Nini dawa ya kutokwa damu puani kunakoambatana na maumivu makali ya kichwa?

Nini dawa ya kutokwa damu puani kunakoambatana na maumivu makali ya kichwa?

Shareef Conscious

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2016
Posts
522
Reaction score
343
Salama jamani?

Kuna ndugu yangu ana tatizo la kutokwa damu puani na hali hii huambatana na maumivu ya kichwa. Hivyo naomba kama kuna yeyote anayefahamu dawa ya hali hii asisite kunijuza/kutujuza hapa(Na kwa faida ya wengine pia)

Iwe ni dawa ya kienyeji ama ya hospitali tutashukuru

Akhsanteni
 
Mie najua dawa ya kienyeji.
Ila kabla sijakushauri dawa naomba nikuulize uko mjini au kijijini? maana kama uko katikati ya mji mfano hap Dar huwezi kupata hiyo dawa
 
Salama jamani!!Hku kwema kiasi,kuna ndugu yangu ana tatizo la kutokwa damu puani,na hali hii huambatana na maumivu ya kichwa,kwa hivyo naomba kama kuna yyte anayefahamu Dawa ya hali hii asisite kunijuza/kutujuza hapa(Na kwa faida ya wengine pia),.Iwe ni Dawa ya kienyeji ama ya hospitali
Akhsanteni
 
Niko mwanza mkuu
Mwanza mjini au nje ya mji?
Enewei, dawa yenyewe, umeshawahi kuona magogo ya miti yaliyoanguka au hata kama limesimama, kuna vitu kama vile uyoga unakuwa umeganda kwenye hiyo miti au magogo, chukua kipande chake, choma, halafu anuse.
 
kuna dawa inaitwa ephedrine
inakuwa ya kupuliza. Hii hubana mishipa ya damu na kuzuia uvujaji wa damu. Ila ni muhimu kucheki masuala kama pressure kabla ya kutumia. Sorry hii ni kwaajili ya pua kuziba.
 
Inapoanza kumtoka aweke barafu kwenye paji la uso huwa inakata,nilikuwa Napata sana hii shida wakati nilipokuwa maeneo flani Kigoma,nakumbuka walikuwa wanasema inasababishwa na hali ya hewa,sasa sijui ki sayansi inasababishwa na nini..?
 
Mwanza mjini au nje ya mji?
Enewei, dawa yenyewe, umeshawahi kuona magogo ya miti yaliyoanguka au hata kama limesimama, kuna vitu kama vile uyoga unakuwa umeganda kwenye hiyo miti au magogo, chukua kipande chake, choma, halafu anuse.
Mjini,ila hii kazi naweza ifanya mkuu,ule uyoga huwa unakua mbichi lkn,so unauacha kwanza ukauke kisha ndio uuchome ama unauchoma ht ukiwa ktk ubichi wake mkuu?
 
Mjini,ila hii kazi naweza ifanya mkuu,ule uyoga huwa unakua mbichi lkn,so unauacha kwanza ukauke kisha ndio uuchome ama unauchoma ht ukiwa ktk ubichi wake mkuu?
Umeelewa lakini? sio uyoga kabisa kabisa! ni yale yanotokezea kwenye magogo kama vile uyoga uyoga. Halafu kama uko Mwanza jaribu kutoka nje ya mji utapata.
 
Inapoanza kumtoka aweke barafu kwenye paji la uso huwa inakata,nilikuwa Napata sana hii shida wakati nilipokuwa maeneo flani Kigoma,nakumbuka walikuwa wanasema inasababishwa na hali ya hewa,sasa sijui ki sayansi inasababishwa na nini..?
Shukrani
 
Umeelewa lakini? sio uyoga kabisa kabisa! ni yale yanotokezea kwenye magogo kama vile uyoga uyoga. Halafu kama uko Mwanza jaribu kutoka nje ya mji utapata.
Nimeelewa vyema kbs,unatumia kwa muda gani,na unavuta mara ngapi mkuu?
 
Back
Top Bottom