sio mzoefu sana ila kwa maoni yangu, biashara imebana kipato, matumizi ni mengi na nauli imewekewa kikomo. Pia, kuna wamiliki ambao wana njaa kiasi kwamba ndo biashara yao ya kula kila siku. Labda pia wanapandisha gharama zao za maisha hivyo gari likija kuhitaji service kubwa, anakuwa hela imembana. Ila ni biashara nzuri ukiwa na usimamizi mzuri na nidhamu ya fedha.