Nini hasa chanzo cha vurugu za mwaka 2001 kule Zanzibar?

Nini hasa chanzo cha vurugu za mwaka 2001 kule Zanzibar?

Christopher Wallace

JF-Expert Member
Joined
Dec 8, 2015
Posts
1,479
Reaction score
3,788
Wakuu wa jukwaa hili, sisi vijana wenu tunaomba mtujuze ni nini hasa kilijiri mpaka kukatokea vurugu kubwa hasa kule visiwani mwaka 2001 na kupelekea wengine kupoteza maisha!

Natanguliza shukrani...
 
Hawezi kusema yote lakini utapata picha
Wakuu wa jukwaa hili, sisi vijana wenu tunaomba mtujuze ni nini hasa kilijiri mpaka kukatokea vurugu kubwa hasa kule visiwani mwaka 2001 na kupelekea wengine kupoteza maisha!

Natanguliza shukrani...
Renzo...
Niruhusu kwanza nilirekebishe swali lako.

Umekosea kuuliza swali lako kwa kuuliza yaliyotokea Zanzibar 2021.

Ulitakiwa ulipanue zaidi swali lako uulize kama hivi:

Kwa nini historia ya Zanzibar imekuwa ni historia iliyojaa umwajikaji damu toka Mapinduzi ya 1964 hadi sasa?

Swali lako likiwa hivi wasomaji watanufaika na michango itajayogusa historia ya Zanzibar toka enzi ya Masultani hadi utawala wa Serikali ya Mapinduzi.

Hivi itakuwa rahisi kupata ukweli wa msiba huu ulioita, "vurugu na kupoteza maisha."
 
Karibu sheikh
 
hakuna cha historia ya tokea enzi eti Zanzibar ni yenye kumbukumbu mbaya,tatizo ni kuwa
TANZANIA hakuna Tume Huru ya Uchaguzi ,hilo ndio tatizo na lilianza kwa wapemba na sasa athari zake zimetua kwa machogo.

Na kubwa waZanzibari wameikataa CCM ,wanaochomekwa kitaalamu huitwa vibaraka ,nani asiejua Kikwete alifanya nini baada ya kuambiwa CCM imeshindwa uchaguzi bahati nzuri hata chombo kimoja cha habari kiliwahi kutangaza kwamba CUF imeshinda,

Mpaka leo katika mikusanyiko ya watu kuna watu wakitajwa majina yao WaZanzibari husema Laana tullah yaani Mwenyezi Mungu amshushie laana mtu huyo.

Propaganda za kusema Zanzibar wanahistoria iliyojaa umwagaji damu huo ni uongo na hauna nafasi tena ,weka Tume huru yenye kujiamini,isiyofuata maelekezo ya chama chochote .

tatizo la Tume huru sasa limetua hata hapa Tanganyika na tunayashuhudia ,sema huku machogo wanaogopa kuandamana wanashindwa kuoganaizi maandamano kiutaalamu ,nchi kubwa kama hii mnashindwaje kuoganaizi maandamano hata ya watu mia mia kila mji ,nina uhakika kama kila kitu kitakuwa organized,lakini jamaa ni magoigoi wa kutupwa.
 
Baada ya CUF kudhurumiwa kwenye uchaguzi Mkuu wa mwaka 2000!
 
Back
Top Bottom