Nini cha kufanya endapo wazazi wako watamkataa mchumba unayetaka kumuoa au kuolewa naye?

Nini cha kufanya endapo wazazi wako watamkataa mchumba unayetaka kumuoa au kuolewa naye?

Mboka man

JF-Expert Member
Joined
Aug 22, 2020
Posts
478
Reaction score
1,647
Hakuna safari ndefu kama safari ya mahusiano huwa ina mabonde na malima lakini Moja kati ya changamoto kubwa katika mahusiano kuelekea ndoa ni wazazi kupinga au kumkataa mchumba unayetaka kumuoa au kuolewa kwa sababu mbalimbali wanazozijua wao.

Ni kitu gani cha kufanya katika hili?
 
In case of a conflict of interest, better listen to & go with your parents' wisdom. Theirs is almost always right and appropriate. ^By the time a son recognizes that his father was probably right, he usually has a son himself^
 
Kwa wale wanaoweza kujifanya yatima na maisha yakaendelea unaweza oa tu. Kwa wale ambao kila kitu anaendesha mzazi mpaka fikra itabidi itabidi unyooshe mikono
 
Maamuzi yatategemeana na sababu zao za kumkataa
 
Wazazi wako wanakutakia mema tangu ulipo letwa duniani.au una taka useme baba yako anataka usimuoe huyo binti ili akupindue amuoe yeye........? Au mama yako anamuonea gere huyo mchumba wako....?

Najua wewe saizi umegubikwa na huba huoni mbele .

Amini wazazi wako bado wanakupenda na wanataka kuona unamaisha mazuri kila siku. Siku utakayo kuja kusema baba na mama walikua sahihi ni siku ambayo utakua umechelewa Sana na umeharibikiwa Sanaa.
 
Hakuna mzazi anayemtakia mabaya mtoto wake,lkn cha kukumbuka ni kwamba na wao sio miungu,huwa wanakwenda wrong wakati mwengine.
 
Back
Top Bottom