matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 7,968
- 19,368
Uchawi upo. Jambo la ajabu kwa sasa nimepata kesi zaidi ya tano ndugu kurogana.
Yaani kuna moja mama hataki kuona vijana wa kike na wa kiume wa wanatoboa.
Ndugu wanafichana mambo na kila mmoja anamuangalia mwenzake kama kihatarishi. Dada mmoja ameniambia Alfajiri anaona anakabwa na Mama yake mdogo, huku akimwambia lazima tukukwamishe tu utake usitake.
Mwingine mtu mzima hata kwenye msiba aliingia kimafia kwa hofu ndugu zake wamemuwekea mtego kwenye vyakula vya msibani wamuue. Yeye ndiye amesaomesha na kusomeshea watoto wao.
Kuna mmoja aliona kwenye ndoto ndugu anamletea zawadi ya chakula, hakumkuta akampa mwingine huyo aliyekila alikutwa amekufa kimazingara makaburini siku kadhaa. Hicho alichokiona kikatokea hivyohivyo.
Mwingine alitafuta mtoto wa ndugu yake anapofanyia kazi, akalazimisha kumpa pesa ya noti 10K, kumbe ile pesa ilikuwa imefanyiwa namna ili jamaa afukuzwe na kufirisika. Mama mwenye nyumba wa huyo jamaa usiku akaona tukio lote ndotoni. Asubuhi akaja kumuhadithia kila kitu wakati hakuwepo na hamjui huyo aliyetoa ile pesa. Akamwambia umewakosea nini ndugu zako mbona wanakutafuta sana. Jamaa akawa analia tu kwa uchungu.
Maisha ni vita vya kiroho. Muamini Mungu, usiamini ndugu, marafiki na watu wanaosema ni wa karibu kwako. Wengine wamwkusogelea ili wakujue vizuri wakikushambulia wafumue hadi mizizi.
Tumia Muda mwingi kwenye sala, kazi, na familia yako, ndugu chagua wale mnaoendana wengine wapende sio lazima wakujue sana.
Ni hayo tu
Mtumishi
Matunduizi.