Nini faida za water dispenser?

Nini faida za water dispenser?

daah kwa maelezo yanayotolewa hapa hata ningekuwa mimi siwezi kupoteza ela kununua iyo kitu

ivi vitu vingine tunanunua kufuata mkumbo tu kwa kuwa fulani analo ngoja namimi niwe nacho

uko ni kujaza takataka tu ndani
 
Wakuu naombeni kujua faida/umuhimu wa water dispenser

Nimekuwa nikiziona Tu.

Mtu friji analo na jug la umeme analo Ila bado anataka na water dispenser.

Nini umuhimu wa water dispenser?
jug la umeme lina kazi yake,friji ina kazi yale ambayo ni pamoja na kupoza maji,lakini wayer dispenser kazi yake ni kupoza na kuchemsha maji na ukitaka kutumia,unabonyeza vitufe vyake ili upate maji ya baridi au ya moto,kwenye friji inakubidi uweke maji kwrnye chupa au madumu na kila ukitaka inakubidi kufungua mlango wa friji ni usumbufu
 
Utapata maji ya baridi au ya moto kwa uharaka zaidi.Kinyumbani nyumbani haina faida sana ila kama uwezo unaruhusu unaweza kuwa nayo. Ila maofisini ni muhimu ili kuepusha watu kila mara kuchemsha maji kwa kutumia majug wakihitaji maji ya chai au kahawa.
Wewe umefocus kwenye kuchemsha bila kutaja matumizi mengine, utampotosha mleta uzi.
 
FAIDA ZA WATER DISPENSER nikama ifuatavyo;

1. Usafi wa maji; inamaana ukiweka maji safi kwenye dispenser kwa asilimia kubwa yanakuwa salama na anayechota anafungua koki hivyo hawezi kuyachafua tofauti na kuchota kwenye mtungi/ndoo.

2. Inauwezo wa kupasha maji joto au kupooza kwa umeme kidogo sana huku ikijizima yenyewe kuepuka kupoteza umeme

3. Inarahisisha kazi kwani watu/wageni wanajihudumia wenyewe kwa kuchota maji wanayotaka wenyewe (moto/baridi) kwani inawekwa mahali inapo onekana vizuri.

4. Muarobaini wa magonjwa ya tumbo (kuharisha) kwani unaweza kujwa maji ya moto/uvuguvugu wakati wowote. lakini pia maji yakiwa hapo hayawezi kuchafuka

5. Inakuhahakikishia kuwa na maji safi na salama ya kunjwa wakati wote kwani mara zote inaonekana kirahisi hivyo maji ya kipungua tu mtu anaona na kuleta mengine

6. Inachukua nafasi kidogo na kupendezesha nyumba
 
Wakuu naombeni kujua faida/umuhimu wa water dispenser

Nimekuwa nikiziona Tu.

Mtu friji analo na jug la umeme analo Ila bado anataka na water dispenser.

Nini umuhimu wa water dispenser?
Ulofa unakusumbua. Ukitaka kikombe cha kahawa unaenda kuwasha heater, maji ya kunywa kwenye friji.
Tafuta hela ubadilishe mboga.
 
Nini umuhimu wa water dispenser?
Nikiamka naenda kuwasha waterdispenser
Naenda kuoga. Nikitoka kuoga napata maji safi ya moto,, huu ndio umuhimu wangu.

Situmii jug, sbb jug nalichemshia maji ya kuoga.
 
Back
Top Bottom