa pesa yake na serikali inafanya tena iwe ngumu kufungua na iwe na bei. Pesa inatakiwa kwenye kwenye biashara.
3. Punguza kodi au ondoa kabiasa kwenye vifaa vya ujenzi kama mbao. Kama tunataka kuweka mazingira yetu sawa na tusikate miti tutoe kodi kwenye mbao ambazo ziko juu sana.
4. Rahisisha utoaji wa vibali vya ujenzi kuwa rahisi
5. Ingiza technologia kwenye masomo. Technologia ikitumika vizuri inaweza kufanya watoto wetu waweze kusoma zaidi kwa bei nafuu yaani kuna vitabu vingi sana vya bure lakini unahitaji mtandao. Hii ni sababu kubwa sana watoto wetu wako nyuma kielimu.
6. Shughulikia swala la umeme rahisi na wa uhakika
7. Achana na upinzani haisaidii nchi kulumbana kuhusu mikutano yeyote aongee chochote . Watu mwishoni watajali maendeleo maneno mazuri yawe ya CCM au CUF hayasaidii ni maendeleo tu. Mfano wa Zanzibar kwasababu maendeleo hayakuweko kila uchanguzi kwa miaka 15 Seif amekuwa akishinda… issue ni maendeleo tu.
Kugombana na upinzani kumepunguza sana sifa yaserikali bila kuongeza chochote cha msingi. Vyombo vyetu wa sheria haviheshimiki kama zamani tena. Kutoka moyoni tunaomba haya muache hayasaidii kabisa
8. Kwenye Afya anzisheni mobile medical: Yaani team ya Dr mbalimbali wanatembea kwenye magari maalumu na kupima, kutoa matibabu mbalimbali. Hatutaweza kujenga Medical Center kila mahali na kuwa na Dr kila mahali kwenye nchi kubwa kama Tanzania. Tusiige Europe wana mazingira tofauti. Kuna mpaka mobile CT, Xrays….., kama ni lazima. Wana set camp kwa muda vijijini. Tujue magojwa mengi ni elimu, chanjo na dawa tu hasa za kisukari na pressure…
9. Ajirini watu wenye ujuzi kuliko wenye elimu. Kuna watu wengi serikalini wana elimu lakini hawana ujuzi. Unaweka wakuu wa TRA kwenye kodi za biashara wakati hawajawahi kufanya biashara, hawajui uchungu wa wafanyabiashara na hali halisi. Ni vizuri mtafute watu ambao ndiyo wawe wasomi lakini hasa wawe wafanyabiashara watawasaidia kuongeza ukusanyaji na urekebishaji wa kodi. Hawa mara nyingi watawapa mpaka mawazo ya ushindani wa nje
10. Bank ni tatizo. Mikopo iko juu sana kwenye riba. Serikali iweke gurantee kupunguza gharama za mikopo, serikali iache kukopa ndani. Lakini wekeni system ya credit rating, vitambulisho vya taifa etc kukuza uhakiki wa watu ili kupunguza risk za bank.
Ardhi/Land: Tuanche sheria za kisifa yaani mfano sasa hivi ukienda kununua shamba pori bagamoyo halafu ukasafisha na kuanza kulima ndiyo uvamizi na wanakijiji wanataka sehemu yako. Wanasiasa kwa sifa wanaweza kuchukua sehemu yako wakati kuna vichaka kibao. Hii
TATIZO LA MIKOPO
Mimi kama diaspora nitaanza na mawazo mawili makubwa halafu naomba wadau muongeze
1. Nashauri Mabalozi ambao wanateuliwa wapimwe uwezo sio tu kuchagua watu ambao ni madiplomasia wa wizarani na ofisi zetu za balozi lakini kuchagua watu ambao wanauzoefu wa biashara, uwekezaji na ushawishi. Tunahitaji wafanyabiashara, diaspora, na watu ambao wamewahi kuongoza biashara kubwa kama banks kuwa mabalozi. Tumechoka watu ambao wanaenda kujifunza kazi na wengi wa mabalozi ni slow sana na hawajui majukumu yao vizuri.
2. Balozi zote ziunde group za ushauri kwa ubalozi-Tanzania. Group hizi ziwe ni wataaalamu tofauti Watanzania au wadau wanaopenda maendeleo ya Tanzania. Mfano kwa hapa USA na Canada ambako mimi nina makazi kuwe na washauri wa mambo ya technologia, elimu, afya, ujenzi, ushirikiano na uwekezaji. Uzuri wa hizi group wadau ambao ni wataalamu watatoa ushauri bure lakini kwa kuhakikisha ushauri unatolewa moja kwa moja kwa balozi na wenyewe kupeleka Tanzania.
Lakini hizo group vilevile kama kuna mtu anataka kuwekeza wanakuwa na uwezo kufanya mikutano moja kwa moja na wahusika kwa kutumia zoom meetings za kimkakati.
Hii inasaidia kwennye kutoa misaada Tanzania, kuongeza utaalamu na ushauri na kuongeza umoja. Tatizo la sasa balozi zetu zimekuwa zinasubiri badala ya wenyewe kuwa wadau wa kwanza wa kuanzisha group. Mfano Balozi badala ya kukimbilia kuandikisha majina ya diaspora wangetakiwa kuanzisha group hizi totafuti kwa kupitia wenyeviti wa jumuia za watanzania ambao wapo kija mji mkubwa.
Ingeweza ikawa website, wahatapp groups ... lakini lengo ni kutoa ushauri, kuongeza uwekezaji na misaada. Hizi group zitakuwa kama vyama ambapo uongozi ndani ya haya makundi unaweza ukawa na ukomo wake ili kutoa fursa za mawazo mapya.
TANESCO
Kuhusu Bwawa la Nyerere: Ukweli ni kwamba Umeme wa Bwawa la Nyerere utatutosheleza lakini sio mwingi kiasi cha kuuza nje. Kuna umeme sasa umefika vijijini, joto la dunia linaongezeka, treni ya umeme, matumizi ya Air condition kuongezeka, viwanda vipya. Mfano viwanda vya chuma na cement vinatumia umeme sana.
TANESCO
TATIZO LA DOLA $
Mawazo yangu ya jinsi ya kutatua tatizo la dollar Tanzania
1. Serikali iongee na kampuni za utalii na kuwaomba walete pesa hapa utaratibu wa sasa watalii wanalipia hotel na karibu kila kitu kabla hawajaja kutalii na pesa karibu zote zinabaki kwenye bank za nje
2. EAC tuharakishe kuwa na pesa moja hii itaongeza nguvu ya hii pesa mpya. Lakini itapunguza sana utumiaji wa dollar
3. Bank ya Tanzania itumie pesa kununua dhahabu ambayo ni nyingi Tanzania. Hii itakuwa rahisi kama tunahitaji dollar zaidi kununua.
4. Tanzania tunatakiwa kuongeza (1) Utengenezaji wa vitu nchini (2) Kuongeza uuzaji wa bidhaa nje ya nchi
5. Tanzania raisisheni utaratibu wa Diaspora kuja na dollar. Kwasasa utaratibu wa passport copy sijui, vitambulisho ili mtu aweze kubadilisha dollar zake unasababisha watu watumie sendwave, world permit na Apps za kutuma pesa na diaspora hawaji na pesa tena kwasababu ya usumbufu wa kubadilisha pesa.
BARUA YANGU KWA VIJANA
Wadogo zangu vijana wa Kitanzania habari zetu. Mimi ni kijana mkubwa 40+ na napenda niwaandikie barua kutoka moyoni kwangu kwa ninayo yaona miaka hii na kwa nchi yetu ya Tanzania. Mambo nitakayo yasema unaweza usayaelewe kwa wakati huu kutokana na umri wako au uzoefu wako kwenye maisha lakini haita kuwa vizuri kila siku kuishia kuwapiga madongo kila siku badala yake huu ni wakati wa kusema kama Kaka.
1. Tanzania ya sasa mwaka huu 2024 ni bora kiuchumi kuliko wakati sisi tuna maliza Form 6 kwa mimi binafsi ilikuwa mwaka 1996 pale Tambaza Secondary. Hivyo asije kutokea mtu akawadanganya kwamba uchumi wa sasa ni mbaya kuliko zamani hii sio kweli.
2. Tanzania bado ni nchi masikini sana pamoja na rasilimali tulizonazo. Mimi nimetembea nchi nyingi sana na nimekuwa naishi nchi tofauti toka mwezi wa nane 1997 hivyo nasema haya kwa kujiamini na uzoefu na sio kwa kubahatisha.
3. Mabadiliko ya tabia nchi ni ya kweli hivyo mazingira ya mvua, mafuriko , kiangazi ni zaidi sasa kuliko miaka ile ya kwetu tukiwa 20's. Hivyo kwenye mipangalio yako tilia hili maanani.
4. Teknologia ni bora sana kwa vyakati zenu kuliko wakati wetu. Ingawa Teknologia kwa vijana wengi hamuitumia kwa faida ya kujiendeleza.
5. Ushindani wa sasa wa kazi, na maarifa kwenu ni mkubwa zaidi maana mnashindana kitaifa na sio Tanzania peke yake lakini vilevile fursa mnazo zaidi ya nyakati zetu.
6. Siasa za Tanzania hazibadilika sana zaidi ya wapinzani kupata nguvu zaidi . Lakini ukweli ni kwamba hatujawahi kubahatika kupata watu kwenye chama chetu tawala ambao wameweka mbele nchi zaidi ya marafiki zao, famillia zao na kundi la wachache viongozi wa vigogo wa kisiasa. Majina kama Kikwete, Mwinyi, Karume, Kinana, Kingunge. Nauye, Makamba., Malecela, Lowassa tumeyasikia kwa miaka zaidi ya 30. Hivyo viongozi wenu wa kisiasa na wabunge hawajawahi kuwajali na hawajali hata sasa kama wanavyo jiaminisha.
Je nawashauri mfanye nini
1. Ushauri wangu wa kwanza . Kila kijana jiulize kwa undani wako unapenda kuwa nani kwenye maisha yako. Usifanye vitu kwa kuiga iga fanya vitu kutoka moyoni.
2. Tumieni teknologia kujiendeleza kiuchumi mfano kutafuta kazi, kuomba mawazo, kutafuta shule, kutengeneza App, kusoma, kutafuta kazi za nje, kumuamini mungu zaidi, kujiunga na makundi ya nje ya nchi ya kimaendeleo n.k. Weka muda maalumu wa kutumia mitandao kwa mambo mengine lakini muda mwingi uwe kwenye maendeleo
3. Ukishajua kitu unachopenda tafuta Mentor. Memntor ni mtu ambaye ni mfano wa wewe unataka kuwa huyu ni mshauri lakini mwenye uzoefu wa kweli. Mfano wewe unataka kuwa mwana siasa basi hata hapa mitandaoni watafute wakina Zitto, Mwigulu na wengine sio lazima wawe maarufu tafuta mmoja mwombe awe mentor wako. Lakini kuna Mentor wa biashara, kilimo, elimu, chochote utakacho. Memntor sio lazima awe Mtanzania. Mimi nipo Texas na kwa asilimia kubwa nimefanikiwa kwa kushauriwa na wazungu ambao kwa wengine wanaweza kuitwa wabaguzi lakini unahitaji mmoja mzuri tu kukushauri na kukutoa.
4. Msikimbilie kuoa. Maisha ya siku hizi na maendeleo ya afya mnakuwa na maisha marefu wengi wenu tumieni muda kutafuta marafiki na watu mtakao endana nao badala ya kukimbia kuona kwa kufikiri umechelewa. Kosa la kukimbia kuoa na kuzaa linaweza kukuharibia ndoto zako.
5. Pesa haitatosha kukupa furaha. furaha utapata kutoka kwa watu na kusaidia watu na sio kuwa na pesa nyingi. Hata pale utakapo pata pesa furaha watu wanapata pale wanapoona watoto wao na ndugu zao wanafurahi na sio pesa yenyewe.
6. Hakuna maisha bila kufanya kazi. Unaweza kupata kazi inallipa sana lakini majukumu nayo yanakuwa makubwa. Muda unakuwa mdogo, kodi nyingi, wafanyakazi wengi kwasabbu kipato kuongezeka mara nyingi gharama za maisha nazo zinaongezeka. Hivyo matatizo hayaishi bali yanahama tu. Hakuna kazi rahisi popote Duniani.
7. Afya zenu nmuhimu sana. Pombe kunywa kwa kiasi, hakikisha unaangalia kila kitu kwenye mwili wako. Mwili ni kama gari ambalo ninaishi mpaka miaka 100 na ni mmoja tu. Gari utanunua lingine lakini mwili wako ni huohuo. Macho ni hayo hayo, miguu ndiyo hiyo hiyo kuwa mwangalifu.
8. Kuweni makini sana na vyakula vya kisasa. Piza, buggers na vyakula vya makopo.
9. Usiogope kutafuta kazi nje ya nchi kwa faida ya famila yako
10. Msisubiri kuletewa maendeleo na serikali tumesubiri kwa miaka 60 sasa!
11. Upinzani pekee sio suluhisho nyie ndiyo mnatakiwa kupigania maendeleo yenu sio vyama vya siasa pekee. Hakuna wa kulaumu kama nyie wenyewe mnaridhika kirahisi na umasikini. Mna nguvu kuliko mnavyojifikiria
12. Kuna wakati kwenye maisha yako pesa na mambo mengine yote hayata weza kukusaidia na wewe kuwa sawa ni lazima uwe na Imani kwa Mungu. Ukifiwa, kuumwa ndiyo utajua hili. Ni lazima uweke imani mbele
13. Achani kuwa fake
14. Uwezo wako uko moyoni kwako. Unajua unaweza sasa kwanini unalalamika sana. Acheni tabila za kulalamika. Mfano kwenye siasa Lissu kapigwa risasi bado ana andamana na sio kulalama pekee.
15. Jiwekee mipango ya maendelo kila mwaka
16. Jiamini na msiogope.
Ka ijumaa hii nitaishia hapo nawatakia siku njema
WAMACHINGA
Watanzania wengi hawajui kwamba Wamachinga hawasaidii nchi yetu badala yake wanatumika kwa siasa pekee. Watanzania wanashangilia wamachinga ambao hawalipi kodi halafu wanalalamika wenyewe kuongezewa kodi!
1. Hawalipi kodi yeyote ya maana na vibali vya machinga ni kama kukejeli Watanzania.
2. Wachafuzi wa mazingira. Hivi hizi gharama za usafi analipa nani hasa kwa watu wasio lipa kodi.
3. Wanauza vitu vya kijinga ambavyo havina msaada wowote wa maana kwa viwanda vyetu wala sera muhimu kama kilimo, elimu au afya.
4. Wanasaidia viwanda vya china sio Tanzania hebu tukaangalie kama vitu vya machinga ni vya Tanzania! Utakuta ni majalala ya kichina hivyo tunasaidia wachina na sio Tanzania.
5. Wanaua wafanyabiashara wadogo ambao wanalipa kodi maana wameweka magenge ambayo hayana mpangilio mbele ya biashara nyingine
KUHUSU KISWAHILI
Kiswahili kinakuwa sana na Tanzania tunapata heshima sana kwa lugha yetu hii. Hii naina maana tusifundishe watoto wetu kiingereza-English kuanzia darasa la kwanza. Inasikitisha sana viongozi wetu wana aminisha kwamba hakuna umuhimu wa kujua kufundisha English kwa elimu ya msingi wakati watoto wao karibu wote wanasoma shule ambazo zinafundisha kiingereza kuanzia msingi!. Hili swala halitakiwi kuwa na watu wenye uwezo na hali ya juu pekee.
Mimi sipendi sana kuongea vitu kwa hisia nitatoa mfano wa ukweli kwa familia yetu. Mtoto wa Kaka yangu amesoma Tanzania English media kuanzia darasa la kwanza amekuja huku akiwa na miaka 18 na kujiunga na community college kwa miaka miwili na baadae akaenda kumaliza degree ya Accounting Mississipi. Mwaka jana akiwa na miaka 22 kabla hajafika miaka 23 tayari kapata kazi, kampuni imempa visa maalumu ya miaka mitatu ya wafanyakazi HB1 visa, na analipwa dollar $65,000 kwa mwaka ambayo ni Tsh 152,490,003. Huyu mtoto ameweza kushindana na wenzake kupata kazi kwasababu ana uwezo mkubwa wa kujieleza na kujua kiingereza vizuri. Nasema hivi si kwa kujigamba bali kuonyesha hili sio swala la watu fulani linawezakana kwa kila mtoto kupata elimu ya hivi.
Tanzania tunaenda kwenye kushindana kampuni nyingi za teknologia mfano zinaenda kuwekeza Kenya kwasabbu ya mfumo wa elimu yao wakati Tanzania tumepata uwekezaji usiozidi $200M wenzetu Kenya wamepata uwekezaji zaidi ya $2B kwenye teknologia kuanzia microsoft, google na kampuni nyingine kubwa. Tofauti ni English tu na ukiangalia wanafunzi wetu wanaosoma english media wakienda Kenya au kuja nchi kama USA wana uwezo sawa au hata zaidi ya wale wa Kenya.
Nashauri tusiweke mazingira ya uongo ya kuaminisha wananchi kwamba tukifundisha watoto wetu english kuanzia darasa la kwanza ni kutokuwa wazalendo wakati viongozi wetu wanasomesha watoto wao english media. Kama tunatatizo la walimu basi tulitatue ikiwa na pamoja na kubadilishana walimu na kenya na uganda kwa sisi tuwapeleke kwa muda walimu wa kiswahili kwao na wao watupe walimu wa english
Tukishinda hapa kupigana madongo ukweli ni kwamba watoto wa masikini tu ndiyo wanakosa nafasi. Kuweni makini sana na mashabiki
KUHUSU EAC
Kwa ufupi tu umoja ni nguvu. Ukiangalia vizuri kuna vitu ambavyo wana EAC tungeweza kufanya pamoja na kurahisisha maendeleo ya nchi zote
1. Madawa tungeweza kuagiza pamoja maana tunaumwa magojwa yale yale hii ingesaidia kupunguza bei ya uagizaji kwasababu tuna nunua kwa jumla. Lakini kwenye chanjo kama za Corona tungeweza kuagiza kwa pamoja na kugawana zikifika hapa!.
2. Mfumo wa elimu tungeweza kuweka mfumo mmoja hii ingesaidia wawekezaji wakija kwenye nchi mmoja kuwa na vijana wenye elimu zenye uwiano sawa. Vilevile ingesaidia kwa elimu za madaktari na walimu.
3. Usalama pamoja na kuwa na majeshi yetu tungeweza kuwa na jeshi ya EAC kwa ujumla kupambana na ugaidi na ku share hata satellite za usalama. Hii ingepunguza matumizi mabaya ya kijeshi maana tumekuwa dump la kuuziwa vifaa vya kizamani.
4. Shirika la ndege moja ni vichekesho kuwa na shirika la ndege kila nchi ! Tungefungua kampuni moja halafu wawe wanakodisha ndege kutoka nchi shiriki na kila nchi itakuwa na share kutokana na mchango wake hii ingepunguza gharama na kuongeza ushindani bila hivi mashirika ya nje yataendelea kutawala anga zetu.
5. Masoko ya mzao ya pamoja yaani kuwe na shirika la kuongoza masoko ya biashara za mazao na bei ziwe wazi na kutangazwa kote kuwe na masoko ya jumla kila mpakani ya kisasa. Kama ilivyo dhahabu bei za mazao ziwe zinatangazwa kwa uwazi .
6. Tuwe na vyuo vya technologia na ufundi pamoja kufundisha teknologia mpya kama programming. Fungueni kampuni na kuingia mkataba na kampuni kama Microsoft, google, Apple na Oracle ili vijana wetu waweze kufanya kazi kutokea nchi hizi washiriki.
India mfano wana vijana kwa milioni wanafanya kazi za nchi nyingine kuanzia engineering design, customer service, payroll and accounting, bank support. kwanini sisi tushidwe wakati tuna vijana wengi.
Kwa ufupi tungeangalia kwa upana tungeweza kuendelea zaidi kuliko sasa
BANK KUU HII NILITOA 2012
Naona badala ya kuongea siasa kila wakati tunaweza kuelimishana kwenye mammbo muhimu hapa.Hii topic nilishawahi kuituma.
Tanzania inakabiliwa na matatizo mengi ya uchumi. Moja la tatizo kubwa linalokwamisha sana maendeleo ni hakuna utaratibu mzuri wa bank kusaidia uchumi kama ulivyo kwenye nchi zenye uchumi mkubwa. Mikopo ni migumu kupata na riba ipo juu sana kiasi kwamba ni vigumu kwa wafanyabiashara wa kawaida kupata mikopo. Bank za Tanzania hazisaidii uchumi kama inavyotegemewa tena ukizingatia pesa karibu zote zimewekewa riba na bank kuu kwa kupitia serikali. Serikali na Bank kuu zinatakiwa kufanya yafuatayo
1. Vitambulisho: Serikali inatakiwa kuwa na vitambulisho vya uhakika ili watoa mikopo wa wapokea mikopo wajuane. Hii vilevile itasaidia kujua historia za watu za mikopo.
2. Historia ya mikopo au (Credit Rating System): Serikali bank kuu na wizara husika zinatakiwa ziweke utaratibu wa kuwa na hifathi (database) ambayo inaonyesha historia za watu kuchukua na kulipa mikopo.
3.Riba za T-Bills/T-Bond za serikali ziwe chini: Serikali inachukua pesa kwa wananchi na mashirika kwa njia hizi mbili. Serikali ikichukua hii mikopo inatoa vitu viwili muhimu (a) muda wa kuwalipa mikopo (b) riba ya mikopo. Riba ya hii mikopo ya serikali ambayo mara nyingi ni lazima ilipwe ni kubwa sana 7%-8% ukilinganisha na nchi nyingine ambazo zina 2%-5%.
Hii ni muhimu sana kwani bank ikitoa mikopo inatoa kutokana na riba hizi. Riba za bank ni lazima ziwe juu kuliko za serikali hivyo kama riba zao ni 5% na serikali ni 7% wanakupa riba ya 12%. Hii ni kwasababu watu ambao wanatoa pesa za mikopo ya bank hawawezi kuwekeza kwenye mikopo ya bank wakati mikopo ya serikali inauhakika wa kulipwa (Risk Fee rate). Kwa bank kupata wawekezaji ni lazima waweke kiwango cha juu zaidi.
TEKNOLOGIA
Ubunifu ni muhimu sana kwa nchi. Ushauri wangu huu ni serious sana kuliko watu nwengi wanavyofikiria.
Mimi ni diaspora hapa USA naona jinsi ambavyo kazi nyingi za technolojia zinafanywa kutokea India. Sasa najiuliza kuna ugumu gani ya vijana wetu wanaomaliza shule na kufanya kazi hizi kutokea Tanzania? inawezekana kabisa lakini kunatakiwa kuwa na makubaliano na hizi kampuni.
Nashauri serikali ifanye mwaliko wa hawa maguru na wakubwa wa hizi kampuni ili wafungue data center Tanzania waweze kuajiri wataalamu tofauti hasa kwenye teknolojia. Tusione aibu kuandikia barua na kualika hata kama wakisema hawana muda tunaweza kubahatisha mmoja.
Niongezee tu kwenye soko la hisa za Marekani 50% ni kampuni za teknolojia hizo hapo ni thamani za kampuni mfano Apple hapo ni $T2.3 na Oracle ni $240B
www.jamiiforums.com
zitto junior Pascal Mayalla

- Mikopo yote ya serikali bila kujali awamu iangaliwe kwa kujua muda wa kulipa mikopo na riba za mikopo
- Group 1: Mikopo yote yenye riba ndogo na miaka mingi ya kulipa. Hii ndiyo mikopo mizuri. Mfano kama una mkopo wa 5% kwa miaka 20 huu ni mkopo mzuri.
- Group 2. Mikopo ya pili ni mikopo yenye riba ndogo lakini muda mfupi. Hii nayo ni mizuri lakini muda ndiyo tatizo
- Group 3. Mikopo yanye riba ya juu ambayo ni zaidi ya 10% lakini muda mfupi. Hapa tatizo kubwa ni riba na huu ni mkopo mbaya
- Group 4. Mikopo yenye riba ya juu zaidi ya 10% na ya muda mrefu. Hii ndiyo mikopo mibaya kuliko yote.
- Mikopo Group 3 fanyeni mpango kama mnaweza kujadili malipo kwa njia ya refinance. Hii ni kama kutafuta wawekezaji/bank ambayo inaweza kulipa hili deni na kukupa muda zaidi wa kulipa na riba nafuu. Inavyotokea ni kwamba hii bank au watoa mikopo wanalipa mkopo wote na lile deni linakuwa mkopo mpya nafuu na wa muda mrefu. Kama ni mkopo wa serikali chukueni hii mikopo na mpeni Raisi aweze kuongea na hiyo serikali husika. Wizara inatakiwa kumpa Raisi kitu ambacho kimekamilika ili akaongee nao. Mfano kama ni mkopo wa serikali ya Japan raisi anaweza kuongea na waziri mkuu wa Japan lakini ni lazima kwanza wizara ifanye kazi yake na kuwa na data zote za mikopo kwbla ya kupeleka kwa Raisi. Tatizo hakuna ubunifu na watendaji wa wizara wanabaki tu na utekelezaji badala ya kuwa wabunifu
- Mikopo Group 4. Hii mikopo yote inabili kila mmoja uangaliwe upya na kutafuta njia zote za ku refinance. Hii ni kutafuta mkopo wa nafuu wa kulipa huu mkopo mbaya halafu mkopo mpya unakuwa wa muda mrefu zaidi na riba ya chini. Kama ni mikopo ya nchi muhusisheni Raisi!
- Nimesikitiswa sana na wale wasomi wanao jaribu kuaminisha Watanzania kwamba kuna mikopo ya bank za biashara mizuri kwa serikali. Mikopo yenyewe mingi ni ya miaka 5 na riba zinakuwa 8%~10%. Hii mikopo sio mizuri kwa serikali hasa ukizingatia uwezo wetu. Serikali kwa ushauri wangu
1. Wasikope chini ya miaka 10
2. Riba ya mkopo isizidi ukuaji wa uchumi mfano Tanzania ukuaji wa uchumi ni 5%~ 7% hivyo riba iwe hapo katikati . Kama mkopo ni kwa dollar isizidi 5% kwasababu mfumuko wa bei wetu unakuaga 2% zaidi ya USA
Mwigulu acha mikopo ya riba ya juu na muda mfupi hii inaongeza payment amount za mwezi na mwaka na kusababisha pesa nyingi kwenda kwenye mikopo.
Mimi kama diaspora nitaanza na mawazo mawili makubwa halafu naomba wadau muongeze
1. Nashauri Mabalozi ambao wanateuliwa wapimwe uwezo sio tu kuchagua watu ambao ni madiplomasia wa wizarani na ofisi zetu za balozi lakini kuchagua watu ambao wanauzoefu wa biashara, uwekezaji na ushawishi. Tunahitaji wafanyabiashara, diaspora, na watu ambao wamewahi kuongoza biashara kubwa kama banks kuwa mabalozi. Tumechoka watu ambao wanaenda kujifunza kazi na wengi wa mabalozi ni slow sana na hawajui majukumu yao vizuri.
2. Balozi zote ziunde group za ushauri kwa ubalozi-Tanzania. Group hizi ziwe ni wataaalamu tofauti Watanzania au wadau wanaopenda maendeleo ya Tanzania. Mfano kwa hapa USA na Canada ambako mimi nina makazi kuwe na washauri wa mambo ya technologia, elimu, afya, ujenzi, ushirikiano na uwekezaji. Uzuri wa hizi group wadau ambao ni wataalamu watatoa ushauri bure lakini kwa kuhakikisha ushauri unatolewa moja kwa moja kwa balozi na wenyewe kupeleka Tanzania.
Lakini hizo group vilevile kama kuna mtu anataka kuwekeza wanakuwa na uwezo kufanya mikutano moja kwa moja na wahusika kwa kutumia zoom meetings za kimkakati.
Hii inasaidia kwennye kutoa misaada Tanzania, kuongeza utaalamu na ushauri na kuongeza umoja. Tatizo la sasa balozi zetu zimekuwa zinasubiri badala ya wenyewe kuwa wadau wa kwanza wa kuanzisha group. Mfano Balozi badala ya kukimbilia kuandikisha majina ya diaspora wangetakiwa kuanzisha group hizi totafuti kwa kupitia wenyeviti wa jumuia za watanzania ambao wapo kija mji mkubwa.
Ingeweza ikawa website, wahatapp groups ... lakini lengo ni kutoa ushauri, kuongeza uwekezaji na misaada. Hizi group zitakuwa kama vyama ambapo uongozi ndani ya haya makundi unaweza ukawa na ukomo wake ili kutoa fursa za mawazo mapya.
TANESCO
Kuhusu Bwawa la Nyerere: Ukweli ni kwamba Umeme wa Bwawa la Nyerere utatutosheleza lakini sio mwingi kiasi cha kuuza nje. Kuna umeme sasa umefika vijijini, joto la dunia linaongezeka, treni ya umeme, matumizi ya Air condition kuongezeka, viwanda vipya. Mfano viwanda vya chuma na cement vinatumia umeme sana.
TANESCO
- Utengenezaji wa umeme (Generation) ambapo umeme unaotokana na joto (Themal) kwa kutumia gas 63.36% na umeme wa maji 36.64%
- Usambazaji wa umeme
- Customer Service lakini wenyewe wanasema Distribution
- Ukweli ni kwamba jitahada za kusambaza umeme nchi nzima hazijaendana na ongezeko la utengenezaji wa umeme.
- Kwenye kusambaza umeme vijijini umeme mwingi unapotea. Kwasasa 16% ya umeme wa Tanesco unapotea lakini hii asilimia inaongezeka zaidi umeme unavyozidi kusambazwa
- Tanesco iwe na wakurugenzi watatu wa kila idara na mmoja wa kampuni yote. Hivyo kila kitengo kiendeshwe kama kampuni. Hii inasadia kujua ni sehemu ganio hasa ina yumba na inahitaji msaada mfano kuna fungu maalamu kwenye malipo ya bill za umeme abayo ni usambazaji tu. Hivyo usambazaji wa umeme ukiwa kama kampuni tutajua kwa undani kama pesa zinatosha au bunge litafute njia nyingine ya kuongeza pesa. Lakini kama kweli tupo 80% ya vijiji au zaidi basi gharama zinatakiwa zianze kupungua baada ya muda maana kusambaza ni mara moja na baada ya hapo ni kutengeneza maharibiko madogomadogo kwa pesa ambayo itaongezeka na wateja wapya. Hiyo ingekuwa kampuni inajitegemea ingeweza hata kukupa maana unamwekea mtu umeme halafu gharama zinarudi polepole lakini mwanzo kuna pesa zinahitajika nyingi zaidi.
- Ukweli ni kwamba umeme wetu ni wa gas 63.36%. Wasiwasi wangu ni kwamba serikali inawezekana kabisa inanunua umeme huu kwa bei ya kimataifa ingawa gas hii inatoka Tanzania. Hii ni kwasababu wauza gas ni songas, TPDC na makapuni mengine ya nje lakini kuna gharama za pipeline ziko hapo. Bwawa na maji tunalojenga litasaidia sana kwenye hili. Lakini vilevile serikali inatakiwa itumie njia ya hedge ambayo unanunua gas nyingi wakati bei ipo chini halafu unaomba hiyo gas iletwe baadae
- Manunuzi yote ya umeme yahamie kwenye mitandao na kutumia simu. Hii itapunguza gharama za madalali na utengenezaji wa kadi za namba kwa Tanesco bila kupunguza kipat
TATIZO LA DOLA $
Mawazo yangu ya jinsi ya kutatua tatizo la dollar Tanzania
1. Serikali iongee na kampuni za utalii na kuwaomba walete pesa hapa utaratibu wa sasa watalii wanalipia hotel na karibu kila kitu kabla hawajaja kutalii na pesa karibu zote zinabaki kwenye bank za nje
2. EAC tuharakishe kuwa na pesa moja hii itaongeza nguvu ya hii pesa mpya. Lakini itapunguza sana utumiaji wa dollar
3. Bank ya Tanzania itumie pesa kununua dhahabu ambayo ni nyingi Tanzania. Hii itakuwa rahisi kama tunahitaji dollar zaidi kununua.
4. Tanzania tunatakiwa kuongeza (1) Utengenezaji wa vitu nchini (2) Kuongeza uuzaji wa bidhaa nje ya nchi
5. Tanzania raisisheni utaratibu wa Diaspora kuja na dollar. Kwasasa utaratibu wa passport copy sijui, vitambulisho ili mtu aweze kubadilisha dollar zake unasababisha watu watumie sendwave, world permit na Apps za kutuma pesa na diaspora hawaji na pesa tena kwasababu ya usumbufu wa kubadilisha pesa.
BARUA YANGU KWA VIJANA
Wadogo zangu vijana wa Kitanzania habari zetu. Mimi ni kijana mkubwa 40+ na napenda niwaandikie barua kutoka moyoni kwangu kwa ninayo yaona miaka hii na kwa nchi yetu ya Tanzania. Mambo nitakayo yasema unaweza usayaelewe kwa wakati huu kutokana na umri wako au uzoefu wako kwenye maisha lakini haita kuwa vizuri kila siku kuishia kuwapiga madongo kila siku badala yake huu ni wakati wa kusema kama Kaka.
1. Tanzania ya sasa mwaka huu 2024 ni bora kiuchumi kuliko wakati sisi tuna maliza Form 6 kwa mimi binafsi ilikuwa mwaka 1996 pale Tambaza Secondary. Hivyo asije kutokea mtu akawadanganya kwamba uchumi wa sasa ni mbaya kuliko zamani hii sio kweli.
2. Tanzania bado ni nchi masikini sana pamoja na rasilimali tulizonazo. Mimi nimetembea nchi nyingi sana na nimekuwa naishi nchi tofauti toka mwezi wa nane 1997 hivyo nasema haya kwa kujiamini na uzoefu na sio kwa kubahatisha.
3. Mabadiliko ya tabia nchi ni ya kweli hivyo mazingira ya mvua, mafuriko , kiangazi ni zaidi sasa kuliko miaka ile ya kwetu tukiwa 20's. Hivyo kwenye mipangalio yako tilia hili maanani.
4. Teknologia ni bora sana kwa vyakati zenu kuliko wakati wetu. Ingawa Teknologia kwa vijana wengi hamuitumia kwa faida ya kujiendeleza.
5. Ushindani wa sasa wa kazi, na maarifa kwenu ni mkubwa zaidi maana mnashindana kitaifa na sio Tanzania peke yake lakini vilevile fursa mnazo zaidi ya nyakati zetu.
6. Siasa za Tanzania hazibadilika sana zaidi ya wapinzani kupata nguvu zaidi . Lakini ukweli ni kwamba hatujawahi kubahatika kupata watu kwenye chama chetu tawala ambao wameweka mbele nchi zaidi ya marafiki zao, famillia zao na kundi la wachache viongozi wa vigogo wa kisiasa. Majina kama Kikwete, Mwinyi, Karume, Kinana, Kingunge. Nauye, Makamba., Malecela, Lowassa tumeyasikia kwa miaka zaidi ya 30. Hivyo viongozi wenu wa kisiasa na wabunge hawajawahi kuwajali na hawajali hata sasa kama wanavyo jiaminisha.
Je nawashauri mfanye nini
1. Ushauri wangu wa kwanza . Kila kijana jiulize kwa undani wako unapenda kuwa nani kwenye maisha yako. Usifanye vitu kwa kuiga iga fanya vitu kutoka moyoni.
2. Tumieni teknologia kujiendeleza kiuchumi mfano kutafuta kazi, kuomba mawazo, kutafuta shule, kutengeneza App, kusoma, kutafuta kazi za nje, kumuamini mungu zaidi, kujiunga na makundi ya nje ya nchi ya kimaendeleo n.k. Weka muda maalumu wa kutumia mitandao kwa mambo mengine lakini muda mwingi uwe kwenye maendeleo
3. Ukishajua kitu unachopenda tafuta Mentor. Memntor ni mtu ambaye ni mfano wa wewe unataka kuwa huyu ni mshauri lakini mwenye uzoefu wa kweli. Mfano wewe unataka kuwa mwana siasa basi hata hapa mitandaoni watafute wakina Zitto, Mwigulu na wengine sio lazima wawe maarufu tafuta mmoja mwombe awe mentor wako. Lakini kuna Mentor wa biashara, kilimo, elimu, chochote utakacho. Memntor sio lazima awe Mtanzania. Mimi nipo Texas na kwa asilimia kubwa nimefanikiwa kwa kushauriwa na wazungu ambao kwa wengine wanaweza kuitwa wabaguzi lakini unahitaji mmoja mzuri tu kukushauri na kukutoa.
4. Msikimbilie kuoa. Maisha ya siku hizi na maendeleo ya afya mnakuwa na maisha marefu wengi wenu tumieni muda kutafuta marafiki na watu mtakao endana nao badala ya kukimbia kuona kwa kufikiri umechelewa. Kosa la kukimbia kuoa na kuzaa linaweza kukuharibia ndoto zako.
5. Pesa haitatosha kukupa furaha. furaha utapata kutoka kwa watu na kusaidia watu na sio kuwa na pesa nyingi. Hata pale utakapo pata pesa furaha watu wanapata pale wanapoona watoto wao na ndugu zao wanafurahi na sio pesa yenyewe.
6. Hakuna maisha bila kufanya kazi. Unaweza kupata kazi inallipa sana lakini majukumu nayo yanakuwa makubwa. Muda unakuwa mdogo, kodi nyingi, wafanyakazi wengi kwasabbu kipato kuongezeka mara nyingi gharama za maisha nazo zinaongezeka. Hivyo matatizo hayaishi bali yanahama tu. Hakuna kazi rahisi popote Duniani.
7. Afya zenu nmuhimu sana. Pombe kunywa kwa kiasi, hakikisha unaangalia kila kitu kwenye mwili wako. Mwili ni kama gari ambalo ninaishi mpaka miaka 100 na ni mmoja tu. Gari utanunua lingine lakini mwili wako ni huohuo. Macho ni hayo hayo, miguu ndiyo hiyo hiyo kuwa mwangalifu.
8. Kuweni makini sana na vyakula vya kisasa. Piza, buggers na vyakula vya makopo.
9. Usiogope kutafuta kazi nje ya nchi kwa faida ya famila yako
10. Msisubiri kuletewa maendeleo na serikali tumesubiri kwa miaka 60 sasa!
11. Upinzani pekee sio suluhisho nyie ndiyo mnatakiwa kupigania maendeleo yenu sio vyama vya siasa pekee. Hakuna wa kulaumu kama nyie wenyewe mnaridhika kirahisi na umasikini. Mna nguvu kuliko mnavyojifikiria
12. Kuna wakati kwenye maisha yako pesa na mambo mengine yote hayata weza kukusaidia na wewe kuwa sawa ni lazima uwe na Imani kwa Mungu. Ukifiwa, kuumwa ndiyo utajua hili. Ni lazima uweke imani mbele
13. Achani kuwa fake
14. Uwezo wako uko moyoni kwako. Unajua unaweza sasa kwanini unalalamika sana. Acheni tabila za kulalamika. Mfano kwenye siasa Lissu kapigwa risasi bado ana andamana na sio kulalama pekee.
15. Jiwekee mipango ya maendelo kila mwaka
16. Jiamini na msiogope.
Ka ijumaa hii nitaishia hapo nawatakia siku njema
WAMACHINGA
Watanzania wengi hawajui kwamba Wamachinga hawasaidii nchi yetu badala yake wanatumika kwa siasa pekee. Watanzania wanashangilia wamachinga ambao hawalipi kodi halafu wanalalamika wenyewe kuongezewa kodi!
1. Hawalipi kodi yeyote ya maana na vibali vya machinga ni kama kukejeli Watanzania.
2. Wachafuzi wa mazingira. Hivi hizi gharama za usafi analipa nani hasa kwa watu wasio lipa kodi.
3. Wanauza vitu vya kijinga ambavyo havina msaada wowote wa maana kwa viwanda vyetu wala sera muhimu kama kilimo, elimu au afya.
4. Wanasaidia viwanda vya china sio Tanzania hebu tukaangalie kama vitu vya machinga ni vya Tanzania! Utakuta ni majalala ya kichina hivyo tunasaidia wachina na sio Tanzania.
5. Wanaua wafanyabiashara wadogo ambao wanalipa kodi maana wameweka magenge ambayo hayana mpangilio mbele ya biashara nyingine
KUHUSU KISWAHILI
Kiswahili kinakuwa sana na Tanzania tunapata heshima sana kwa lugha yetu hii. Hii naina maana tusifundishe watoto wetu kiingereza-English kuanzia darasa la kwanza. Inasikitisha sana viongozi wetu wana aminisha kwamba hakuna umuhimu wa kujua kufundisha English kwa elimu ya msingi wakati watoto wao karibu wote wanasoma shule ambazo zinafundisha kiingereza kuanzia msingi!. Hili swala halitakiwi kuwa na watu wenye uwezo na hali ya juu pekee.
Mimi sipendi sana kuongea vitu kwa hisia nitatoa mfano wa ukweli kwa familia yetu. Mtoto wa Kaka yangu amesoma Tanzania English media kuanzia darasa la kwanza amekuja huku akiwa na miaka 18 na kujiunga na community college kwa miaka miwili na baadae akaenda kumaliza degree ya Accounting Mississipi. Mwaka jana akiwa na miaka 22 kabla hajafika miaka 23 tayari kapata kazi, kampuni imempa visa maalumu ya miaka mitatu ya wafanyakazi HB1 visa, na analipwa dollar $65,000 kwa mwaka ambayo ni Tsh 152,490,003. Huyu mtoto ameweza kushindana na wenzake kupata kazi kwasababu ana uwezo mkubwa wa kujieleza na kujua kiingereza vizuri. Nasema hivi si kwa kujigamba bali kuonyesha hili sio swala la watu fulani linawezakana kwa kila mtoto kupata elimu ya hivi.
Tanzania tunaenda kwenye kushindana kampuni nyingi za teknologia mfano zinaenda kuwekeza Kenya kwasabbu ya mfumo wa elimu yao wakati Tanzania tumepata uwekezaji usiozidi $200M wenzetu Kenya wamepata uwekezaji zaidi ya $2B kwenye teknologia kuanzia microsoft, google na kampuni nyingine kubwa. Tofauti ni English tu na ukiangalia wanafunzi wetu wanaosoma english media wakienda Kenya au kuja nchi kama USA wana uwezo sawa au hata zaidi ya wale wa Kenya.
Nashauri tusiweke mazingira ya uongo ya kuaminisha wananchi kwamba tukifundisha watoto wetu english kuanzia darasa la kwanza ni kutokuwa wazalendo wakati viongozi wetu wanasomesha watoto wao english media. Kama tunatatizo la walimu basi tulitatue ikiwa na pamoja na kubadilishana walimu na kenya na uganda kwa sisi tuwapeleke kwa muda walimu wa kiswahili kwao na wao watupe walimu wa english
Tukishinda hapa kupigana madongo ukweli ni kwamba watoto wa masikini tu ndiyo wanakosa nafasi. Kuweni makini sana na mashabiki
KUHUSU EAC
Kwa ufupi tu umoja ni nguvu. Ukiangalia vizuri kuna vitu ambavyo wana EAC tungeweza kufanya pamoja na kurahisisha maendeleo ya nchi zote
1. Madawa tungeweza kuagiza pamoja maana tunaumwa magojwa yale yale hii ingesaidia kupunguza bei ya uagizaji kwasababu tuna nunua kwa jumla. Lakini kwenye chanjo kama za Corona tungeweza kuagiza kwa pamoja na kugawana zikifika hapa!.
2. Mfumo wa elimu tungeweza kuweka mfumo mmoja hii ingesaidia wawekezaji wakija kwenye nchi mmoja kuwa na vijana wenye elimu zenye uwiano sawa. Vilevile ingesaidia kwa elimu za madaktari na walimu.
3. Usalama pamoja na kuwa na majeshi yetu tungeweza kuwa na jeshi ya EAC kwa ujumla kupambana na ugaidi na ku share hata satellite za usalama. Hii ingepunguza matumizi mabaya ya kijeshi maana tumekuwa dump la kuuziwa vifaa vya kizamani.
4. Shirika la ndege moja ni vichekesho kuwa na shirika la ndege kila nchi ! Tungefungua kampuni moja halafu wawe wanakodisha ndege kutoka nchi shiriki na kila nchi itakuwa na share kutokana na mchango wake hii ingepunguza gharama na kuongeza ushindani bila hivi mashirika ya nje yataendelea kutawala anga zetu.
5. Masoko ya mzao ya pamoja yaani kuwe na shirika la kuongoza masoko ya biashara za mazao na bei ziwe wazi na kutangazwa kote kuwe na masoko ya jumla kila mpakani ya kisasa. Kama ilivyo dhahabu bei za mazao ziwe zinatangazwa kwa uwazi .
6. Tuwe na vyuo vya technologia na ufundi pamoja kufundisha teknologia mpya kama programming. Fungueni kampuni na kuingia mkataba na kampuni kama Microsoft, google, Apple na Oracle ili vijana wetu waweze kufanya kazi kutokea nchi hizi washiriki.
India mfano wana vijana kwa milioni wanafanya kazi za nchi nyingine kuanzia engineering design, customer service, payroll and accounting, bank support. kwanini sisi tushidwe wakati tuna vijana wengi.
Kwa ufupi tungeangalia kwa upana tungeweza kuendelea zaidi kuliko sasa
BANK KUU HII NILITOA 2012
Naona badala ya kuongea siasa kila wakati tunaweza kuelimishana kwenye mammbo muhimu hapa.Hii topic nilishawahi kuituma.
Tanzania inakabiliwa na matatizo mengi ya uchumi. Moja la tatizo kubwa linalokwamisha sana maendeleo ni hakuna utaratibu mzuri wa bank kusaidia uchumi kama ulivyo kwenye nchi zenye uchumi mkubwa. Mikopo ni migumu kupata na riba ipo juu sana kiasi kwamba ni vigumu kwa wafanyabiashara wa kawaida kupata mikopo. Bank za Tanzania hazisaidii uchumi kama inavyotegemewa tena ukizingatia pesa karibu zote zimewekewa riba na bank kuu kwa kupitia serikali. Serikali na Bank kuu zinatakiwa kufanya yafuatayo
1. Vitambulisho: Serikali inatakiwa kuwa na vitambulisho vya uhakika ili watoa mikopo wa wapokea mikopo wajuane. Hii vilevile itasaidia kujua historia za watu za mikopo.
2. Historia ya mikopo au (Credit Rating System): Serikali bank kuu na wizara husika zinatakiwa ziweke utaratibu wa kuwa na hifathi (database) ambayo inaonyesha historia za watu kuchukua na kulipa mikopo.
3.Riba za T-Bills/T-Bond za serikali ziwe chini: Serikali inachukua pesa kwa wananchi na mashirika kwa njia hizi mbili. Serikali ikichukua hii mikopo inatoa vitu viwili muhimu (a) muda wa kuwalipa mikopo (b) riba ya mikopo. Riba ya hii mikopo ya serikali ambayo mara nyingi ni lazima ilipwe ni kubwa sana 7%-8% ukilinganisha na nchi nyingine ambazo zina 2%-5%.
Hii ni muhimu sana kwani bank ikitoa mikopo inatoa kutokana na riba hizi. Riba za bank ni lazima ziwe juu kuliko za serikali hivyo kama riba zao ni 5% na serikali ni 7% wanakupa riba ya 12%. Hii ni kwasababu watu ambao wanatoa pesa za mikopo ya bank hawawezi kuwekeza kwenye mikopo ya bank wakati mikopo ya serikali inauhakika wa kulipwa (Risk Fee rate). Kwa bank kupata wawekezaji ni lazima waweke kiwango cha juu zaidi.
TEKNOLOGIA
Ubunifu ni muhimu sana kwa nchi. Ushauri wangu huu ni serious sana kuliko watu nwengi wanavyofikiria.
Mimi ni diaspora hapa USA naona jinsi ambavyo kazi nyingi za technolojia zinafanywa kutokea India. Sasa najiuliza kuna ugumu gani ya vijana wetu wanaomaliza shule na kufanya kazi hizi kutokea Tanzania? inawezekana kabisa lakini kunatakiwa kuwa na makubaliano na hizi kampuni.
Nashauri serikali ifanye mwaliko wa hawa maguru na wakubwa wa hizi kampuni ili wafungue data center Tanzania waweze kuajiri wataalamu tofauti hasa kwenye teknolojia. Tusione aibu kuandikia barua na kualika hata kama wakisema hawana muda tunaweza kubahatisha mmoja.
Niongezee tu kwenye soko la hisa za Marekani 50% ni kampuni za teknolojia hizo hapo ni thamani za kampuni mfano Apple hapo ni $T2.3 na Oracle ni $240B
Ushauri: Wizara ya Uwekezaji, Teknolojia na Ikulu andikeni barua kuwaalika hawa mapema
Ubunifu ni muhimu sana kwa nchi. Ushauri wangu huu ni serious sana kuliko watu nwengi wanavyofikiria. Mimi ni diaspora hapa USA naona jinsi ambavyo kazi nyingi za technolojia zinafanywa kutokea India. Sasa najiuliza kuna ugumu gani ya vijana wetu wanaomaliza shule na kufanya kazi hizi kutokea...
zitto junior Pascal Mayalla