Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,390
- 152,301
Hivi ni kweli vituo vya Radio na Television vinaendeshwa kwa kutegema matangazo na udhamini wa vipindi tu?
Hivi vituo vingi ni vya watu binafsi tena zaidi ni wafanyabiashara. Sasa kupitia matangazo na udhamini wa vipindi tu, wanaweza kweli kuendesha vituo hivyo kwa faida na kulipa kodi serikalini? Je, kuna vyanzo vingine na kama vipo ni vipi hasa?
Nimeuliza maswali haya hasa baada ya jana kusikia kuwa Bakhresa ametumia zaidi ya sh bilioni 56 kuanzisha Azam tv.
Ni hatua nzuri na ya kupongeza lakini nini hasa vyanzo vya mapato vya kuendesha biashara hizi kiasi kwamba mtu anaweza kulipa wafanyakazi, kurudisha hela ya uwekezaji, kulipa kodi na bado akapata faida?
Hili ni swali ambalo nimekuwa nikijiuliza muda mrefu bila majibu licha ya ukweli kuwa matangazo huwa yanalipiwa hela nyingi.
Wenye kujua mtusaidie na wengine.