Nini chimbuko la Vita vya Uhujumu Uchumi - 1983-84?



Mkuu Mkandara, Asante pia kwa uchambuzi wako. Tatizo la rais wetu ni moja. Kuweka urafiki mbele sana kuliko masirahi ya taifa ( mfano issue ya wanamtandao) hao ndo wanayumbisha nchi hii kwa sababu karibu wengi wao ni wabaka uchumi.

Akiweza kuwachulia hatua tena kali hao wabaka uchumi, basi atakuwa ametuvusha kikwazo cha kwanza. Pili unafiki wa wabunge wetu ambao wengi ni rubber stamp za vyama vyao na wala hawasimami katika kupigania haki za mtanzania.

Tunasafari ndefu mzee. Kama ni hiyo safari basi tupo kwenye kilima kikali na gari alina break!
 


Mkandara ninakuelewa points zako. Na vilevile naelewa kuwa kuna factors nyingi.

Lakini hili mjadala uwe na maana ni lazima tuangalie factor inayo dominate kama hipo na kuacha factor nyingine.

Factor inayo dominate hapa ni wazalishaji kushindwa kukidhi mahitaji ya ndani.

Initially ilifikiriwa kuwa waliouza waliochukua bidhaa Tanzania na kuziuza nje ya nchi walisababisha upungufu wa bidhaa.

Vita vilipotangazwa hivyo vita 1983-84, mipaka ilifungwa na bidhaa zikawa zinauzwa ndani ya nchi. Pamoja na hizo juhudi bado upungufu ulikuwepo. Hivyo hoja yako inapoteza maana.

Kama unaona nawatukana viongozi kwa kutumia vitabu, let be it. Kuna simple rule ya kufanya analysis. Kama kuna kitu kinaleta negative impacts katika jamii, basi basi tumia approaches zitakazo reverse hizo impacts. Hizo approaches zako zikishindwa basi jua kuwa vile vitu ulivyo-assume kuwa vinaleta negative impacts sio vyenyewe.

Serikali ilifanya assumption kuwa uuzaji wa vitu nje ya nchi ulisababisha uhaba wa bidhaa Tanzania na kuuhujumu uchumi. Vita vya uhujumu uchumi zilikuwa ni approaches za ku-reverse negative impacts katika uchumi. Vita hivyo havikuwa na manufaa. Mipaka ilifungwa na bado bidhaa zilikuwa adimu. Kwa mtaji, I am afraid to say, assumptions za serikali na zako zilikuwa batili.
 
Naona umeaona tuegemee kwenye facts...sasa kuna taarifa hii ambayo ilisomwa bungeni na P Marmo...pengine itasaidia.

Uliyoleta facts sio kwa sababu inasema kuwa watanzania waliopeleka vitu nje. Lakini wakati huo volume ya thamani ya vitu vilivyopelekwa nje kwa magendo ilikuwa sawa na volume ya thamani vilivyorudi Tanzania kwa magendo.

Nimetoa mfano kuwa mitumba ilikuwa inapatikana Burundi na Rwanda. Na wafanya biashara wa mitumba walichukua Radio za National 277 na kuziuza huko. Pesa za kigeni walizopata walinunua nguo na viatu na kurudisha Tanzania.

Ingekuwa phenomena hii ni direction moja ningekubaliana na Mkandara. Lakini ilikuwa ni Bi-directional.
 


Shadow:

Matatizo sio rais wenu. Matatizo ni mfumo mzima wa utawala kuwa out-dated.
 
Zakumi,
Mkuu tunaongea vitu viwili tofauti?.. Hivi hapa wewe unatazama shilingi gani maanake nashindwa hata kukuelewa. Kwa mfano unaposema:- Factor inayo dominate hapa ni wazalishaji kushindwa kukidhi mahitaji ya ndani.

Mkuu hii sio sababu ya vita ya Uhujumu Uchumi na kama unajaribu kusema kuwa ile vita ilishindikana kwa sababu Uhaba wa vitu haukutokana na magendo bali uwezo wa viwanda vyetu kuzalisha then utakuwa unazidi kupotosha ikiwa kuna watu zaidi ya 4,000 walikamatwa. Hakuna solution ya Kiuchumi inayotoa dawa ya mali inayofichwa na supplier wala hakuna dawa ya kisomi inayojibu hilo isipokuwa rule of law kwani huo ni uhalifu. Huwezi kutumia demand na supply kukidhi mahitaji yenye mfumo wa magendo.

Na mimi hapa nimekuhakikishia kwamba magendo yalikuwepo tena ktk hali ya juu sana.
Biashara ya kubadilishana haikuwepo wala haikuwa ruksa kwa sababu miaka hiyo Tanzania tulifunga mipaka yetu na Kenya. Hata watalii tu wakija Tanzanai iliwalazimu wachukue visa ya kuingia TZ toka huko kwao...Kilichofanyika ni kinyume cha sheria au mfumo mzima wa uzalishaji nchini kwani vitu vilitengenezwa kwa ku target market ya ndani sio kupelekwa Kenya.
Kisha nimekwambia inbalance (Uhaba) wa demand na Supply siku zote unazungumziwa kitu kinachohusika..sio demand na supply itumike kwa vitu vyote kwa wakati mmoja kwani factors kama price, quality, wages na kadhalika haviwezi kuwa sawa kwa vitu vyote..
Wakati wanakamatwa watu kwa kupeleka Kenya mathlan Sukari, kulitokea Uhaba wa sukari nyumbani na sababu kubwa ilikuwa ni magendo.. hivyo hivyo tulikosa Colgate kwa sababu Tanzania hatukuwa na kiwanda cha Colgate wala supply wa Colgate pia hatuweza kuagiza nje kukidhi demand ya colgate.. inbalance ya vitu hivi viwili inakuwa na solution mbili tofauti..

Nitarudia kusema tunazungumzia zoezi la Vita ya uhujumu Uchumi ambayo binafsi naamini kabisa ilikufa kwa sababu walimwondoa Sokoine baada ya kuanza hatua ya pili kuwakamata vigogo, vita hiyo haikumalizika kama unavyodai wewe..Na ujamaa ulipokufa ndio kabisaaa mwalimu aliishiwa nguvu mafisadi wakachukua ushindi. Since then sijaona kama tume solve kitu. tanzania kwa mara ya kwanza chini ya Mkapa watu wamekufa njaa tena sio kidogo.. wengi sana na kisingizio kilikuwa Ukame. Ukame ktk nchi ambayo inatumia mfumo wa Utandawazi na soko huria wanaweza kuagiza chakula toka nje bado tulishindwa - Kama sio Ufisadi na kukosa uchungu wa raia wako ni kitu gani..Lini Tanzania tumekuwa na supply ya kutosha maanake naona bei za bidhaa ndio zinazidi kupanda tu mwaka hadi mwaka.

Kati ya watu 4,000 waliokamatwa wengi wao ni samaki wadogo na ndio wao waliobakia rumande lakini kati ya hao walioachiwa wengi ni vigogo ambao kwa kutumia rushwa tena waliweza kutoka na kulipwa fidia.. Hii ndio Tanzania yetu na tunapotaka kutafuta solution ni muhimu sana tukubali ukweli wa watu na mazingira yetu lakini tukitaka kutumia vitabu kutwist ukweli ambao ni wazi kabisa then we are doomed..
Nyerere alishindwa kuendeleza zoezi lile na sababi zinajulikana kabisa isipokuwa vigogo wengi wa wakati ule ndio wao leo hii mmawaziri. That is a fact na wataendelea kutubabaisha na siasa za Uchummi na kunyoosha vidole kwa mwalimu na Sokoine wakati hali ya nchi yetu haisongi mbele.
Toka Mkapa aingie madarakani viongozi wengi wanatukana sana Utawala wa Nyerere, yet hakuna zuri walofanya ambalo wanaweza kuwaonyesha wananchi zaidi ya hayo maghorofa ya wahindi..sasa hivi tunataka ku deal nao hawa mafisadi na solution ni kurudisha upya vita ya Uhujumu uchumi.. period wasitake kusema sijui chuki mara oooh uchumi wa dunia umeharibika.. hell no! tutakula nao sahani moja hadi kieleweke!
 

Mkandara:

Colgate zilikuwa zinapatikana Kenya. Lakini mfanyabiashara wa Tanzania aliyetaka kuingiza colgate kutoka Kenya alibidi awe na Shillingi za Kenya. Na njia mojawapo iliyotumika kupata shilingi za Kenya ilikuwa ni kuchukua za bidhaa za Tanzania zinazoweza kuuzika Kenya. Hivyo wafanyabiashara waliuza matairi au ngozi.

Waliporudi Tanzania walileta Colgate. Katika scenario kama hii huwezi kusema kuwa upungufu wa matairi ulisababishwa na wafanyabiashara wa Tanzania kuuza matairi Kenya kwa sababu hata watanzania wangeacha kuuza bado upungufu wa matairi ungekuwepo kwa sababu ulikuwa unategemea mambo chungu mzima yakiwepo upatikanaji wa pesa za kigeni kutoka BOT ambazo zilikuwa katika short supply.

Kama colgate zingekuwa zinapatikana Tanzania, hakuna mfanya biashara wa Tanzania ambaye angejisumbua kwenda Kenya kwa sababu ya kupata shillingi za Kenya tu.

Kwa mfano huo hapo juu, hili kufanya bidhaa za Tanzania zisiuzwe nje ya nchi na kusababisha upungufu wa bidhaa hizo, uzalishaji wa bidhaa zote muhimu ulitakiwa kutosheleza mahitaji ya watanzania.

Huwezi kusema kuwa sasa hatuna technologia ya colgate basi watu watumie majivu au chaki. Na ukisema hivyo kumbuka atatokea mtu atakayechukua dhahabu Tanzania na kuiuza nje ya nchi na kuturudishia colgate.

Wakati wa uhujumu uchumi, magendo yalikuwa bi-directional. Vitu vilitoka Tanzania kwa magendo na kuingia kwa magendo. Na waliofanya hivyo walikuwa ni walewale.

Na vilevile ingekuwa ni waKenya wanaokuja na colgate Tanzania na kurudi Kenya na Matairi, usemi wako ungekuwa na nguvu.

Watanzania Walikuwa ni wenye shida ya vitu na ndio waliopeleka vitu nje na kurudi na vitu vingine.
 

- Mkuu Joka, samahani sikuwepo kidogo lakini hapa tupo ukurasa mmoja sana.
 
Zakumi,
Sasa wewe ebu nifahamishe yale matairi yaliyopelekwa Kenya yalitengenezwa kwa hela za Kenya! na Upungufu huo ungekuwepo vipi kama matairi yameweza kutengenezwa kulingana na demand ya ndani... hata sikuelewi mkuu..

Kwa mfano huo hapo juu, hili kufanya bidhaa za Tanzania zisiuzwe nje ya nchi na kusababisha upungufu wa bidhaa hizo, uzalishaji wa bidhaa zote muhimu ulitakiwa kutosheleza mahitaji ya watanzania.
Mkuu nimekwambia kuwa bidhaa zinazozungumzia ni zile zenye soko ndani sio kwa ajili ya export.au unahesabu na magendo kuwepo katika hesabu ya uzalishaji yaani kama magendo yanachukua matairi 1000 ya nyumbani kunahitajika matairi 1000 basi yatengenezwe matairi 2000!.. Duh hii tena siasa ktk Uchumi mkuu wangu, hakuna solution ya kiuchumi inayoweza ku solve taizo la magendo (corruptuion) kwani haina kipimo isipokuwa sheria..Basi hata sisi tunaoibiwa simu inatakiwa tuwe na simu mbili tatu sijui nne maanake ikiibiwa moja unazo kibao ndani ya nyumba...
Mkuu wangu hata siku moja magendo kama biashara haramu hayaendi nje ya bi directional, sehemu moja watakuwa wanahitaji kitu fulani na kwingine kunahitajika kitu kingine kwa hiyo unapozungumzia Uhaba wa supply na demand ni kitu kile kinachokwenda na kinachorudi. In this case Tanzania tulikuwa na uhaba wa colgate na sio Matairi, hivyo kupeleka matairi Kenya kulizusha sababu kubwa ya Uhaba wa matairi nyumbani nje ya mipango ya uzalishaji..Hii ni common sense tu kabla hujatafuta dawa ya ku balance demand na supply..Huwezi kupeleka Kenya dawa za mswaki ukarudi na dawa za mswaki ama ukaenda na Matairi ukarudi na matairi ili kuonyesha kwamba kote kulikuwa hakuna shida (demand).
Mhusika wa biasharara awe Mkenya au Mtanzania haiwezi kupotosha maana ya magendo. wanaoingiza Unga Marekani ni WaColombia, Wamarekani wenyewe, Wa Mexico na kadhalika yote hii haipotoshi ukweli kwamba Marekani kuna demand kubwa ya Cocaine sasa unapotaka kufahamu kwa nini kuna demand kubwa hivyo ndio hapo unaingia ndani kutafuta sababu zilizotangulia kukuza soko hilo na inaweza kuwa Uharamu wake.. Sasa unaposema kupiga vita haifai bali ni swala la demand na supply mkuu dunia itakuwa haina sheria tena. Watu waki rape wanawake utasema wana Ukame - solution wapeni wanawake!..binadamu mkuu haridhiki na ndio maana tuna sheria na magereza kibao..
 
Thank you very much.

Vipi kuhusu current uhujumu wa uchumi, chimbuko lake linafafana na chimbuko la uhujumu uchumi 1983/84 ?
 
Mama,
Wahusika wengi ni wale wale toka miaka hiyo kwani leo hii ndio viongozi wetu wakishirikiana na matajiri wahindi corrupt toka enzi za mwalimu..walitoka uongozi wa mashirika baada ya kuyaua leo hii ni mawaziri.. kwa hiyo wanafanya ku pass madhambi yao na warithi wake ni wengi mno utafikiri kuna kizazi kipya..
 

Duh, kazi kweli kweli.....

Kwa hiyo ili hii dhambi ya uhujumu uchumi iondoke tusubiri kizazi hicho kiwe wiped out by nature pamoja na warithi wao!

Je Tanzania yenye neema itaonekana nchi hii ikiongozwa na vijana waliozaliwa more less sawa na CCM ? I mean vijana waliozaliwa kuanzia mid-seventies au tusubiri kizazi cha eighties todate ?
 
Kusema kweli nionavyo Tanzania itapata mabadiliko tu siku kiongozi atakuwa Mtanzania aliyekwisha ishi nchi za nje na anafahamu nini uongozi bora.

Labda tuikodishe Ikulu kwa wazungu under contract kwa miaka mitano maanake siku niliyoona Darwin's Nightmare nikaona mkulu fulani mtu wa kuheshimika akisema ovyo basi nilikata tamaa. Nikategemea kizazi hiki lakini nacho siku hizi naona wengi wameingia ktk mfuko wa ufisadi..sasa itabidi turuke hadi kizazi kinachokuja yaani wale waliozaliwa wakati wa shida mid 80s na 90s..
Pengine ndivyo tulivyo maanake nikitazama Haiti imepata Uhuru miaka mingi kuliko nchi nyingi sana hapa duniani lakini hadi leo hii ni gunia la chawa wakati jirani zao Dominican Republic wamefanikiwa..Huko kwingine wala sitaki kwenda nadhani kuna laana fulani!...hakuna hata nchi moja Afrika ya weusi yenye nafuu jamani...
Mtanisamehe...Inauma sana.
 
Mkandara kaka, nausoma uzalendo wako. Mimi nakushauri uwe huyo kiongozi unayemtaja hapo, Au Rev au mwingine yeyote. Aliyeishi nchi za nje. Kuna vijana wengi tu humu wanaweza pia, kwa pamoja itawezekana. Tanzania yenye neema itayowafaidisha wananchi wote na sio watanzania wachache au wageni, iko mikononi mwenu. Shime jamani wakati ndio huu......
 


Mkuu Mkandara, Tatizo ni ubinafsi na choyo tulionayo. Ebu Tizama Nigeria, Congo na Angola. Nchi hizi tatu ni taji wa maliasili pamoja na kilimo. Patrice Lumumba alikuwa na mawazo mema kwa nchi yake lakini kibaraka Mobutu akawauza wacongo wenzake kwa zawadi ya kutawala atakavyo. Unajua mtu mweusi anaona raha sana kila kukicha anafunguliwa milango ya ikulu za magharibi lakini kutizama watu wake ilo halimo.

Tumeua mifumo mingi. ebu niambie kila kukicha wasomi wetu wako wekney migomo unategemea nini? Tunazalisha watu wa namna gani? Nchi mifumo ya utawala na uongozi bora haipo. Tuko kwenye zama za bora liende. Mfano nani alijua kwamba madudu ya awamu ya nne yangeonekana mapema hivi? hata kikija kizazi cha 1990s ni walewale kasoro tarehe. Kuna kazi kubwa sana ya kubadili mentality za watu hawa.
 
Mama,
Duh! mbona hunitakii mema maanake kuongoza sijui zaidi ya jazba..Kiongozi anatakiwa mtu mwenye subira, uvumilivu na mwisho ya yote moyo wa kujitoa mhanga..Mimi hapa maji yakifika shingoni nitaingia kizani...kwi kwi kwi!
Siwezi kabisa kazi hiyo napenda kuwa nyuma na kusema sana! labda kazi ya redio ya Taifa itanifaa au msemaji wa rais mtarajiwa itanifaa!
 
Hahahahaaaa.

Tumelia sana jamani, huu ni muda wa kuchukua hatua, kufanya mambo kwa vitendo. Tusianze kukimbiana tena jamani.

Dawa ya tatizo ni suluhisho. Na suluhisho hapa ni mabadiliko ya uongozi, na uongozi huo unahitaji wazalendo...wenye uchungu wa kweli na nchi hii. Mwenye kujiona anaweza jamani na ajitokeze. Hata kama sio kwa ajili ya 2010 ( it is too late kama mmoja hajaanza maandalizi); basi aanze kujiandaa kwa ajili ya 2015.
 

Mama:

Kama umesoma posti zake, Mkandara mwenyewe alikuwa anahujumu nchi.
 

Kama Field Marshall ES is in the same page na Jokakuu, basi I rest my case.

Systematically, nimekuonyesha chanzo kilikuwa ni upungufu wa bidhaa. Ambao ulisababisha watanzania kuuza bidhaa zilizokuwa zinahitaji nchi jirani hili kuleta bidhaa zilizokosekana ndani ya nchi. Kitendo hiki kilileta domino effects.

Pamoja na juhudi za serikali kuwa na vita dhidi uhujumu uchumi. Vita hivyo havikuwa na manufaa kwa sababu vitu vilivyopelekwa nje kimagendo au kihalali havikutosheleza mahitaji yetu kama vingebaki ndani na hii ni fact (period, finito, konec).
 
wandugu,

..kamata-kamata ya wahujumu uchumi ilikwenda sambamba na uanzishaji wa maduka ya kaya.

..maduka ya kaya kazi yake kubwa ilikuwa ni kufanya rationing au kutoa bidhaa kwa mgao. wananchi kwanza walitakiwa wajiandikishe idadi yao ktk kila kaya/familia. mwenyekiti wa shina[nyumba 10] wa CCM alikuwa akihakiki zoezi hilo. baada ya hapo kila familia/kaya ilikuwa inaruhusiwa kununua kiwango maalum cha bidhaa adimu[sukari,unga wa sembe,mafuta ya kupikia] kulingana na idadi ya wanafamilia.

..kama madai ya Mkandara ni ya kweli, kwamba kulikuwa hakuna uhaba wa bidhaa zozote zile, huu msamiati wa BIDHAA ADIMU ulitokea wapi?

..kama uzalishaji viwandani ulikuwa unatosheleza demand basi serikali isingelazimika kuanzisha maduka ya kaya na kuuza bidhaa kiduchu-kiduchu. tena ilifikia wakati serikali ikalazimisha wananchi kununua unga wa mhogo instead ya unga wa mahindi.

..mwaka 1984 baada ya hali kuzidi kuwa mbaya serikali iliamua kufungua milango ya biashara. kwa maneno mengine serikali iliamua kuruhusu wale wenye fedha zao kuingiza bidhaa adimu toka nje kwa ajili ya walaji wa ndani. kama tulikuwa tumejitosheleza kwa uzalishaji wa ndani, kama anavyodai Mkandara, then kwanini serikali ilichukua uamuzi wa kuruhusu bidhaa toka nje?

..kama viwanda vyetu vilikuwa vina uwezo wa kifedha/mitaji na kiuzalishaji basi utoroshaji bidhaa kwenda nje maana yake ni kuongezeka kwa soko na walaji. kwa msingi huo vilipaswa kuongeza uzalishaji. sasa tujiulize kwanini hilo halikutokea.

..kwa lugha rahisi:kwanini viwanda vya Kenya vilishamiri kutokana na soko la Tanzania, lakini viwanda vya Tanzania viliuawa kwa magendo ya bidhaa kwenda Kenya?

..Tatizo letu wa-Tanzania ni kutumbukiza siasa hata mahali ambapo hapana uhusiano na siasa.

NB:

..moja ya kituko cha vita vya wahujumu uchumi ilikuwa kukamatwa kwa mzee wa miaka kama 80 aliyekuwa akiitwa Kengere Mingi. Mzee huyu alikamatwa porini Dodoma, au Morogoro[sina uhakika], akiwa na ngombe na mifugo karibia 5000!!

..serikali ilikamata wananchi na kuwaweka mahabusu bila nafasi ya kupewa dhamana. baadaye ikapeleka mswada wa sheria ya uhujumu uchumi bungeni, na kutumia sheria hiyo kuwashitaki, na kuwatia hatiani, wananchi ambao tayari walikuwa mahabusu. huo ulikuwa ni ukiukwaji mkubwa wa utawala wa sheria na katiba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…