Ningependa kujua haya

Ningependa kujua haya

hidencode

Member
Joined
Nov 8, 2018
Posts
13
Reaction score
9
Habari wadau
Ningependa kuuliza kuwa kuna athari gani kula mchanganyiko wa matunda mengi katika mlo mmoja?

Hii inatokana na katika migahawa mingi hapa Dar es salaam, na hata ukipita maeneo ya postal utakuta watu wanakatakata matunda aina nyingi na kuyaweka kwenye kifungashio kwaajili ya kuuzia watu

Je huo mchanganyiko hautengenezi kitu ambacho ni hatari katika mwili wa binadamu!?

Mwisho kuna makala nyingi nimeona wakizungumzia faida za unywaji wa maziwa. Je faida hizi tunazipata zaidi kwenye maziwa freshi au maziwa mtindi? Je kati ya maziwa freshi na mtindi yapi bora kwenye afya ya binadamu?

Natanguliza shukrani zangu kwa watakaonijibu
 
machanganyiko wa matunda hauna madhara mkuu, sema tu kama utataka kula na chakula ndio utofautishe muda angalau nusu saa kabla.

Kwa maziwa, fresh ni mazuri zaidi kiujumla, ila maziwa mtindi huwa yanakuwa yameanza kumeng'enywa hivyo ukinywa mwili hautumii nguvu nyingi na ni mazuri kwa wagonjwa hasa magonjwa yanayohusiana na mfumo wa mmeng'enyo wa chakula.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo mkuu faida ninazozipata kwenye maziwa freshi ndio hizo hizo nazipata kwenye maziwa mtindi ila kwa kiasi kidogo au ulikua na maana tofauti na hiyo?
 
Yap, almost yote sawa.
 
Hauwezi kuchanganya matunda yenye contents zisizoendana pamoja,tikiti,matango ni jamii moja ..hauwezi changanya matunda tofauti tofauti ukayala kwa pamoja tu bila kuzingatia chemistry zao ndani ya tumbo.
 
Ni adhari gani unaweza kuzipata endapo ukichanganya matunda yasiyo na content zisizoendana? Hebu tupe mfano wa matunda yasiyo na content zinazoendana
 
Kuna mdau alishawahi kuweka humu madhara ya kuchanganya matunda na kula kwa pamoja,nikiuona huo uzi nitauweka!!
 
Back
Top Bottom