Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Katika mambo huwa yananishangaza na kunifikirisha sehemu mbalimbali za nchi hii ni uwepo wa majengo mengi ya nyumba za watu walionza kujenga kubaki bila kumaliziwa(mapagala) kwa muda mrefu sana na hatimaye kugeuka magofu.
Tatizo huwa ni nini?
Ni ujenzi wa kukurupuka?
Ujenzi bila kuwa na taarifa muhimu za kutosha? (Ile mtu anaambiwa ukipiga mahesabu sana hutajenga, we anza tu)
Kwa nini mtu anapoona amefikia mahali pumzi katika ujenzi imekata na hakuna dalili ya kuendelea muda mrefu ujao asiliuze tu jengo(pagala) lake na hiyo pesa akaitumia kujaribu kufanya mambo mengine?
Nachelea kusema sekta ya real estate Tanzania inaweza kuwa chanzo cha umasikini mkubwa kwa raia wengi wenye kipato cha kawaida waliojaribu kujiingiza katika hii sekta
Ni hasara kubwa sana kuwa na pagala lililogeuka gofu.