Shida ya kununua mapage ni moja.
Hujui walichokuwa wanafollow hao followers kwa sababu yeye keshafuta almost posts zote na kakubakishia chache anakuuzia wewe. Ukiitumia wewe ni hasara, mfano yeye alikua anapost umbeya na udaku udaku akapata followers wakina mwajuma ndala ndefu na vivulana vya mjini. Wakajaa huko. Au alikua anapost wanawake wakitingisha makalio na mapozi ya nusu uchi. Akawajaza madogo wanaobalehe.
Wewe unakuja kuwauzia viatu vya 50,000 au laki kati ya hao wote hakuna atakayekuwa mteja wako wa maana. Wao wanachojua ni hela ya bundle tu. Utakuta mtu ana followers 3000 lakini akipost bidhaa analikes 11.
Interest 2 watakaoulizia ulizia kisha basi. Hakuna utakayeclose naye deal.
Kuna manzi mmoja namjua. Alikua anajipost sana kavaa nusu uchi na anaonekana kwenye video za maunderdog kadhaa za music. Kifupi ni malaya tu wa town. Akapata followers kibao. Sasa hivi anaiuza ile page.
Unatarajia nini hapo.