Nini hasa chanzo kikuu cha Mapato ya TV / Radio Stations?

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Hivi ni kweli vituo vya Radio na Television vinaendeshwa kwa kutegema matangazo na udhamini wa vipindi tu?

Hivi vituo vingi ni vya watu binafsi tena zaidi ni wafanyabiashara. Sasa kupitia matangazo na udhamini wa vipindi tu, wanaweza kweli kuendesha vituo hivyo kwa faida na kulipa kodi serikalini? Je, kuna vyanzo vingine na kama vipo ni vipi hasa?

Nimeuliza maswali haya hasa baada ya jana kusikia kuwa Bakhresa ametumia zaidi ya sh bilioni 56 kuanzisha Azam tv.

Ni hatua nzuri na ya kupongeza lakini nini hasa vyanzo vya mapato vya kuendesha biashara hizi kiasi kwamba mtu anaweza kulipa wafanyakazi, kurudisha hela ya uwekezaji, kulipa kodi na bado akapata faida?

Hili ni swali ambalo nimekuwa nikijiuliza muda mrefu bila majibu licha ya ukweli kuwa matangazo huwa yanalipiwa hela nyingi.

Wenye kujua mtusaidie na wengine.
 

Vinalipa sana tu hasa ukiwa na wasimamizi wenye weledi mkubwa lakini pia wawe ni watu ambao wanajua na wameishi ndani ya tasnia hiyo...

Kuna mambo mawili hapo:

LOW RISK = LOW RETURN: Yaani hapa ukiwekeza mtaji mdogo katika media industry basi na return yako itakua taratibu sana maana utatoa product dhaifu ambayo itachukua muda mrefu audiance kukuelewa na kupata attention kubwa hivyo hata kupata wadhamini na matangazo makubwa inakua shida sana.

HIGH RISK = HIGH RETURN: Hapa ukiwekeza mtaji mkubwa katika media industry ni rahisi sana kukubalika haraka kwa audiance kwa sababu utatoa product bora na pia promotion ya media yako itakua ni kubwa sana so inakua rahisi sana kupata sponsorship na matangazo makubwa ya pesa nyingi sana..mfano ni uwekezaji uliofanywa na AZAM ni mkubwa sana hvyo itakua rahisi sana kwao kufanikiwa maana kabla hata watu hawajaona content ya product itakayotoka lakini tayari wako attention na wanaisubiria kwa hamu kubwa na hii itakua rahisi sana kupata matangazo makubwa ndani ya muda mfupi.

All in all Media zinalipa sana ukiweka strategy nzuri na usimamizi mzuri na watu sahihi.
 
Mi labda niongezee swali tu ambalo nalo linaniumiza siku nyingi. Vipi kuhusu yale mashirika makubwa habari maana wale mwanzo mwisho ni habari tu halafu ni za kina zinazopelekea wao kutumia gharama kubwa vipi na hao wanapataje faida?
 
Kinadharia ni kweli kiuhalisia, vyanzo vikuu vya mapato ya kujiendesha kwa Radio na TV Stations, inatokana na matangazo ya biashara, vyombo hivyo inayoyapata toka kwa wadhamini wa vipindi hivyo na wale wanaolipia airtime ya matangazo yao, kwenye vipindi vya Radio na TV Stations hizo.

Kwa maana hiyo iwapo Radio Station X, ina wasikilizaji wengi na TV Station Y, ina viewers wengi sana wa TV Station hiyo, vyombo hivyo vitaattract wafanyibiashara kutangaza zaidi kwenye vyombo hivyo vya habari.

Kutokana na hali hiyo vyombo vya habari huwa vinajitahidi wakati wote kuleta programmes zao za Radio na TV Stations, ambavyo wana uhakika, programmes hizo zitavutia wasikilizaji na waangaliaji wengi zaidi wa vyombo vyao vya habari.

Hata hivyo hiyo theory inaapply zaidi kwenye vyombo vya habari vya binafsi, na haiko hivyo kwenye vyombo vya Umma na vile vinavyomilikiwa na taasisi za kisiasa na za kidini.

Mathalani TBC, kutokana na kuwa chombo cha Umma, ambacho kinaendeshwa kwa ruzuku, inayotokana na kodi za wananchi wa nchi hii, bila kujali itikadi zao za kisiasa, kwa hiyo chombo hicho kimekuwa hakijali kinapoendesha programmes zake kwa kujiegemeza wazi wazi kwa kukipendelea chama tawala cha Sisiem, kwa kuwa wanajua hata kama watazamaji wote watawakimbia na kuangalia TV Stations nyingine, lakini wao wanajua itakapofika mwisho wa mwezi, mishahara ya wafanyakazi wao ni lazima italipwa, kutokana na fungu litakalotoka hazina!

Vivyo hivyo kwa Radio Station kama Uhuru FM, nao wanajua hata kama Radio yao itakuwa na wasikilizaji 'kiduchu' sana, bado wafanyakazi wake, 'watalamba' mishahara yao kutokana na ruzuku kutoka Lumumba.

Hata hivyo kutokana na swali lako je kwa investment kubwa, kama aliyofanya Bakhresa kwenye AZAM Media ya mabilioni ya shilingi, je upo uwezekano wa kumlipa?

Hapo majibu yake yanaweza kuwa mawili.

Jibu la kwanza ni kuwa inawezekana yeye Bakhresa ameamua kuinvest heavily kwenye vyombo vyake, akiwa na malengo ya siku za baadaye sana kuwa ataweza kuwa amerejesha hayo mapesa yake.

Lakini wapo wafanyibiashara wengine wakubwa wanainvest heavily kwenye vyombo vyao vya habari, bila kutarajia kuwa pesa hizo walizoziwekeza zitarudi kirahisi, ila tu wakiwa na malengo ya kisiasa, kama ilivyo mfano wa Berlusconi wa Italy, na wengine wanaamua kuinvest kwa hela nyingi kwenye vyombo vyao vya habari, just only for prestige, kuonyesha 'kufuru' ulimwengu wamtambue how rich he or she is!
 
Mi labda niongezee swali tu ambalo nalo linaniumiza siku nyingi. Vipi kuhusu yale mashirika makubwa habari maana wale mwanzo mwisho ni habari tu halafu ni za kina zinazopelekea wao kutumia gharama kubwa vipi na hao wanapataje faida?

hizo media kama bbc (Uingereza), CNN (USA),Aljazeera (QATAR) zinaendeshwa kwa ruzuku kutoka kwa nchi hizo na kamwe HAWABANWI cha kurusha wako huru katika uhariri. lakini pia urusha vipindi kwa ufadhili fulani.mfano wanaweza kutuma crew nchini tanzania kufuatilia issue ya albino kwa ufadhili wa under the same sun na katika habari zao wasiwataje au wanaweza kufutailia jambo fulani kwa maslahi ya mfadhili fulani bila hata jamii kujua.pia mara moja moja huweka matangazo mafupi mfano aljazeera wana tangazo la QATAR airways.
 

Asante mkuu kwa majibu yako hasa hizo aya mbili za mwisho zinaweza kuwa na ukweli ambao wengi wasiojua au kuutarajia.
 
Mi labda niongezee swali tu ambalo nalo linaniumiza siku nyingi. Vipi kuhusu yale mashirika makubwa habari maana wale mwanzo mwisho ni habari tu halafu ni za kina zinazopelekea wao kutumia gharama kubwa vipi na hao wanapataje faida?

Hapa mimi mwenyewe nataka kujua.
 
Kwa kuongeza tu hayo mashirika makubwa kama BBC pia yanafadhiliwa na pesa za wananchi wote wanaoishi UK kwa kulipa TV licence ambapo kila nyumba yenye TV inalipa hio fees .Hio fees ndio inayolifadhili BBC kwa kiasi kikubwa plus ruzuku kutoka serikalini.
 
Kwa kiasi kikubwa biashara hii kwa nchi za dunia ya tatu Mfano Tanzania inalipa. Mosi hadhira kubwa ni ya watu wasio jitambua kiasi kwamba wanapenda kuangalia vipindi vyenye mambo lahisi yaliyo fanyiwa utafiti wa kina. Kwa maana hiyo utaajiri cheap Labour wengi kama yule jamaa maarufu sana mwenye jukumu la kuchombeza chombeza. Pili ni vyombo vilivyopo, vyombo vya habari vingi vimeshindwa kujipambanua kwa Kuja na vipindi "unique". Kwa maana hiyo waweza kuwa ni mchanga Lakini ukawapita wakongwe. Ndg Diallo akiongea na wanachuo wa SAUT mwaka 2008 alisema "turnover" ya media zake ni 1bil kwa mwezi.
 
magazeti ni biashara kichaa hayalipi
radio angalau na gaharama zake za kuendesha na mtaji ni kidogo
tv inalipa japo gharama za kuanzisha ni kubwa na production cost ni kubwa
 
 
 

Umeiva ndugu kwenye Corporate Finance
 


Sina uhakika kuhusu Al Jazeera lakini CNN hakijiendeshi kwa ruzuku Mkuu. CNN ni subsidiary ya kampuni kubwa ya habari ya Time Warner ambayo baadhi ya subsidiaries zake nyingine ni jarida maarufu la TIME, pia wanamiliki vituo vya TV vya HBO, Cartoon Networks, Turner Broadcasting Systems, studio ya kutengeneza movies ya Warner Bros na lebo ya muziki ya Warner Music Group.
 

Uwekezaji wa vyombo vya habari ni uwekezaji wa muda mrefu (long term investment). Wanaowekeza huko hawatarajii kupata faida leo wala kesho bali wamelenga muda mrefu ujao na ndio maana kama huna mpunga mrefu huwezi kufanya hiyo biashara. Pia matangazo ya TV ni ghali sana, tangazo la kawaida la sekunde 15 si chini ya 350,000/= kwa muda wa kawaida. Ukitaka lirushwe wakati ambao watu wengi wanaangalia TV (mfano wakati wa taarifa ya habari n.k) lazima ukohoe si chini ya 500,000/=. Kununua airtime ili urushe kipindi chako cha saa moja lazima utoe si chini ya 5,000,000/= bado kuna package nyingine kama sponsorship n.k.
 
 
Kwa Azam kuwa na media yake ni kwamba bidhaa zake na huduma anazotoa zitapata free ride ya matangazo hivyo kuokoa fedha nyingi sana ambazo angelipia kwingine ( A penny saved is a penny earned ), Azam team itaonyeshwa live mechi zote, pia, ni njia mojawapo nzuri sana ya kulinda business empire yake na campaign ''mbofumbofu'' dhidi yake na faida nyingi tu atapata kwa kutangaza kwa wingi bidhaa zake n.k.
 
Mi labda niongezee swali tu ambalo nalo linaniumiza siku nyingi. Vipi kuhusu yale mashirika makubwa habari maana wale mwanzo mwisho ni habari tu halafu ni za kina zinazopelekea wao kutumia gharama kubwa vipi na hao wanapataje faida?

Toa mfano wa shirka ambayo mwanzo mwisho haina matangazo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…