Nini Chimbuko la Matumizi Mabaya ya Madaraka Tanzania?

Nini Chimbuko la Matumizi Mabaya ya Madaraka Tanzania?

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Joined
Aug 7, 2018
Posts
685
Reaction score
1,124
Kwa nyakati tofauti kumekuwa na Viongozi walionukuliwa wakisema "Nchi hii imechezewa sana, Nchi iligeuzwa Shamba la Bibi lakini wahusika hawatajwi. Wapo waliowahi kutoa kauli za Vitisho ikiwemo Unanijua Mimi ni Nani?" na wengine waliwahi kutuhumiwa kutumia Mamlaka yao kuvunja Sheria za nchi hadharani

Je, unadhani mambo hayo yanasababishwa na nini na kwanini hakuna Uwajibishwaji wa wazi kwa wahusika?

20240606_175743.jpg

Jiunge nasi katika Mjadala utakaojadili Chimbuko la Matumizi Mabaya ya Madaraka, ungana nasi leo Juni 6, 2024 Saa 12:00 Jioni hadi Saa 2:00 Usiku kupitia #XSpaces ya JamiiForums

Link ya Mjadala jamii.app/JFMadaraka

=======

Mjadala umeanza kwa muongoza mjadala, Ipyana Gwaselya kumkaribisha Tito Magoti baada ya kuufungua.

Tito Magoti(Mtetezi wa haki za Kibinadamu): Mada ni pana, nitaangazia kwa upande niliouchagua, matumizi mabaya ya madaraka kwa viongozi wa Umma. Kumekuwa na matumizi mabaya ya madaraka kwa muda mrefu kwasababu ya kukosekana uwajibikaji. Imeonekana na kawaida kukiuka miiko ya maadili bila kuwajibishwa na mhusika akaendelea na uongozi.

Tuna mifumo butu, bunge ni kama halipo, hatuoni chachu ya Bunge kusimamia uwajibikaji hata tukitazama ripoti za CAG.

Utamaduni huu umekuwa kama sehemu ya utamaduni wa uongozi wetu(matumizi mabaya ya madaraka).

Ipyana Gwaselya: Kuna viongozi waliwahi kutuhumiwa kwa matumizi ya madaraka nchini na Je waliwajibishwa inavyopaswa?

Eugine Kabendera: Nawapongeza Jamii kwa kuendesha mijadala hii. Nawakumbuka haraka haraka Basil Mramba na mwenzake ambao walipewa adhabu ya kufagia lakini hatujawahi kuona hukumu kama ya jana aliyefungwa miaka 7 kwa kutapeli milioni nne za Ridhwani Kikwete.

Napenda nimguse leo Paul Makonda, hali aliyokuwa nayo miaka 10 iliyopita na leo ni vitu viwili tofauti, unaweza ukajiuliza huyu mtu ana biashara gani!

Chimbuko
Namna na jinsi viongozi hawa wanavyopatikana. Binadamu tuna tamaa hatukatai lakini sheria na hukumu zake ziko vipi? Kama adhabu ni kwenda kufagia Palestina! Sheria zimekuwa bubu na butu.

Viongozi lazima wawe na shughuli za kufanya.

Ipyana Gwaselya: Sheria za Tanzania zina Nguvu ya kupambana na matumizi mabaya ya madaraka

Thomas: Mimi naweza kusema Sheria za kuwafuatilia wanaofanya Madudu zipo ili Changamoto ni pale ambapo hatua zikichukuliwa Wananchi hawapati Taarifa

Kila Mwaka tuna tukio la Ripoti za CAG na huwa anasema kwenye Ripoti iliyopita ni mambo mangapi yalishughulikiwa. Shida hatufanyi 'publication' ya hatua zilizochukuliwa

Mara nyingi hatua tunaona zinachukuliwa kwa Viongozi wa nafasi za Uteuzi kwasababu Ajira ya Mtumishi wa Umma kuna process ndefu ya kumuondoa

Ili kuweka public trust, hatua zozote zikichukuliwa visisubiri ripoti ya CAG ya mwakani.

Abdul Nondo: Matumizi mabaya ya madaraka ni kutumia cheo vibaya kuumiza watu kukidhi matakwa yake. Hautoi huduma, fedha za kutoa huduma unazitumia kwa maslahi binafsi.

Tatizo kubwa ninaloliona kama chanzo cha Matumizi mabaya ya Madaraka ni kutokuwa na Mifumo Imara ya Utaasisi kama Katiba Imara, Tamaduni Imara na Sheria imara. Viongozi wanatumia utashi wao badala ya kutumia Utaratibu

Sheria zetu zina mianya mingi zinazofanya viongozi kuongoza kwa utashi wao.

Huwezi kuzungumza matumizi mabaya bila kuongelea upatikaji wa viongozi. Kiongozi wa kumteua mtu kwasababu tu ni kada, ndugu. Hawi royal kwa wananchi bali kwa aliyemteua.

Polisi anapofanya Mauaji kwa Raia kunatakiwa kuwe na Chombo tofauti na Polisi wenyewe ambacho kitafanya Uchunguzi na kuleta Uwajibikaji kwa wahusika

Katiba Imara ndio itakayofanya Viongozi walioko Madaraka wajione kwamba wao ni Agent na kumpa Madaraka Mwananchi

Tusipotambua Power ya Mwananchi hawa Viongozi wataendelea kuwa hivi walivyo

Kamala Dickson: Kuna mambo ambayo ni Mtambuka. Mfano kwenye kipindi fulani kuanzia kwa JK Taasisi zilikuwa na Uhai na unaona hata Watu ambao imezalisha kwa ajili ya Uwajibikaji

Ukiangalia Vyombo vya Habari kipindi hicho unaona kulikuwa na Jicho la Uwajibikaji ambao ulitokana na Watendaji kuanzia Mwandishi mpaka kwa Mlaji

Tumeona Wakurugenzi fulani ambao baada ya CAG kutoa Ripoti wamehamishwa Vituo badala ya kuchukuliwa hatua. Kama Wewe umeteuliwa na unataka kumuwajibusha mwenzio ambaye naye ameteuliwa halafu kahamishwa Kituo inakuwa ngumu kumchukulia hatua.

Tito Magoti: Sheria zetu zipo lakini zinajitegemeza kwa Viongozi wa Kisiasa hasa Rais, Uwajibikaji nao umetegemea neno la Rais, akitia neno utaona Mawaziri na kila Mtu anahangaika kuonesha kwamba anafuatilia

Niambie ni Polisi gani ambaye anaweza kwenda kumkamata Mkuu wa Wilaya au Kiongozi yeyote Mwanadamizi wa Serikali?

Lakini Mimi nikiandika hapa hata Tweet nitachukuliwa kwasababu Sheria zetu zinabagua na Usawa mbele ya Sheria ulishakufa muda mrefu kwenye Nchi yetu.

Tunasikia skendo mbalimbali Mikoani kwamba huyu kaiba hiki au kafanya hivi lakini watasubiria mpaka Waziri Mkuu aende kutembelea hilo eneo

Watu wanapakatwa na kurudishwa Ofisini utadhani hawajawahi kufanya Matukio yoyote. Nani asiyejua kwamba Mkuu wa Mkoa wa Arusha aliwahi kuvamia Kituo cha Habari akiwa na Silaha, pia ameshatoa kauli nyingi mbaya mbaya dhidi ya Watu lakini leo hii amerudi Ofisini

Tulihitaji uthibitisho gani kujua kwamba huyu Mtu hafai kushika Madaraka.

Niambie ni skendo gani kubwa ambayo ilishughulikiwa mpaka ikaacha historia. Mwenzangu amesema hapa Watu walifanya makosa halafu wakapewa adhabu ya kwenda kufagia Hospital ya Palestina, haya ni Maigizo

Askari walimuua Mwanafunzi wa NIT, Akwilina halafu wakaenda wakafungua kesi ila Mwendesha Mashtaka anakuja anaifuta kwamba hana nia ya kuendelea na hiyo kesi.

Kuna Polisi wana kesi kule Mtwara ila inazungushwa tu ila ifike mahali Watu tusahau. Tunaishi kama vile tupo Gheto.

Onesmo Mushi: Kuna kitu huwa tunakiangalia vibaya nacho ni tafsiri ya Madaraka, inaaminika wenye nguvu katika Nchi ndio wanaokuwa na nafasi ya kuiweka Serikali madarakani wakati kwa uhalisia ni Wananchi ndio wanaoiweka madarakani.

Kwa bahati mbaya Wananchi tumeruhusu viongozi na Taasisi zao kuchukua madaraka na maamuzi yetu, pia sisi Wananchi, tumeruhusu Serikali ituongoze kwa imani na siyo kwa kuchambua sera za kiongozi.

Eugene Kabendera: Umma wa Watanzania hauwezi kuufananisha na Umma wa Jamii nyingine kama vile ilivyo nchi kadhaa, sisi ni Watu wa kuvumilia na kumuachia Mungu, tunatakiwa kutoka huko na kuzungumza

Mfano mtu anaweza kukukanyaga kwenye Daladala na ukavumilia, unafika unapokwenda ndio unazungumza, unatakiwa kusema kuanzia mapema kuwa unaumia
 
Hakuna uwajibikaji, wangenyongwa kama 10 hivi bila kujali ni nani au mtoto wa nani watu wangeshika adabu.
 
Tatizo ni watanganyika wenyewe wamewalea viongozi Kwa uoga wao ndiyo maana wanacheza watakavyo.siku tukipatikana wajasiri kama watu wa Burkina Faso,Mali,niger, Cameroon au congo kishasa hawa viongozi hawataendelea na huo uhuni wao maana itakuwa kitendo Cha kuwashughulikia itakuwa ni nje nje.
 
Root cause ni Katiba ya nchi ambayo ni Mbaya na isiyofaa.
Huwa niko tofauti na hoja ya katiba, mbona vizuri vilivyomo havifatwi! Kila leo watu wanaenda kinyume na katiba na sheria ziko wazi ila hakuna wa kuadhibiwa.

Kenya hapo wametengeneza katiba lakini bado ngoma ngumu..
 
Huwa niko tofauti na hoja ya katiba, mbona vizuri vilivyomo havifatwi! Kila leo watu wanaenda kinyume na katiba na sheria ziko wazi ila hakuna wa kuadhibiwa.

Kenya hapo wametengeneza katiba lakini bado ngoma ngumu..
Ni kwa sababu Katiba mbovu ime-paralyse mifumo yote ya Kiutawala na kiutendaji iliyopo ktk nchi hii.
Hakuna mfumo hata mmoja unapofanya kazi.
 
Nimemkumbuka mheshimiwa, alirudia rudia nchi hii imechezewa sana halafu nae akaja kuichezea kwa mujibu wa CAG🙁
Magufuki alikuwa FISADI tu kuliko mafisadi wote waliowahi kutokea Tanzania. Alitumia UWONGO na propaganda kujifanya mzalendo na mchukia rushwa, lakini yeye ndiye alikuwa mpokea rushwa mkubwa.

Watanzania by 90% ni wajinga ndiyo maana waliamini kila ambacho Magufuli alichokuwa anawambia baada ya kuvitisha vyombo vya habari visifanye kazi kwa uhuru
 
Kamam kifungu Cha rais kutoshitakiwa akiwa au ametoka madarakani hakitaondolewa tutaendelea kuona matumizi mabaya madaraka. Ifike mahali kusiwe na mtu asiyeshitakiwa.
 
Huwa niko tofauti na hoja ya katiba, mbona vizuri vilivyomo havifatwi! Kila leo watu wanaenda kinyume na katiba na sheria ziko wazi ila hakuna wa kuadhibiwa.

Kenya hapo wametengeneza katiba lakini bado ngoma ngumu..
Uko sahihi.
Katiba peke yake bila watu wa kuisimamia ipasavyo ni kazi bure.
 
Hayo majamaa ya sisiemu inamaana hayajaongea kitu au yalikacha kuhudhuria kwa maelekezo kutoka juu maana hamjaweka updates yamechangia kitu gani?🤣
 
Baadhi ya mambo yanayochangia ni pamoja na:

Ukosefu wa uwazi na uwajibikaji: Katika baadhi ya matukio, viongozi hupewa madaraka makubwa bila utaratibu wa kutosha wa uwazi na uwajibikaji. Hii inaweza kuwapa fursa ya kutumia madaraka yao kwa manufaa yao binafsi bila hofu ya kukamatwa.

Udhaifu wa sheria: Sheria za kupambana na rushwa na matumizi mabaya ya madaraka zinaweza kuwa dhaifu au hazitekelezwi kwa ufanisi. Hii inaweza kuwafanya viongozi wahisi kuwa hawawezi kufikiwa na sheria na kuwapa ujasiri wa kutumia madaraka yao vibaya.

Rushwa na ufisadi: Rushwa inaweza kuwa imekita mizizi katika baadhi ya jamii, na watu wanaweza kuona ni kawaida kutoa au kupokea rushwa ili kupata huduma au kupendelea. Hii inaweza kuwafanya viongozi wahisi kuwa wanaweza kutumia madaraka yao vibaya bila kuadhibiwa.

Umaskini na ukosefu wa ajira: Watu maskini na wenye kunyimwa fursa wanaweza kuwa katika hatari kubwa ya kunyanyaswa na viongozi wanaotumia madaraka yao vibaya.
 
Back
Top Bottom