Nini chanzo cha ongezeko la tuhuma za ndugu kurogana na kukwamishana?

Uchawi ni nini?

Unahakikishaje huo unaofikiri ni uchawi, ni uchawi kweli, na si kitu kingine usichokielewa tu?
Uchawi ni matumizi ya nguvu za ziada zilizonje ya ubinadamu kusababishia wanadamu wenzako mabaya, kuwaumiza, kwamisha kuwarudisha nyumq hata ikibidi kuwaua au kuwadhuru kabisa.

Mambo haya yamekuwepo katika kila jamii ya mwanadamu katika vipindi vyote vya uwepo wake.
Mfano Ulaya. Zamqnj za walatini walitumia neno la kisheria Maleficium
Kuwashughulikia kisheria waliojiingiza katika ushirikina. Wengi walikuwa ni wanawake wakiroga ndugu na majirani.
Ni mambo ya imani yanayopimwa kwa matokeo zaidi yaanq yanahusisha nguvu nje ya ubinadamu
 
Nguvu za ziada zilizo nje ya ubinadamu maana yake nini?

Nikimpiga mtu risasi ili kumsababishia mabaya, hapo nimesababisha mabaya kwa uchawi?

Bunduki na risasi zinatumia nguvu za ziada zilizo nje ya ubinadamu.
 
Ndugu, manuizi ya kichawi yanaathiri zaidi fikra. Bunduki inaathiri mwili.
Ukiweza kuzishinda fikra za kichawi, utafanikiwa.
Ila, uchawi upo. Watu wanaloga hadi visima visitoe maji.
 
HICHO KITU MNAITA MIZIMU mkidai ni roho marehemu ni majini yanajigeuza kwa sura za marehemu
jiepushe nazo
 
Ndugu, manuizi ya kichawi yanaathiri zaidi fikra. Bunduki inaathiri mwili.
Ukiweza kuzishinda fikra za kichawi, utafanikiwa.
Ila, uchawi upo. Watu wanaloga hadi visima visitoe maji.
Kwanza kabisa, sijakuuliza wewe. Nimemuuliza aliyenijibu hapo awali kwamba uchawi ni matumizi ya nguvu za ziada zilizo nje ya ubinadamu.

Sasa, ukija wewe kujichomeka katika majibizano, wakati wewe si uliyenijibu hivyo awali, unaondoa mtiririko wa majibizano.
 
Afya ya akili
 
Ndugu, manuizi ya kichawi yanaathiri zaidi fikra. Bunduki inaathiri mwili.
Ukiweza kuzishinda fikra za kichawi, utafanikiwa.
Ila, uchawi upo. Watu wanaloga hadi visima visitoe maji.
Uchawi ni nini?

Unahakikisha vipi kisima hakitoi maji kwa sababu ya uchawi na si kwa sababu nyingine yoyote?
 
Hakuna logic ni uongo , ndugu yako haweza kukuroga ni mbinu wanatumia waganga wa hovyo kuwagombanisha .Watu , ndugu wanapata furaha wakisikia ndugu zao wanapiga maendeleo hata watu wa jamii yao .

Leo unasema eti wanarogana , ndugu yako sio adui yako .
 
Chanzo ni kuwasikiliza sana hawa manabii uchwara wanaotuambia eti uchawi na ushirikina wa mababu zetu walioturishisha! Na sisi kwa ujinga wetu tunawaamini.
 
Mkuu uliwahi kusikia mtu karogwa ulaya au Marekani kaskazini huko?

Kama kuroga kupo, kulikoni tusiwaroge japo watekaji wetu?
 
Uchawi haupo wacha kupoteza muda wako...Fanya kazi...kushindwa kwako kimaisha usitafute kichaka cha uchawi kujifichia humo...tatua changamoto zako....tumia akili .

Uchawi haupo, haujawai kuwepo na hautokaa kuwepo
Imani potofu hii.
 
Mkuu uliwahi kusikia mtu karogwa ulaya au Marekani kaskazini huko?

Kama kuroga kupo, kulikoni tusiwaroge japo watekaji wetu?
Kwa Mujibu wa Pew Research Center dini inayokua kwa kasi Marekani ni dini ya wachawi WICCA.
 
Ukiona Ukoo/Familia Ina Umasikini ndani yake, na Waliotoboa wanahesabika Tena wametoboa Kwa mbinde, na inawabidi kama Wajitenge hivi na Familia ili wa survive... MEANS KUNA UCHAWI KWENYE FAMILIA....!
I kweli
 
masikini wana fikra za ajabu sana yaani imagine watu wanaroga hadi mbwa mahindi siji maua etc IMAGINE.
 
Ni kweli wazungu wanafanya kama hobby au burudani tu. Umasikini unaqnzia kwenye qkili. Kama jamii yote ikiamini imerogwa, au jamii ikaamini hakuna mtu kutoboa lazima abrokiwe hata kwa majini hapo lazima nchi ibaki shamba la bibi la wachina na wazungu.

Hayo yatafikiwa viongozi wa kisiasa na kidini wakiacha kwenda kwa waganga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…