Nini chanzo/ sababu za kukosa hamu ya chakula?

blessed lenny

Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
38
Reaction score
8
tafathali sana naombeni msaada wenu, mimi huwa sina hamu ya kula na mara nyingi huwa nasikia tumbo limejaa, asubuhi nasikia uchovu sana na tumbo linakuwa linauma ila nikiamka tu linatulia
 
habari zenu wana jukwaa, ni imani yangu kwamba mu wazima wa afya!

mwenzenu nimekumbwa na tatizo la muda mrefu sana toka mwaka 2004 nikiwa darasa la sita, nimekuwa nakosa hamu ya chakula kabisa, ama hata pale ninapokula, basi nakula kidogo saaana na endapo nikijilazimisha kula, huwa najisikia kutapika!

ndugu zangu, tatizo hili limenisumbua sana, nimezunguka baadhi ya hospitali hapa jijini na nimepewa ushauri na tiba za kitaalamu, lakini naona mambo ni yale yale tu hamna mabadiliko! yani kula kwangu imekuwa nafikia kipindi naweza kaa kuanzia asubuhi mpaka hata jioni ndio nakumbuka kula, tena napo kidogo tu!


naombeni ushauri wenu ndugu zangu na tiba mbadala ili nisije zidisha tatizo!
 

kama upo mjin hiyo ni faida but kama upo kijijin hiyo ni hasara!
 
kama upo mjin hiyo ni faida but kama upo kijijin hiyo ni hasara!

not well said mkuu! hivi haujui kama mtu asipokula kwa muda mrefu huenda akapata vidonda vya tumbo??

hiki hasa ndicho kinachonipa wasiwasi kwa sababu sijapata mustakabali halisi wa future yangu!
 
Habari zenu ,Doctors.

Jamani mwenzenu nina tatizo la kukosa hamu ya kula chakula. Mara nyingine naweza kula kwa kiasi kidogo sana , na nikijilazimisha naweza hisi hali ya kutapika.

Naombeni msaada wenu wa kimawazo nifanyeje?

Asanteni.
 
Uende hospitali ukapate vipimo sbb zinaweza kuwa nyingi,homa,minyoo na sbb nyingine nyingi!pole sana
 
Kunywa dawa ya minyoo,tafuta wamasai wakupe dawa kwan dawa za wamasai ni za asili na bei rahisi.Pendelea kunywa juice ya kutengenezwa na matunda fresh baada ya kula huongeza hamu ya kula.Tatizo la kutaka kutapika husabaishwa na nyongo.Wamasai wana dawa nzuri sana.Mwisho pendelea kula chakula ambacho unakipenda sana mara kwa mara na usiwaze hilo kama ni tatizo litaisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…