Zakumi
JF-Expert Member
- Sep 24, 2008
- 5,063
- 2,478
Wanabodi,
Inabidi niendeleze mjadala huu kwa sababu kutokana na mawazo ya Zakumi nashindwa kabisa kuelewa kwa nini viongozi na wasomi wetu wanashindwa kuelewa hali halisi ya nchi yetu..anajaribu sana kupandikiza mbegu za kulaumu watu na uwezo wa nchi badala ya mfumo..
Nimemsoma sana Zakumi lakini kila mara naona kwamba anatumia sana kitabu badala ya kuangalia watu na mazingira ktk hali halisi kufuatia miaka hiyo..
Imefikia hata kusema kulikuwepo na Tatizo la Umeme mikoa ya Mwanza miaka hiyo jambo ambalo nashindwa hata kumwelewa..Mwanza wala Musoma haikuwa na matatizo ya Umeme wakati wa Nyerere, kwa sababu tulikuwa tukizalisha umeme zaidi ya matumizi yetu na ndio umeme huo huo umetumika hadi miaka ya hivi karibuni pamoja na kupanda kwa population, uwejekeshaji na kadhalika X2..
Amekazania sana kusema vitu vilivyokuwa vikisafirishwa nje vilikuwa havitoshi hata kama vingebakia nchini akiwa hana takwimu za kuonyesha hivyo isipokuwa kutumia nadharia inayoonyesha demand na supply inavyocheza..
Leo hii watu wanaingiza magari toka nchi za nje haina maana huko nje kuna Upungufu wa magari kwa sababu tu kuna Operation ya kukamata watu wanaosfirisha magari nje hasa nchi za kiafrika..Anashindwa kufikiria kiini au sababu hasa ya vita kama hii kuwa inatokana na mfumko wa wizi wa magari haya kuyapeleka nchi za Afrika na haihusiani kabisa na hali ya uzalishaji wa magari nchi hizo.
.
Pia nitarudia kwamba fikra za criminal hata siku moja haziwezi kupimwa na Uchumi kwa sababu huwa wako one step ahead ya somo la kiuchumi..nayo ni kuwepo ktk hali halisi ya watu na mazingira yanayoohusika na uchumi tunaounzungumzia.
Kwa mfano, kabla na wakati wa Uhujumu Uchumi tulikuwa tukichukua Prawns toka Chakula barafu kwa Tsh 600/Ib wakati thamani ya shilingi ilikuwa Tsh.21 kwa Us dola. Sasa Ukitumia hesabu za Kisomi utakuta bei hiyo ilikuwa kubwa ajabu (almost Usd 30/Ib) na unaweza bisha hadi kesho ukaanza kutumia mfumko wa bei kutokana na demand... lakini hata hivyo huko nje prawns hao hao waliuzwa dollar 10 kwa Pound! sasa hawa watu wanauza vipi...mahesabu hayapandi kabisa.
Lakini kwa wabaingazaji walijua bei ya dola Mtaani ni Tsh 175 hivyo inaponunua Apound of Prawns kwa 600 ni sawa na Usd 4 tu.. Soko Harare lilikuwa Zd 10 na chenji ilikuwa 1Zd =1Usd..
Hapa nyumbani bei ya prawns under price control chini ya Tsh. 50/Ib hivyo, mfanya magendo akiingia Chakula barafu tu wajomba wanashangilia wanajua wataingia 600/ib wakati zinazokwenda mfuko wa Chakula barafu ni Tsh 50 /ib..pato la ziada Tsh.550/Ib wanagawana wahusika ndani ya ofisi ya Chakula barafu..Kama kutakuwepo na Upungufu wa prawns mahoteli yetu ya Kitalii, mfanya magendo na Mpokea rushwa hawatazai hilo isipokuwa kiwango cha fedha anazoweza yeye kutengeneza kutokana na sheria ambazo hazikuzingatia hali halisi.
Magendo hayatazami uzalishaji na ugawaji wa prawns Tanzania isipokuwa soko lake nje lipo vipi, Na hatukupeleka Kenya kwa sababu ilikuwa hailipi kama Zimbabwe na South Africa..Hatukutazama kama sisi tunazalisha in excess au less ya demand ya ndani ila tulichofahamu ni biashara haramu..Uharamu wake unakuja kwamba hairuhusiwi kusafirisha prawns nje bila kuwa na kibali pamoja na mlolongo wa regulations kupitia benki kuu..Hivyo hivyo kila siku walanguzi walikuwa wakitafuta masoko nje kutokana na ukweli kwamba mali hizo zilizalishwa nchini..
Chimbuko la Magendo nchini lilitokana na siasa ya Ujamaa ktk Biashara..Vitu kama price control, Export regulations na kadhalika ndivyo vilichangia sana watu kuanza kupitia mlango wa nyuma kinyume cha sheria kwa sababu soko lilikuwepo nje lakini sheria hazikuruhusu watu kufanya biashara hizo free kwani viwanda vilivyokuwa mali ya serikali na mali iliyozalishwa ilikuwa kwa malengo ya huduma za ndani nchini na kama Export basi serikali ndiyo ilihusika pia kwa sababu nyinge ya kisiasa kuwa unafanya biashara na nchi yenye kukubaliana na mrengo ama utawala uliopo. Politics ndizo zilikuwa zikiendesha Uchumi wa nchi badala ya Uchumi kuendesha Politics..
Haya mambo menngine mtasema weeee... lakini ukweli upo on the ground..
1 Magendo - ni ku supply vitu kinyume cha sheria.
2. Rushwa - ni kutoa/kupokea malipo ya ziada ktk huduma..
3. Uhujumu Uchumi - ni pamoja na crimes zote zinazohusiana na Uchumi wa nchi iwe moja kwa moja au kwa kupitia (indirectly)..
Mkandara:
Kabla ya kukujibu suala la umeme ningependa kukushukuru kwa kusema ujamaa ndio uliosababisha. Kwa sababu bila ujamaa tusingekuwa na viwanda vya kiserikali na serikali isingekuwa na sababu ya ku-control price. Na hizo hoteli za kitalii ingebidi ziwe zina compete na wanaopeleka prawns Zimbabwe. Na kwa mashindano hayo mvuvi atanogewa na mapato na kuongeza productivity yake itakayofanya bei kujisahihisha yenyewe.
Hili suala la umeme hata ndugu Mwanakijiji alinibishia lakini sikutaka kwenda mbele, lakini ngoja nijaribu ku-prove point yangu once again.
Kama nitakuwa sikosehi Mutex ilifunguliwa 1981. Wakati kinafunguliwa kiwanda hiki, mji wa Musoma ulikuwa unatumia umeme ulizalishwa kwa kinu cha diesel ambacho kilikuwa hakitoshelezai mahitaji ya mji au kiwanda.
Na vilevile Mwanza ilikuwa nayo inategemea kinu cha diesel kuzalisha umeme. Hivyo uzalishaji wa Mwatex nao ulikuwa unaathirika sana na kukosekana kwa umeme wa uhakika.
Umeme wa uhakika ni ule uliokuwa kwenye gridi la taifa ambavyo vinu vyake ni vya maji. Lakini umeme huu ulifika mikoa ya Mwanza na Mara mwishoni mwa 80s au Mwanzoni mwa 90s.
Hivyo umeme wa uhakika ulifika Musoma mjini miaka kumi baada ya kiwanda cha Mutex kufunguliwa rasmi.
Ninaweza kukubaliana na wewe kuwa kwa miaka hile. Umeme uliozalishwa ulikuwa wa kutosha. Lakini ni lazima ukumbuke kuwa umeme hausafirishi wirelessly. Ni lazima kuwepo na miundo mbinu ya wire za kusafirisha umeme. Kwa bahati mbaya mikoa ya kanda ya ziwa ilichelewa kupata. Hivyo hivyo kila mji ulikuwa na magenerators yake.
Na nikirudi kwenye swali la Mwanakijiji alilouliza tofauti kati ya 3MW za kinu cha diesel na 3MW za kinu cha maji, tofauti hipo na tena kubwa sana.
Katika matumizi ya energy wataalamu hawapo interested sana na output ya kinu. Na kama wangekuwa basi 3MW ya kinu chochote isingekuwa na tofauti sana.
Umeme kama energy unapatikana kwa kubadilisha energy iliyokuwemo kwenye vyanzo kama vile maporomoko ya maji, mafuta ya kuendeshea magenerator, mionzi ya juu n.k. Hivyo uwiano wa gharama za vyanzo(input energy) na thamani ya umeme unaozalishwa (output energy) ni lazima uwe wa kueleweka kiufundi na kibiashara.
Na kama uwiano sio kitu cha muhimu basi kulikuwa hakuna gharama za kujenga gridi za umeme. Kila mji ungekuwa na generator za kuzungushwa na punda au ng'ombe.
Kutokana na shida ya mafuta iliyokuwepo na uwiano mbaya wa kuzalisha umeme kwa kutumia magenerator ya diesel. Viwanda vya Mwanza, Musoma na miji mingi iliyokuwa na shida za umeme ilikuwa kutimiza majukumu ya kisiasa lakini sio ya kiuchumi au kibiashara.
Unashindwa kunielewa kuwa Mwanza na Musoma zilikuwa na matatizo ya umeme kwa sababu unashindwa kuelewa kuwa matumizi ya nyumbani ni madogo sana kuliko matumizi ya viwanda. Kumbuka katika miaka ya 80s, 90s sehemu kubwa ya umeme wa majumbani ilikuwa ni kwenye taa, radio na kupiga pasi.
Hivyo generators zilikuwepo kule Nyakato zilikuwa zinaweza kutosheleza matumizi ya majumbani bila matatizo. Lakini kwenye uendeshaji wa mashine, gharama ni kubwa. Na wakati huohuo nchi ilikuwa kwenye mgao wa mafuta.
Najua bado utabisha tu. Tuachane na viwanda vya Musoma. Kuna kiwanda vya Polyster Morogoro. Mategemeo ya kiwanda hiki yalikuwa kiwe kikubwa kuliko viwanda vyote vya nguo Afrika Mshariki na ya kati. Pamoja na kuwa Morogoro ina umeme wa kutosha na sehemu nzuri kiusafirishaji, kiwanda hiki na vinginge vilivyokuwepo Morogoro vilichemsha BIG TIME.
Najua utaendelea kubisha. Kwa sababu utaendelea kutafuta external factors tu za kushindwa kwetu. Lakini sehemu kubwa ya kushindwa mambo mengi ni kwa sababu tunacheza bahati nasibu.
Vilevile kutokana na mazungumzo yako. Inaonyesha kuwa umefanikiwa kimaisha. Mafanikio ya mradi unaoendeshwa na mtu mmoja unaweza kuwa na mafanikio makubwa. Lakini mbinu zinazotumika kuleta mafanikio ya mradi huo, zinakuwa na mafanikio machache sana kwenye miradi iliyo complex na yenye kuhitaji manpower ya watu wengi.
Unasema kuwa najaribu sana kutumia kitabu. Nafanya hivyo kuondoa myths.
Kama uzalishaji kwa kutumia njia za kiserikali ungekuwa na mafanikio makubwa, basi nchi ya kwanza kufanya hivyo ingekuwa Marekani.
Moja ya tofauti kubwa ya serkali za karne ya 20 na zile zilizopita, ni juhudi za serikali nyingi hata zile za kibepari kuendesha miradi katika massive ambayo haijawahi kutokea duniani.
Nakutaka Mkandara kwa dakika moja tu fikiria complexity ya miradi ya kumpleka mtu mwezini na kurudi dunia salama. complexity ya ku-manage miradi hii ina tabia zinazofanana na complexity ya ku-manage uzalishaji wa bidhaa za watu kutumia majumbani nchi Tanzania.
Hivyo suala lenye kuonyesha uzaifu katika poor management sioni sababu ya kulitafutia sababu za kulaumu watu wengine kwa sababu price control is manageable na man-made.
Kwa maoni yangu gharama za kuwafunga wafanyabiashara na kuwaita wahujumu uchumi zilikuwa kubwa kuliko ya kuendeleza vitu kuwa bei rahisi kwa sababu tu ujamaa unataka hivyo.