Nini chanzo na tiba ya kuvimba Tumbo pamoja na Miguu..

Nini chanzo na tiba ya kuvimba Tumbo pamoja na Miguu..

Mgodo visa

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2016
Posts
3,590
Reaction score
3,632
Kama kichwa/Mada inavyo jieleza hapo juu..

Yuko ndugu (dada) yangu anasumbuliwa na tatizo la Tumbo pamoja na Miguu kuvimba, kwa zaidi ya miaka mitatu sasa (hii ilikuwa ni baada ya kujifungua)

Tumejaribu kwenda ama kutumia tiba mbalimbali (za kienyeji na kisasa) ila bila mafanikio.

Naomba kupitia JF Docter, yule anaeweza kutambua tiba ya matatizo haya, anifahamishe.

Tumekwenda hospitali mbalimbali ikiwemo Muhimbili, kila wanapo fanya uchunguzi, vipimo havioneshi tatizo.

Natanguliza shukrani kwanza kwa wote..
 
Kama MUHIMBILI imeshindikana me nani wakuweza kutoa Dx..........Ila jaribu kwenda kumpima vipimo vya moyo kama Echocardiograph na Electrocardiogram huwenda akawa na matatizo ya moyo
 
Inawezekana moyo, figo na ini vinashida tumia maji lita 5 kwa siku pia juice ya kitunguu saumu na tangawizi
 
Kichocho hicho.Mpe dawa ya kichocho.hiyo ni moja ya complications za kichocho kupata ascitis au kujaa maji tumboni kwenye peritoneal cavity.
 
ninamashaka na unachosema kwamba mpaka muhimbili hawajajua tatizo ni nini.

ndio huenda tatizo ni moyo(kwa asilimia kubwa) , ini au figo, sasa hapa inategemea namna anavyojieleza kwa daktari, na majibu ya maswali atakayoulizwa na uwepo wa dalili nyingine ambazo daktari ataziona kwa mgonjwa.

sasa humu ni mtandaoni tu, huyo mtu anahitaji aonane na daktari afanyiwe uchunguzi vizuri.

si lazima iwe hospitali kubwa, hata ya wilaya tu.

itakapolazimu kuonana na specialists basi aende kwa private hospitals
 
Inawezekana moyo, figo na ini vinashida tumia maji lita 5 kwa siku pia juice ya kitunguu saumu na tangawizi
mkuu hiyo amount ungejua kwanza urine output ya mhusika kabla ya kuhisi ni renal failure, maana anaweka akapiga hiyo kumbe shida ni moyo akawa anaongeza tu cardiac pre load na kufanya tatizo kuwa baya zaidi.
 
Mkuu kama muhimbili ambapo kuna maprofesa mambo kama hayo umesema wameshindwa..
Basi diagnosis zetu yutakazotoa hum zitakuwa marudio tu labda kama unataka tiba mbadala ya kina mshana jr..

Mimi dx yangu nasuspect hepatosplenomegaly (kuvimba kwa ini na bandama) inayopelekea edema(kujaa kwa maji) ya miguu
 
Back
Top Bottom