Ningependa Sunday Manara siku moja atueleze ilikuwaje mwanawe Haji Manara akawa Simba damu?

barafuyamoto

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2014
Posts
32,378
Reaction score
29,739
Habari zenu!
Kwanza NAPENDA NIJIPONGEZE na NIWAPONGEZE mashabiki, wapenzi na wadau wote wa Simba kwa ushindi wa jana dhidi ya watani zetu wa jadi, Yanga. Leo mtaani kutamu kweli, watani kama wamelowekwa maji, wapoleeee na heshima ipo.

Lengo la huu uzi ni kuhusu huyu msemaji wa Simba, Haji Manara. Jamaa ni kama kaapishwa na kanywa maji ya bendera ya Simba. Humuelezi kitu kuhusu Simba. Ni shabiki wa kutupwa wa Simba. Sasa najiuliza, hivi baba zake Sunday Manara (baba yake mzazi), Kitwana Manara na Kassim Manara ambao hawa ni Yanga damu na walichezea Yanga enzi zao, walishindwa kumshawishi mwanao kuwa upande wao??

Ningependa sana siku Sunday Manara na hao Manara wengine wahojiwe na watueleze ilikuaje kuaje mpaka Haji akahasi maana nina uhakika walijaribu kila wawezalo ila ilishindikana.

THIS IS SIMBA.
Hii jana hapo taifa. Alihamasisha sana kabla ya mechi wana simba waende na hawakumuangusha.

Interview ya Manara.
 
amependeza sana na huo Uzi wa msambazi

1.Babu mzaa mama yake Haji Manara, kama sikosei mzee Mikidadi Kasanda aliwahi kuwa kiongozi mkubwa Simba equivalent na cheo cha Raisi kwa sasa, miaka ya 1973 au 74 wakati mapinduzi makubwa ya kimpira kwa vilabu na soka Tanzania yalionekana. Anaweza kuwa Babu ali mu influence, labda mama kama mpenzi wa Simba naye, ali mu influence etc

2. Kuna tetesi Sunday Manara aliwahi kutaka kwenda Simba, kaka yake kitwana akamtishia kuwa akienda Simba anamnyanganya mpira wote anampa Kassim. Sunday akaogopa. Inawezekana alikuwa na mapenzi na Simba kimoyomoyo, yamerithiwa kwa mtoto kama kuna kitu kama hicho.

3. Wakati mwingine ukiwa karibu na mpinzani unaweza kujua siri nyingine za mafanikio hata nguivu za adui kuliko watu wa nje. Yule anaweza kuwa alisikia baba zake wakiivulia Simba kofia kwenye baadhi ya mambo na yeye yakamvutia.
 
MIKIDADI KASANDA SIO BABU YAKE HAJI.......
BABU YAKE HAJI MZAA MAMA ANAITWA PIA MZEE MUHAJI ALIKUWA MWENYEKITI WA SIMBA NA UKOO WA MAMA YAKE HAJI WOTE NI SIMBA DAMU NAYE HAJI AMELELEWA HUKO. INGAWA HAJI ALIPELEKWA YANGA B KUCHEZA MPIRA WALIPOMKATAA NDIO HAJI AKAWA SHABIKI WA SIMBA
 


Nashukuru kwa masahihisho.
 
Kumbe chuki zote hizi ni sababu ya kukataliwa? Kama Ferguson na Liverpool ,kama Yule jamaa wa ni pombe gani aliyokupa huyoooo?Ni dawa gani aliyokunyweshaaa! Ukachanganyikiwa na kuisahau ,sura yanguuuu ,siku ya harusiiiiiiii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…