Push ups ni kwa ajili ya kujenga misuli na mazoezi ya maungio/joints.
Kuna aina nyingi za pushups ila nyingi zinahusisha misuli ya kifuani ( pectoralis major ) na ya nyuma ya mkono ( triceps brachii muscles ), hiyo ndio musuli inayojengeka vuzuri kwa kupiga push ups.
kuna push ups watu wa workouts wanaziita V, hizi huwa pia zinahusisha misuli ya kwenye bega (deltoid muscles) .
Hivyo hiyo ni gym tosha.
wanaonyanyua vyuma pia inategemea wananyanyua kwa staili gani, ndio maana mtu kama unaenda gym ni vyema uwe na instructor wa kukuelekeza namna ya kunyanyau chuma ili kufikia lengo lako katika kujenga mwili.
wale wanaolala kwenye bench na kuvyavyua chuma ni sawa tu na wanaopiga push ups tofauti ni uzito na body mechanics.
Wale wanaokaa au kusimama na kunyanyua chuma kwa kukuvya kiwiko(elbow joint) hawa wanafaida ya kujaza misuli ya mbele ya mkono (biceps) .
Hivyo ni vyema kubalance mazoezi ili mtu kuwa na shape nzuri.
I hope umeelewa.