Zakumi
JF-Expert Member
- Sep 24, 2008
- 5,063
- 2,478
Kwa hiyo, ukweli ni kwamba hawa watu walikuwepo!..
Mkandara acha Cherry picking na selective Nostalgia.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa hiyo, ukweli ni kwamba hawa watu walikuwepo!..
Naona Jokakuu kafanya kazi tayari lakini ngoja nikupe link.
http://www.worldbank.org/aid/africa/tanzania2.pdf
Heheheheheee...hivi mwaka '83 na '84 raisi alikuwa nani vile?..Lol
alikuwa Julius Kambarage Nyerere.
Joseph Warioba said:"Mwaka 1985 hatukuwa na akiba ya fedha za kigeni. Tulikuwa tunashindwa hata kulipia meli moja ya mafuta. Sasa kama akiba yetu ikipungua, bei ya mafuta imepanda, bei ya vyakula imepanda, tukajikuta hatuna akiba ya fedha za kigeni, tunafanyaje? "
Zakumi,
..nimewahi ku-post ripoti ya kina Prof.Wangwe ktk thread nyingine. sasa inaelekea kuna wenzetu hawakuitilia maanani. lakini Prof.Wangwe ni kati ya wachumi wanaoheshimika Tanzania.
..Waziri Mkuu Warioba alipata kuielezea hali ya kifedha ya serikali wakati Mwalimu anaondoka madarakani. maneno yake ni haya hapa:
..Mwanakijiji anajaribu kutubana kwasababu ktk kuielezea hali ya kifedha ya serikali wakati ule mimi na wewe tulisema "hazina ilikuwa tupu."
..sasa anachotaka tumuonyeshe makabrasha ya Hazina na Benki Kuu yakionyesha balance ya Tsh 0.00.
..ukiona Mwanakijiji ana-argue on trivial things and semantics ujue hoja imemshinda.
Zakumi,
Hapana mkuu unajua mnashindwa kabisa kuelewa kwa nini nazungumza yote haya..Hakuna jambo lolote aliloandika Jokakuu au wewe ambalo nalipinga isipokuwa mnachofanya ni exactly ninavyofikiria.. Kwamba mnatumia vitabu na siasa kujaribu kusolve problem iliyokuwa complex na kubwa kuliko vitabu na siasa...
Ni sawa na tatizo ambalo nchi za magharibi wana face today hakuna jibu rahisi kabisa ila itakuja kuwa rahisi baada ya matukio I mean when it's too late ndipo utasikia kila aina ya mapendekezo.. Inge.. Tunge, Ange yaani hizo angefanya hivi ama vile hazina hata hesabu.
Labda nikupeni mfano mdogo sana..unaolingana na sisi wenyewe tuache kutazama nchi nzima.. mathlan ktk bajeti ya matumizi yako huwa unategemea kipato chako na cha mkeo kuweza kuendesha familia na kwa bahati mbaya/nzuri (?) nyote ni wafanyakazi, meaning mnaishi maisha yasiyokuwa ya biashara..mshahara kwa kutoa huduma kwa familia (Ujamaa). Bahati mbaya mkeo anakosa kazi kutokana na matatizo ambayo iadha kwa kujitakia ama yalikuwa hayawezi kuepukwa(vita, Ukame, mafuta, uchumi wa dunia kuporomoka)..sasa pato limepungua kiasi kwamba hata uwezo wa chakula ndani ya nyumba ni mdogo..
Yes inatakiwa zifanyike mbinu za kutafuta pato zaidi kwa sababu hata wewe mwenyewe upo njia panda.. hujui lini kazi utasimamishwa..Hivyo kwa sababu hakuna kazi huko nje inabidi mkeo labda afikirie kuanza kimradi ka kufungua biashara hata kama iwe kimgahawa cha kupika vitumbua. (wakati wa Mwinyi). Lakini before all that unakuja gundua kwamba mbali na chakula kupungua ndani ya nyumba..Kuna mapaka shume na nguchilo ambao ambao huja kula akiba ya chakula chenu..
Now, alichofanya Sokoine na Nyerere ni kuhakikisha kwanza chakula cha ndani hakiibiwi tena na hao nguchilo pamoja na kwamba hali ya uchumi bado iko palepale yaani Mbaya!..Yes, kwa mtu ambaye hatazami mbali ataona ni kupoteza muda kupambana na mapaka shume na nguchilo wakati ukweli ni kwamba pato la nyumba kwa kutegemea kazi moja haliwezi kutosheweleza, muhimu ni mara moja kwa mke kuanza hiyo biashara ya vitumbua kuongeza pato na pengine kuondoa tatizo la chakula ndani ya nyumba...Huu ndio mtazamo wa Jokakuu ambao unapinga ku deal na nguchilo ikiwa ndani ya nyumba huna hata chakula cha kutosha...Kashindwa kufahamu kwamba hata hivyo vitumbua haviwezi kuuzika ikiwa hakuna wanunuzi. Vitu tulivyokuwa tukizalisha Tanzania vilikuwa havina soko tena nje kama miaka ya 70s. Ukosekana ji wa foreign money sio sababu kwani lini nchi za kiafrika kweli zimeweza kujimudu kwa foreign reserve zaidi ya mikopo ya nje kutumika tukilipia interest bila kulipia Principal na kudai kuwa tuna akiba, tukitegemea kusamehewa madeni. Hatuwezi ku balance payments zetu bila kuagiza mali nje zaidi ya uwezo wetu ku export!...kwa hiyo badala ya balance itokane na exports inatokana na Imports (through grants) kubwa kukidhi mahitaji yetu hivyo kukuza zaidi deni la nje...Hii ndio true picture ya nchi za kiafrika, kwa hiyo ziku zote sisi ni wadeni tu hatuwezi kudai mafanikio ya kiuchumi bila kukopa, kulaza malipo na kudanganya wananchi kwa kutumia mahesabu ya uongo yasiyojali wala kuzingatia kushuka kwa thamani ya shilingi..
Na mimi nasema na kuunga mkono hatua za mwalimu na Sokoine.. Ulikuwepo umuhimu wa ku- deal na nguchilo kwa sababu kwa kila vitumbua Kitakachopikwa ni kuwaongezea idadi ya Ulaji hao nguchilo ambao kama walikuwa wachache wakisha sikia harufu ya vitumbua watakuja jazana zaidi na kuigeuza nyumba yako jalala...(Yaliyofuata wakati wa Mwinyi)... According to Shevji.
Ndicho alichokiona Mwalimu na Sokoine kabla, pamoja na kwamba walifahamu kuwa kiuchumi Tanzania imefikia mahala ambapo inatubidi tuanze kupika vitumbua (Kuingia Ubepari)...Lakini kabla hatujafanya hivyo ni muhimu kuhakikisha kwamba hatuna hao mapaka shume na nguchilo ambao hakuna mtu anaweza kusema kwa uhakika uwezo wao wa kula mazao yetu..tuzibe ufa laa sivyo tutajenga nyumba ndio yalikuwa maneno ya mwalimu..
Sasa ikitazama mawazo ya wachumi wetu wote waliotangulia, wote wame avoid tatizo sugu la nguchilo.. wameshindwa kuitazama Tanzania kwa mazingira na watu wake wakifikiria kwamba kinachowezekana Ulaya na vitabuni kinawezekana Afrika..Wakati wa Ukame huwezi kupoteza muda endelea kufikiria jinsi ya kupata maji wakati una pakacha linalovuja.. Yes, ni muhimu sana kufahamu kwa nini maji yamekosekana na sababu zipi zilizotangulia hadi kufikia maji yakawa adimu na kisha kufikiria mbinu mpya za kuzalisha maji na kuyahifadhi..
Hizi ni strategies tu ambazo huwezi kuziweka ktk practical unless unaisha gundua yote yaliyotangulia na kama kutakuwepo na sababu ya maji hayo kuibiwa kabla hayajawafikia wananchi basi ni muhimu sana kuvuta wizi huo kwanza. Kwani pakacha linalovuja siku zote ni muhali na hata ukitumia nguvu za namna gani huwezi kupata malipo sawa ya nguvu zako kutokana na pakacha lenye tobo. Kila unapozidisha ujazo wa maji ndivyo tobo zinavyozidi kupanuka na kupoteza maji mengi zaidi.. It goes on and on..
Mkuu wangu sasa hivi tupo ktk matokeo ya kuogopa ama kuwaacha nguchilo, matokeo yake limekuwa tatizo sugu la chumi za nchi zote za kiafrika kwa sababu tunafikiria kuwa maadam nguchiro ni mnyama pori au nje ya nyumba ( corruption = a foreign culture) haiwezi kutudhuru ndani.. Na kibaya zaidi ni kuiga vitabu ama siasa za nje kwa visingizio kuwa mbona Wazungu wanafuga Paka na nguchilo na haiwasumbui kiuchumi iweje sisi tusiowafuga ndani iweze kutudhuru..
Mimi nasema hivi, wazungu kufuga paka na nguchilo ni ktk mila zinazojenga mazingira yao tofauti kabisa na sisi, wao wanafuga wanyama hawa kama pet, na hawa paka na nguchilo wana special food ambayo inahesabika toka mifukoni mwao..Ni swala ambalo wanaweza kuli control na wakalifanyia budget ndivyo wenzetu nchi za Ulaya wanavyo deal la Corruption. Corruption zao ni mali ya ndani inayozunguka na kurudi ndani ktk benki zao, aghalab hutokea matukio kama ya hujuma kama hizi tulizoziona sasa hivi..
Kwa sisi waafrika na wajamaa tunawaambia kwamba Paka ni paka tunguchilo ni nguchilo tu siku zote hata umfuge vipi ipo siku atarudi ktk unyama wake na kuanza kufanya madudu ya kinyama.. ndio tulioyaona ktk Mortgage, Mashirika ya magari, stock market, financial institution hawa wote ni mapaka yaliyokuwa yamefungwa yakilishwa na ku behave tofauti na mapaka wetu..Mwisho wa yote haya tunaona wenzetu waliwaita hao mafisadi wao kujibu mashtaka na imefikia hadi viongozi wao sasa hivi kuwa questioned, hata kabla Obama hajashika kiti cha Ikulu na regulations zinawekwa kinyume cha utaratibu wao wa zamani. na ukitazama mpango wa Obama ktk kuinua hali ya uchumi Marekani sheria nyingi za kijamaa zimeingizwa.. hakuna tena mchezo wa responsibility without Accountability! na kazi ya kuwafichua mafisadi sio kazi ya Obama wenzetu wana vyombo madhubuti vinavyofanya kazi hiyo tu.. Kwa nchi kama Tanzania na nchi za kiafrika kwa ujumla rais ndiye Alpha na Omega....The buck stops there!.. Akisema Hosea au said Mwema watu wanawaona vichaa tu hadi tumsikie Kikwete ama Pinda waki sisitiza...
Kutokana na RUKSA ya Mwinyi mkuu wangu ndio maana hadi leo bado tuna mapaka shume na nguchilo hadi leo...Haya yote ni kutokana na uwezo wangu kusoma alama na kujua kwa uhakika tulikotoka na tunakokwenda kwa kuzingatia watu na mazingira.. Sisi ni wasafiri tunaokwenda na baiskeli hivyo ni muhimu tufikiria uwezo wa baiskeli, vizingiti vinavyoweza kutuzuia tukiwa na baiskeli yetu badala ya kuchukua ya wazungu ambao wao wanaruka na ndege!..Wao wana hakika ya usafiri wa haraka lakini wakija anguka watakufa wote na sisi na unyonge wetu, nguvu ya miguu itatufikisha pale tulipokusudia kufika na baiskeli.. hatuwezi kushindana nao wazungu na wala kuwaiga hadi hapo tutakapo weza kumudu ndege kama chombo cha Usafiri..
..Mwanakijiji anajaribu kutubana kwasababu ktk kuielezea hali ya kifedha ya serikali wakati ule mimi na wewe tulisema "hazina ilikuwa tupu."
..sasa anachotaka tumuonyeshe makabrasha ya Hazina na Benki Kuu yakionyesha balance ya Tsh 0.00.
..ukiona Mwanakijiji ana-argue on trivial things and semantics ujue hoja imemshinda.
JokaKuu... ninatumia maneno vizuri sana na sipendi kusema kitu ambacho simaanishi. Wewe na Zakumi mlisema "hazina ilikuwa tupu". Hiyo ni kauli inayodai ukweli (it is a definitive statement).
katika kauli hiyo hakuna utata wala qualification yoyote ile. Mtu akiisoma na hana uwezo wa kuihoji ataamini kuwa mwaka 1983/84 Tanzania haikuwa na kitu.
Katika kuthibitisha ukweli wa kauli yenu mmetumia mfano "tulishindwa kugomboa hata meli moja". Kwa kutumia mfano huo mnajaribu kuithibitisha kuwa kauli yenu ilikuwa na ukweli (kwamba hazina ilikuwa tupu ndiyo maana tulishindwa kugomboa meli moja).
katika ushahidi mliouleta wenyewe taarifa ya kina Wangwe haikusema Hazina ilikuwa tupu!
Sasa kama kauli yenu ilitegemea ripoti ya kina Wangwe na ripoti mmeiweka wenyewe inaonesha kuwa haikusema hivyo kwa mtu mwenye fikra huru anaweza kuona kuwa kauli yenu siyo was factually wrong but was put out purposeful to mislead the public.
Sasa kwako hilo linaweza kuwa trivial kwangu siyo ni kubwa mno.
Lakini zaidi ni Zakumi aliyesema kuwa "namba zipo" na hilo pia ni kauli inayodai ukweli na nilipomuomba aweke hizo namba ameleta ripoti ya Wangwe ambayo ndani yake hakuna mahali panapoonesha "namba" kuwa Hazina ilikuwa tupu!
Now, you tell me if my deduction is inherently wrong or it is you and Zakumi who for reasons known to you and you alone mlijaribu kueneza kitu kisicho ukweli mkiamini hakuna mtu mwenye uwezo wa kuhoji kauli. Wrong u were.
So, kwa faida ya mjadala mzurii naomba mbadilishe kauli yenu kuhusu Hazina kuwa tupu wakati ule 1983/84 ili tuwe katika uwanja mmoja wa mjadala. Vinginevyo nawauliza nyie swali; Je mwaka 1983/84 hazina ya Tanzania ilikuwa tupu?
Mwanakijiji said:JokaKuu... ninatumia maneno vizuri sana na sipendi kusema kitu ambacho simaanishi. Wewe na Zakumi mlisema "hazina ilikuwa tupu". Hiyo ni kauli inayodai ukweli (it is a definitive statement).
katika kauli hiyo hakuna utata wala qualification yoyote ile. Mtu akiisoma na hana uwezo wa kuihoji ataamini kuwa mwaka 1983/84 Tanzania haikuwa na kitu.
Katika kuthibitisha ukweli wa kauli yenu mmetumia mfano "tulishindwa kugomboa hata meli moja". Kwa kutumia mfano huo mnajaribu kuithibitisha kuwa kauli yenu ilikuwa na ukweli (kwamba hazina ilikuwa tupu ndiyo maana tulishindwa kugomboa meli moja).
katika ushahidi mliouleta wenyewe taarifa ya kina Wangwe haikusema Hazina ilikuwa tupu!
Sasa kama kauli yenu ilitegemea ripoti ya kina Wangwe na ripoti mmeiweka wenyewe inaonesha kuwa haikusema hivyo kwa mtu mwenye fikra huru anaweza kuona kuwa kauli yenu siyo was factually wrong but was put out purposeful to mislead the public.
Sasa kwako hilo linaweza kuwa trivial kwangu siyo ni kubwa mno.
Lakini zaidi ni Zakumi aliyesema kuwa "namba zipo" na hilo pia ni kauli inayodai ukweli na nilipomuomba aweke hizo namba ameleta ripoti ya Wangwe ambayo ndani yake hakuna mahali panapoonesha "namba" kuwa Hazina ilikuwa tupu!
Now, you tell me if my deduction is inherently wrong or it is you and Zakumi who for reasons known to you and you alone mlijaribu kueneza kitu kisicho ukweli mkiamini hakuna mtu mwenye uwezo wa kuhoji kauli. Wrong u were.
So, kwa faida ya mjadala mzurii naomba mbadilishe kauli yenu kuhusu Hazina kuwa tupu wakati ule 1983/84 ili tuwe katika uwanja mmoja wa mjadala. Vinginevyo nawauliza nyie swali; Je mwaka 1983/84 hazina ya Tanzania ilikuwa tupu?
Mwanakijiji,
..haya basi Hazina yetu ilikuwa imefurika mapesa.
..sasa naomba tujadili taarifa ya WATAALAMU WA UCHUMI, Prof.Wangwe na wenzake.
Mwaka 83/84 hazina ilikuwa na shi'ngapi?
Mwanakijiji,
Mkuu wala usisumbue kichwa chako. hawa jamaa watunzi wakumbwa wa ngonjela..Umesikia hayo ya kukomboa meli moja!...wakati sisi wenyewe tulikuwa na meli zetu waajiriwa ni kina FMES ambaye anaweza kuthibitisha hapa kuwa miaka hiyo meli zetu zilikuwa zikienda hadi Singapore..
Kisha basi kabla sijasahau.. hadi mwaka 1983, ndege zetu za ATC zilikuwa zikienda Dubai, London, Comoro, Zimbabwe, Bujumbula, Malawi, Zambia just to name few kisha wanasema hatukuwa na hela hata za kununu mafuta..Haya leo tuna fedha hazina ndege zetu zinakwenda wapi kama hata sio kufungiwa hata kuruka..
Nimemaliza kuzungumza na mshjikaji wangu Othman Matata kama unamfahamu, kanambia TRC ilikuwa ikifanya kazi vizuri tu wakati wa mwalimu pamoja na kwamba huduma zilikuwa na mapungufu ya standard sio nzuri.. lakini Railway ilikuwa ikifanya kazi..
Hata siku moja miji yote Tanzania iliyokuwa na umeme haikukatika umeme pamoja na shida zote za kufunga mikanda... lakini tumekuja shuhudia Umeme wa mgao wakati wa Mwinyi na Mkapa...
Mkuu Zakumi kashindwa hata kunielewa zaidi ya kufikiria kwamba napinga utumiaji wa vitabu, wakati nazungumzia issue moja ambayo haiwezi kuwa solved na uchumi wenyewe kwa sababu hakuna kitabu hata kimoja cha uchumi kinazungumzia njia za kupambana na Magendo, rushwa na hujuma zote za kiuchumi zisizozingatia regulations...
Kasoma mawazo ya Profesa Chevji bado anatafuta pa kutokea..yeye mwenyewe kachukua visehemu na kudai tusimtazame Mwinyi..
Mkuu wangu Binafsi naamini kabisa kwamba Uhujumu uchumi ulikuwa lazima na bado ni lazima hadi kesho...unless Ndivyo tulivyo - Umaskini wa hali na mali ni moja ya culture ya mwafrika..