Zakumi
JF-Expert Member
- Sep 24, 2008
- 5,063
- 2,478
Wanabodi,
Sasa naona tunapoteza mwelekeo.. Kama alivyosema Nyani Ngabu hakuna mtu anayesema Tanzania mwaka 1984 ilikuwa katika hali nzuri kiuchumi kuliko leo hii ama Mwalimu hakuweza kukuza mfuko wetu.. laa hasha swala hapa ni mada yenyewe yenye kichwa - Nini chimbuko la vita ya Wahujumu Uchumi!... Na mimi nimeelezea vitu ambavyo vinaonyesha kwamba sisi wananchi na sio viongozi ndio sababu na kulikuwepo na kila haja ya vita vile pamoja na kwamba hatukuweza kufanikiwa hadi mwisho kutokana na Mwinyi kuachana na vita vile..
Sasa tatizo langu kubwa ktk mada hii ni swala la kulaumu na kunyoosha vidole kumsuta mwalimu na Sokoine kuwa ndio sababu na kwamba hapakuwepo na haja ya kufanya hivyo..
It's exactly lawama tunazowashusia wazungu wakoloni ktk kushindwa kwetu kujiendeleza kuwa mkoloni alitufanya hivi ama vile na itasikitisha zaidi ikiwa leo hii tupo huru tunashindwa bado kufanya kitu cha maana tunarudi nyuma kusema sababu ni mkoloni..
Nakumnbukwa mwalimu Nyerere alitumia Mkoloni kama kigezo cha kutuamsha sisi tufanye nini.. Umuhimu wa sisi kujitawala na akaweka mikakati ambayo inapambana na utawala dhalimu wa kikoloni... hivyo hakutumia kabisa mkoloni kuwa sababu ya Tanzania kushindwa kujiendeleza isipokuwa alitumia Mkoloni kuelezea Ugumu wa kasi ya maendeleo yetu..Kwa hiyo mwalimu alioanza kila kitu from the scratch, tuliunda mashirika karibu yote tokea kuweka msingi wake tofauti na nchi nyinginezo kwa sababu mwalimu alizingatia tofauti zilizopo kati yetu na nchi kama Kenya...Mwalimu alitujengea nyumba akaturithisha hata kama kulikuwa hakuna fedha benki lakinii Assets zilikuwepo, miundombinu ilikuwepo ya kulingana na mwanzo wa nchi kujitawala...hiyo pekee ni urithi mkubwa sana..
Yes, Mwalimu alishindwa na sababu inajulikana kwamba hakutaka kupangisha nyumba yetu..Na sote tunafahamu kwamba ni pamoja na Utaifishaji wa mashirika na biashara binafsi zilichangia kushuka kwa uchumi wetu kwa sababu kilichotakiwa tu kuwa mikononi mwa serikali ilikuwa commanding heights which includes all Miundombinu..
He failed economically because of UJAMAA as an economic gateaway! -
Leo hii Tanzania pamoja na maendeleo yote tunayojigamba nayo tumerudi nyuma ktk rank za dunia wakati nchi jirani zetu wote wamepanda.. Tanzania ya Nyerere was ranked nadhani 120 ktk nchi maskini leo hii tunashika mkia sijui wa 147 ikiwa na maana tunazidi kuporomoka wakati wenzetu wanaendelea..Na ajabu ni kwamba tunatumia makuzi ya kimwili kuonyesha maendeleo yetu.. Kila mji duniani una maghorofa siku hizi kila nchi ina vitu toka nje kila nchi ina magari kama yetu lakini hali ya wananchi wake ndio kielelezo safi cha maendeleo..Mtoto aliyezaliwa Tandale uwanja wa fisi mwaka 1961 inawezekana kabisa hakuwahi kuvaa nepi.. akila uji wa ulezi au kande na kadhalika lakini baada ya umri wake kukua iweje tutegemee mtu huyu ataendelea kutembea Uchi.... Kuvaa kwake suruali ya mtumba na T.shirt ya msaada ni moja ya mabadiliko ktk makuzi yake siwezi kuita kuwa ni maendeleo as such..atakula Ugali badala ya Uji na kadhalika ni mabadiliko ya makuzi haya sio maendeleo yake hata kidogo.
Kinachoninda mimi ni pale mnapochukua kuvaa kwa Tanzania suruali ya mtumba mnaita ni maendeleo kwa sababu tu tulipata Uhuru tulikuwa uchi hatukuvaa nguo.. na hakuna mtu kati yenu anayetazama hali ya mtu huyu na mazingira yake kama yamebadilika pia..Kwanza suruali ya mtumba ni Umaskini, T. shirt ya msaada ni Umaskini maisha yake bado ni yale yale ya kuomba msaada...
Binafsi naamini maendeleo ya mtoto huyo Tanzania yatapimwa ktk makuzi yake iwe elimu, afya, malazi yake, Pato (ajira) na ikiwa familia yake imetoka katika umaskini..Mwkaa 1961 mtu akiwa na pato la millioni moja kwa mwaka aliitwa tajiri dunia nzima - as A millionaire..hesabu hizo hazipo tena leo utaonekana mtu wa kawaida tu mwenye fedha ya Usalama..
Wakuu zangu, tutazunguka weee kuzungumzia mifano ya nchi nyinginezo bila hata aibu kwani wao ni watu na Mazingira tofauti..swala kubwa hapa ni Uhujumu Uchumi ambao tulishindwa kuupiga vita hadi mwisho miaka ile.. Leo hii ni tatizo tata na isijekuwa kuna watu hapa wanafikiri hata Kikwete anapoteza Muda kwa sababu wanataka kuona Ubepari at it's best!.
Mkandara:
Wewe unayezunguka bro. Wengi tunakiangalia kile kipindi cha 1979-1984.
Na wengi hapa sio wajamaa au mabepari. Na kama tungeweza kutoka katika matatizo 1979-1984 bila kolombwezo za IMF, WB na masharti ya wahisani, basi Tanzania ingekuwa nchi yenye kujitegemea.