Bigbootylover
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 2,847
- 1,828
Habari zenyu wakuu, juzi juzi hapa zilisambaa habari kuhusu huyu jamaa wakuitwa UDEUDE, msanii na mtunzi wa nyimbo kadhaa za mastaa hapa bongo kwamba alipigwa risasi, akiwa na msanii mwenzake na wote wakapoteza maisha kwa tuhuma za ujambazi huko TANGA, kwanza naomba kujuzwa kama ni kweli na pia nijue hasa nini kilitokea! Yaani inamaana mastaa wetu wanaishi maisha mazuri huku wakifanya mambo mabaya nyuma ya pazia? Tafadhali naomba kujuzwa