Nini chanzo cha ongezeko la Maafisa ubashiri (Wanaobeti) na maafisa usafirishaji (Bodaboda)..?

DR Mambo Jambo

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2012
Posts
11,622
Reaction score
26,005
Ni kwamba hizi biashara zinalipa sana au Ni kwa sababu vijana wetu wengi hawana shughuli mjini...?

Ni kwa sababu Hatuna njia nyingine ya kufikiri kujikimu kwa mahitaji yetu ya kila siku..?

Au ni kwa sababu ya Kuongezeka kwa Gharama za maisha?

Ushauri jinsi ya kujinasua au kuzifanya shughuli hizi bila kudhurika yaani kama maafisa usafirishaji wengi wanavyopata ajali na kupoteza maisha kwani hawajali afya zao??

pia nini kifanyike kupunguza uraibu wa hawa maafisa Ubashiri ambao Wanaongezeka kwa kasi sana...
Je kuna haja nao wakaunda chama chao kama hawa maafisa ubashiri ili kujifunza sheria na taratibu za biashara zao Asanteni na karibuni...

Baadhi ya Maafisa Ubashiri wakiwa kazini katika kusuka Odds Tata ili wapate Chochote kwa Kanjibhai...

Hawa ni baadhi ya maafisa Usafirishaji wakijitahidi katika majukumu yao...

Maisha mkuu!
 
Maisha yamefanyaje ?
Yanachangamoto,unaweza kufanye usichotegemea na hukipendi,mimi niliendesha bajaji ili nipate hela hiyo kazi sikuipenda ila watoto wangu walikuwa shule na mahitaji yanatakiwa!Ikanilazimu mkuu,mambo yakawa safi sana tena sanaa!
 
Ukitaka kufanya unayo upenda.. utalala njaa na kutia aibu mjini
 
Yanachangamoto,unaweza kufanye usichotegemea na hukipendi,mimi niliendesha bajaji ili nipate hela hiyo kazi sikuipenda ila watoto wangu walikuwa shule na mahitaji yanatakiwa!Ikanilazimu mkuu,mambo yakawa safi sana tena sanaa!
Safi sana mkuu...kungekuwa na Option ya kupin hii comments ningeipin mkuu hii inatia moyo watu wote wanaoona hizi kZi ni uhuni πŸ“ŒπŸ“ŒπŸ“Œ
 
Bodaboda ni kwasababu ya ukosefu wa ajira.
Kubeti ni urahabu kama ilivyo pombe ama mirungi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…