Rev Kishoka:
Hivi leo akitokea mtu na akisema sub-prime mortagage crisis ilikuwa na nia ya kuupindua ubepari, itabidi tumpe masikio?
Over-deregulation ina matatizo yake katika uchumi kama vile tunavyoona sasa hapa US.
Over-regulation nayo ina matatizo yake, kama yale yaliotokea Tanzania au katika nchi za kikomunisti. For God sake, Poland watu walikuwa wanapanga foleni kwa ajili ya mkate, kwanini sisi tufikiri matatizo yetu yalikuwa na external influence sio mapungufu ya siasa zenyewe?
Zakumi,
Katika Security intelligence spectrum, kilichotokoea Marekani ni suala la usalama wa taifa. Kuanguka kwa uchumi ni suala la usalama wa taifa hata kama si lazima apinduliwe mtu.
Jiulize ikiwa ulafi na uroho wa watu unajulikana na unatumika kama chambo na maadui kuangamiza Taifa, kuna shida gani basi kutokea mazingaombwe na hivyo uchumi wa nchi kuanguka?
Ikiwa China, Russia, India, Brazil na EU wanapigania kuwa na sauti kubwa kiuchumi, kisha wakatumia uroho wa Wamarekani na udhaifu wao wa kuwajibika katika kuwa na sheria kali, je si rahisi kuangamiza uchumi kwa kuwa na mipango mibovu ya kiuchumi ambayo huweza kutoa kipigo cha ajabu?
Je umesahau kisa cha Sovieti kuanguka chali pamoja na Ujamaa mbuzi ilikuwa ni mshindano ya silaha yaliyowekwa kama kiini macho na Reagan na kina Brezhnev wakakimbilia kuweka pesa zote kujenga silaha zinazopepea badala ya kujenga uchumi ndani ya nchi?
Uhujumu bwana Zakumi una sura nyingi sana na si siri kuna Wamarekani wanaoanza kuhoji na kujiuliza hivi kama Madevu Osama na ukichaa wake angeamua kuangusha uchumi na si kuua watu ingekuwaje?
Yesm it may be a conspiracy theory, however there are too many key facts that when are tied and woven together, ,they demonstrate a colusion or consipiracy to sabotage economy and country.
Je ni vigumu kuamini kuwa uhujumu uchumi was classic method ya kupindua Serikali kuliko mtutu wa bunduki?
Angalia outcome yake, maduka yakashehena na bidhaa za kuagiza, tukaanza kukopa hovyo na kutumia hovyo, tukashusha thamani ya sarafu, tukaanza mipango kibao ya kurutubisha uchumi kupitia IMF, tukamalizia na kufungua milango kwa wawekezaji.
Sasa tujiulize, miaka 23 baada ya Nyerere kukimbiza ubawa, je tumefaidika vipi kiuchumi na huu mfumo mpya ambao kwangu mimi mjamaa naona kuwa nusu yake ni nguvu za uhujumu uchumi?