Nini cha kuzingatiwa pindi mtoto mchanga anapozaliwa

Nini cha kuzingatiwa pindi mtoto mchanga anapozaliwa

kimara Kimara

Member
Joined
Jul 7, 2024
Posts
80
Reaction score
173
Habari za Muda Huu waungwana,

Kwa wale Mliowahi kupata Watoto, mkawakuza mpaka Wakakua na afya njema, Mlizingatia mambo yapi Pindi walipozaliwa?

Mimi niliwahi kupata mtoto, Bahati mbaya akafariki, Ninaomba kujuzwa wa wenye uzoefu ni mambo gani Muhimu kuzingatia.

Mambo baadhi ninayohutaji kuyajua.

1. Mtoto anapaswa kuanza kushikwa na watu akiwa na muda gani? (Watu wanaokuja kusalimia)

2. Ni muda Upi sahihi wa kutoa taarifa kua umepata mtoto kwa watu wako wa karibu. (Kabla ya arobaini ama baada ya arobaini)

3. Unajikinga Vipi na Husda na Vijicho vya watu wabaya Juu ya Mtoto wako mchanga?

4. Je, Baba mtoto akianza kuchepuka nje na wanawake wengine mtoto anaweza kuanza kuugua?

5. Mtoto akiwa anashikwa shikwa na watu wa nje waliotoka kufanya zinaa anaweza dhurika?

6. Kifanyike nini ili mtoto awe na afya nzuri na imara?

7. Kitovu cha mtoto mchanga kinatupwa wapi ama kinatunzwa?

Na mengine ambayo siyajui naomba kuyajua, natanguliza shukrani. [emoji120]
 
Me kwa mwanangu nimetilia sana mkazo iyo no 3 kwa kutokuruhusu mtot kutolewa nja kila wakati na kwangu hakuji wageni mara kwa mara
mda mwingi sana yupo ndani tu mpk sas anakaribia miaka 2 yupo vzr na mwenye afya tele
Nje ya nyumba au nje ya geti?
 
Kazi kwelikweli... binafsi huwa nasubiri wamalize miezi mitatu (baada ya chanjo) kabla ya kuanza kupokea wageni wa kuja kuniona...

Sababu ni kuhitaji tu kupumzika mimi binafsi na kuacha mtoto akomae kwanza

Kitovu ni wewe tu, ukichoma au ukiflash uwani fresh

Mtoto kukua vyema ni lishe tu na kumpa muda wako kama mzazi, then mengine nature itaamua

Yaliyobaki wenye uzoefu watajibu
 
Back
Top Bottom