nimegundua vijana wengi na watu wazima ambao sio wazee ambao hunyoa kipara kichwa chote muda wote huwa wanavipara kama vya wazee ikitokea wameacha kunyoa nywele. Asilimia kubwa.
Jana nikiwa kwa babashopu dogo ananiambia unakakipara kanaanza katikati ya kichwa alafu kuna uchochoro mwingine unaanzia mbele kwa mbali ila muda sio mrefu vitaungana na utamiliki kipara cha muda wote.
Kwa kweli siko tayari Kunyoa kipara kichwa changu chote, maana ni kinyume na mila ninazoziheshimu sana.
Wakuu.
1: Chanzo ni nini? maana hata ukoo wetu hauna watu hao.
2: Kuna dawa yoyote ya asilia, maana ya kizungu kama aloyopaka rooney siitaki.
3: Kikija Sinyoi nywele kichwa chote bali nitaendeleza kufuga kama kawaida, Je wanaonyoa wanaogopa nini?
CHANZO NA SABABU ZA KUOTA UPALA KATIKA UMRI MDOGO
Lishe duni,
Nafasi kubwa ya nywele imajengwa kwa protini, pia kuna virutubisho vingine vingi vinavyosaidia uzalishaji wa nywele, kama madini ya zinki, chuma, potasiamu, vitamin E, B, C na hewa ya oksigeni. virutubisho hivi tunavipata kutokana na vyakula tunavyokula kila siku. baada ya kuliwa, virutubisho hivi husambazwa kwenye ngozi ya fuvu la kichwa (Scarp) kwa njia ya damu. Mtu yeyote akikosa virutubisho hivi kwa kiwango kinachotakiwa lazima atapatwa tatizo la kupukutika kwa nywele.
Tambua kuwa madawa na mafuta mengi ya nywele tunayoyatumia hutengenezwa kwa tutumia vyakula vyenye virutubisho hivi, hakuna uchawi mwingine. Katika Makala ijayo nitakueleza kwa undani zaidi ni vyakula gani unavyopaswa kula ili uweze kuwa na nywele nzuri, wala hakuna haja ya kuhangaika na madawa.
Msongo wa Mawazo. (Stress),
Msongo wa mawazo ni chanzo kingine kikubwa sana cha tatizo la nywele na ndicho haswa kinachowakumba vijana wengi wa sasa na kuwasababishia vipara katika umri mdogo. Kitaaramu imegundulika kuwa msongo wa mawazo unaathiri mzunguko wa damu kwenye ngozi ya vuvu la kichwa hivo damu hushidwa kufikisha virutubisho na hewa ya kutosha kwa ajiri ya uzalishaji wa nywele.
Kikawaida binadamu anapokuwa anawaza sana misuli iliyozunguka fuvu la kichwa kusinyaa na kukunjamana kitu ambacho husababisha ngozi na mishipa midogo midoho ya damu kusinyaa na kukunjamana pia hivyo damu inashidwa kupenya na kusambaa kwa urahisi katika maeneo yote ya ngozi ya kichwa kitu kinachopelekea upungufu wa virutubisho na hewa kwa ajili ya ukuaji wa nywele na hatimaye nywele huanza kudhoofika. baadhi ya wasomi na watu wanaopigana sana na ugumu wa maisha hupata vipara kwa njia hii.
Matatizo katika mfumo wa homoni,
Homoni zinahusika sana na kukuaji wa nywele. Upugnufu ama madiliko katika homoni husababisha kudhoofu kwa nywele, kuna sababu nyingi zinazoathiri mfumo wa homoni, mfano Magonjwa, Ujauzito, mwili kukosa hewa ya oksigeni yakutosha pamoja na uvutaji wa sigara.
Kurithi toka kwa wazazi,
Pia inaaminika bainadamu anaweza kurithi tatizo la upara kutoka kwa kizazi chake kilichotangulia. Lakini hapa huwa najiuliza sana sabubu kuna baadhi ya watu wamepata vipara wakati kwenye ukoo wao hakujatokea mtu mwenye upara.
Ukiwa na Shida yoyote ile
Usipo pona kwa Dawa za Hospitali nitafute mimi nipate kukutibia upate kupona ukihitaji matibabu yangu
Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Herbalist Dr. MziziMkavu Email barua ya
pepe.fewgoodman@hotmail.com What's App +905344508169 Au Ni add Kwa Facebook tumia jina hili Herbalist mzizimkavu. Au boonyeza hapa.
Herbalist MziziMkavu