Umeshasema kuna tamaduni mbalimbali na tathmini isiyo rasmi.
Uta assume vipi kwamba kuna kitu kimoja, cha kwanza kabisa? Kwanza ndoa yenyewe ni dhana pana sana na hata hujai define vizuri unaiongelea kwa wigo upi hapa.
Kwa mfano, unapoongelea ndoa unaongelea ndoa za kidini? Kisheria? Kitamaduni? Common law marriage ni kati ya ndoa unazoongelea ama la?
Mtu akikwambia hakuna kitu kimoja kinachosukuma watu kuoa. Wengine wanaoa kufuata utamaduni.Wengine wanataka kuheshimika, wengine wanataka kupata mtoto ndani ya ndoa, wengine wanataka msaada wa mwanandoa, wengine wanataka makaratasi, wengine wanakuwa pressured na jamii there are so may reasons for so many people. Unaposema "cha kwanza kabisa anaoa/kuolewa kwa ajili ya nini" naona kama unataka kufanya watu wote wanafikiri sawa na wana historia sawa inayowafanya waiangalie ndoa kwa jicho lile lile.
This could not be more misguided.