1. Surrender hati manispaa: andika barua kwa mkurugenzi ya kurudisha hati lengo likiwa ni kutoa fursa ya kugawa kiwanja .
Mchakato utaanza hapo manispaa, kwenda kwa kamishna wa ardhi wa mkoa mpaka kwa msajili wa hati wa mkoa ambae atakupa document inaitwa deed of surrender, hapo mchakato wa kurudisha utakuwa umekamilika.
2. Andika barua kwa mkurugenzi wa manispaa kuomba kufuta upimaji( survey plan) ya hicho kiwanja, katika hiyo barua ambatanisha na ile deed of surrender.
Mchakato utaanza hapo manispaa ambapo wao watakachokifanya nikuonesha tu wamepokea ombi na hawana pingamizi na mwisho wataforward ombi lako kwa mpima wa mkoa ambae yeye ndie atakayefuta na kuwapa taarifa manispaa kwa barua kuwa amefuta, ( kumbuka kuweka sababu ya kwa nini unaomba kufuta)
3. Andika barua kwa mkurugenzi kuomba kufanya ammendment ya mchoro wa mipango miji wa eneo husika, hapa utaambanisha na mfano wa mchoro wa namna mnavyotaka kugawa.
Ammendment ikipita manispaa itaenda mpaka mkoani na kusajiliwa
4. Tafuta mpima atakayepima kuja kupima viwanja ambavyo ammendment imekubali, mpima atapima na kuwasilisha manispaa, ikipita manispaa itaenda mkoani na kusajiliwa
5. Viwanja vikishasajiliwa unarudi manispaa kuomba hati kwa kujaza form no. 19 pamoja na fomu za kumbukumbu za eneo na mipaka.
Mchakato ukitoka hapo utaenda kwa kamishna wa ardhi wa mkoa na mwisho kwa msajili wa hati,
Hapo kila mtu atakuwa amemiliki kiwanja chake