Nini cha kufanya kwanza unapoumwa na nyoka, ili kuokoa maisha?

Omukisa

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2024
Posts
642
Reaction score
1,305
Karibu 300% ya nyoka wote duniani wana sumu, na 50% ya visa vya nyoka wanaowauma binadamu huwa hawaachi sumu ndani ya mwili wakati wa wanapomuuma binadamu. Kwa hivyo ni karibu visa 15 kati ya 100 ya nyoka ambapo muathiriwa huhitaji matibabu

Nini cha kufanya ukiumwa na nyoka ili kuokoa maisha?

Kulingana na Shirika la Afya Duniani, kuumwa na nyoka wenye sumu kunaweza kusababisha kupooza, kupumua kwa shida, na wakati mwingine kukatwa kiungo ni hatua muhimu ikiwa sumu itaenea sana.

Mbali na hili, iwapo sumu ya nyoka itaenea zaidi mwilini na iwapo myu aliyeumwa na nyoka hatapoea matibabu anaweza pia kufariki , kwahiyo hatua zingine zinapaswa kuchukuliwa mara moja wakati unapoumwa na nyoka.

Nini cha kufanya wakati unaumwa na nyoka?
  • Unapoumwa na nyoka, kwanza hakikisha kuwa mtu aliyeumwa na nyoka na anayempatia huduma yuko mbali na nyoka. Usijaribu kumkamata nyoka.
  • Mtazame kwa mbali nyoka na ujaribu kukumbuka anakaaje, hii itasaidia kuwa rahisi kutibiwa wakati wa kupelekwa hospitali.
  • Ikiwa umevaa mapambo, saa, mkufu au vitu vingine kulipokuwa eneo la ulipoumwa na nyoka, ondoa.
  • Usikimbie baada ya kuumwa na nyoka, kaa kimya iwezekanavyo na ikiwezekana usimruhusu aliyeumwa kutembea.
  • Ita gari ikupeleke kwenda hospitali mara moja bila kupoteza muda, ili maisha ya mtu yaweze kuokolewa.
  • Kama inawezekana, kumbuka wakati tukio la kuumwa na nyoka lilipotokea na dalili gani zilifuata.
  • Unapofika hospitalini, kwanza mpe daktari maelezo ya jinsi nyoka alivyoonekana na kilichotokea.

Nini isichotakiwa kufanya wakati wa kuumwa na nyoka?
  • Usiweke bandage kwa nguvu sana wakati umeumwa na nyoka. Hata kama bandage imefungwa, inapaswa kulegezwa kidogo.
  • Ikiwa bandeji imefungwa kwa nguvu sana, sumu inaweza kuenea hadi sehemu ambayo nyoka amekuuma, na sehemu hiyo ya mwili inaweza kukatwa.
  • Baada ya kuumwa na nyoka, songa kidogo iwezekanavyo. Harakati nyingi zinaweza kusababisha sumu kuenea haraka katika mwili.
  • Usimpatie dawa yoyote ya mitishamba au dawa nyingine isiyojulikana mtu ambaye ameumwa na nyoka.
  • Usimpe kinywaji cha aina yoyote muathirika wa nyoka.
  • Mtu akianza kutokwa na damu, na kuongezeka kwa kiasi cha mkojo, akipata uvimbe kwenye eneo alipoumwa na nyoka, ukushindwa kupumua, maumivu ya kifua na dalili za kupooza, mpeleke hospitali mara moja.

Nini cha kuzingatia zaidi unapoumwa na nyoka?
  • Usijaribu kunyonya sumu kutoka kwa mtu aliyeumwa na nyoka
  • Usikate sehemu ya mwili iliyoumwa na nyoka ili kutoa sumu
  • Usiende kwa mganga wa kienyeji
  • Usimpe kamwe dawa za nyumbani mgonjwa aliyeumwa na nyoka
  • Usijifunge nyoka kujiuma yenyewe
  • Usisafishe wala kupaka barafu kwenye sehemu iliyoumwa na nyoka
  • Usijaribu kumshika au kumuua nyoka, kumuua nyoka hakuondoi sumu
Source: Nini cha kufanya kwanza unapoumwa na nyoka, ili kuokoa maisha? - BBC News Swahili
 
unamsaidiaje mtu alieumwa na nyoka akiwa katikati ya mazoezi?
 
Hapo kwa sentensi moja ulimaanisha.

Mgonjwa akimbizwe hospital kwa matibabu.
 
Nyoka wengi wanauma bila kuacha sumu, sumu hutumia kuwindia tu labda umshike mkia au ubane sehemu na asione upenyo wa kupita hapo lazima akushambulie kwa sumu, nishawahi kuumwa na Cobra na sikutumia dawa yoyote......

Dryer bite nyoka huifazi sumu yao cos ndo maisha yao maana bila iyo lazima huko mbugani atapata tabu sana......
 
Sijaiona point ya kufunga sehemu ulipoumwa ili damu isitembee, hii imekaaje?
 
unamsaidiaje mtu alieumwa na nyoka akiwa katikati ya mazoezi?
Ngoja wataalam waje wakupe mwongozo. Ila nadhani huduma ya kwanza iliyotajwa hapo juu inaweza kumsaidia kabla ya kumpeleka hospitali.
 
Nyoka wengi wanauma bila kuacha sumu, sumu hutumia kuwindia tu labda umshike mkia au ubane sehemu na asione upenyo wa kupita hapo lazima akushambulie kwa sumu, nishawahi kuumwa na Cobra na sikutumia dawa yoyote......

Dryer bite nyoka huifazi sumu yao cos ndo maisha yao maana bila iyo lazima huko mbugani atapata tabu sana......
Huko sahihi
 
Back
Top Bottom