Baba jayaron
JF-Expert Member
- Jun 29, 2015
- 4,689
- 6,484
Hizo Asas huwa zinasaidia sana kuwafanya wananchi kuelewa haki zao za kikatiba pale nchi husika zikiwa zina heshimu katiba za nchi zao.Habari wana JF
Kama kichwa kinafyojieleza hapo juu.
Hii mikataba mbalimbali ya kimataifa ambayo serikali husaini kwa ajili ya ushirikiano wa kimataifa na upatikanaji wa fedha za maendeleo kwa namna mbalimbali ni namna gani huleta faida/msaada endapo serikali itaamua kwa makusudi ya maslai yake (kikundi) kukiuka makubaliano hayo ?
Asasi za kiraia/ haki za binadamu tumeona zikiwa mstari wa mbele kutoa matamko yasiyokua na meno kwa serikali isiyosikia wala kujali na zaidi kuwatisha hata hao wasemaji ama viongozi wa asasi hizo.
Endapo matamko yao au kukiukwa kwa makubaliano hayo hayatomzuia/zuia serikali kukandamiza ama kuvunja haki za binadamu, demokrasia na utawala bora ni hatua gani zinawezatumika kuzibiti serikali ya namna hio?
Au tuzikatae Asasi za namna hio?
Au tujitoe kweny mikataba ya namna hio?
Maana tazama nchi kama uganda ambayo miaka karibu 30 wanahangaika na changamoto hizi hizi?
Inaonesha kabisa Asasi hizo na hio mikataba ni kwa nchi zenye ustaarabu lakini si za afrika.
Natanfuliza shukrani
Kwa hivyo tatizo ni katiba?Hizo Asad huwa zinasaidia sana kuwafanya wananchi kuelewa haki zao za kikatiba pale nchi husika zikiwa zina heshimu katiba za nchi zao.
Lkn hapa kweli jaziba nafasi hiyo maana katiba yetu haitoi nafasi hiyo
Sasa mabwana zetu nao wanaweza kutufanya nn kama kutusaidia?Hizi zina impact kubwa sana zinaporipoti kwa wafadhili na mabwana zetu wa huko nje.
yes ni katiba mbovu ambayo inawapa madaraka makubwa watawala na kuwalinda hata pale wanavpo tenda ukatiliKwa hivyo tatizo ni katiba?
Nadhani haishii kwenye katiba tuu naona hata mindset za Watanzania nitatizo kubwa kuliko katibayes ni katiba mbovu ambayo inawapa madaraka makubwa watawala na kuwalinda hata pale wanavpo tenda ukatili
Unaona kama leo unadhani Tundu anaachiwa??? Hapana na yeye atatunisha misuli leo maana anajua hawatamfanya kituAfrika bado inajenga mifumo ya kidemokrasia na huu mchakato huwa unachukua muda mrefu sana. Hizi asasi na mikataba ndio ngao pekee iliyobaki inayomzuia dikteta asigeuke kuwa mungu mtu kabisa. Giving up sasa hivi ni kujisalimisha mapema kwenye utumwa.
Nakubaliana na wazo lako la mindset.Nadhani haishii kwenye katiba tuu naona hata mindset za Watanzania nitatizo kubwa kuliko katiba