Nini chanzo na tiba ya kutapika?

Nini chanzo na tiba ya kutapika?

kachui

Member
Joined
Apr 10, 2015
Posts
64
Reaction score
3
Nina mdogo wangu akila tu chakula anatapika Mara kwa Mara ,hali hii inanipa wasiwasi kwa mdogo wangu, jamani naombeni dawa mbadala nimsaidie mdogo wangu wana JF Mungu awabariki sana.
 
hebu akapime kwanza labda anaumwa..
pia asitumie chakula chenye mafuta mafuta..

lakini kwa dharula tu anaweza kutumia dawa inaitwa FENEGAN, ameze kidonge kimoja tu kwa siku, lakini asizoee aende na hospitali kujua tatizo ni nini.
 
Asante sana ndg mungu akubariki
 
Ni wa kike?umri gani?asije akawa ni mjamzito maana siku hizi hata kakiwa kana miaka 10 mimba ndiii
 
Hilo tatizo unanikumbusha binamu yangu mmoja yeye kila alipokuwa akiona nyoka anatapika vibaya sana. Mzee alivyofanya uchunguzi kujua chanzo nini kumbe kuna siku alienda kwa bibi akamuandalia kitoeo cha samaki flani jamii ya nyoka wanaitwa "kamongo au mkunga" bahati mbaya yule samaki alinona mafuta mengi hivyo binamu alikula akapitiliza baadae akashikwa na ugonjwa wa kuhara na kutapika mfululizo! so binam ikawa kila akiona nyoka anakumbuka samaki wa bibi.
Tatizo tulilimaliza kwa kumtengenezea tiba mbadala kwa kuchemsha mizizi ya ng'watya na ng'wihunge(mambo ya usukumani haya) akanywa.

Ushauri wangu; mpeleke mdogo wako hospitali akapate tiba. Vilevile ni vizuri kuchunguza chanzo cha tatizo tangu siku ya kwanza hali hiyo kujitokeza.
 
Jamani na mimi mama yangu akila chakula sanasana kikiwa kigumu anatapika, hospital nyingi wanasema hana tatizo na yeye hasikii maumivu popote, hali ya kutapika imepungua kaanza kuharisha ni mtu mzima kiumri
 
pole mkuu.. hebu toa mfano wa hicho chakula kigumu.. na je anakunywa na kinywaji gani? je anatapika wakati wa kula au baada ya kula.
ok wakati ukiendelea kumtafutia ufumbuzi unaweza pia ukatumia ndimu/limao, ukachanganya kwenye chakula japo sio tiba kabisa.
 
endapo unatapika wakati wa kugegedwa dawa yake ipo
 
Back
Top Bottom