Nini hasa kusudi la kuishi?

Nini hasa kusudi la kuishi?

Maisha ni season hivo inategemeana umeamua binafsi kucheza kama nani!
Ndio maana wapo walio amua kucheza kama
Jambazi
Tapeli
Daktari
Fisadi
Askari
Mkulima
Mwizi
Mwalimu
Mchawi
Mganga
Nazaidi yahapo.
Hayo maisha yataendelea kua season katika maisha yako hadi pale utakapo amua kuishi maisha mengine kabisa ukiwa hai kwawakati huu au hapo utakapo zaliwa upya.
Maisha yetu sio season bt yamegeuka kua season ajili ya uchache wa maarifa.
 
Ujana usikutapeli aisee na usiishi kama Ted Jorgensen
Unataka kusema kula mishangazu ni hulka za ujana..

Hapana mkuu nipo care pia na play safe..
Mambo yangu yanaenda.
Sihongi mtu
Siombwi ya vocha
Siombwi ya saluni
Siombwi vicoba

Mkuu imagine hapo.....
 
Manyanza

JF-Expert Member​

AKIWA Kijana, alifanya tukio. Hakujuta. Na akasahau. Akaishi miaka 44 mingine. Ndipo akatokea mtu akamkumbusha kile alichokifanya. Akaumia. Akatamani asahihishe makosa yake. Hakupata fursa hiyo. Miaka mitatu baadaye akafariki dunia akiwa mwenye huzuni kubwa.

Zingatia, ujana ni tapeli mkubwa wa maisha. Ujana utakulaghai na kukufanya uone maisha ni hayohayo uliyonayo katika wakati uliopo. Ujana unaweza kukughilibu na kukusahaulisha ujio wa kesho. Ujana hufumba macho na huziba masikio. Si walisema ujana maji ya moto?

Ted Jorgensen, alipokuwa na umri wa miaka 17, alikutana na binti mrembo, Jacklyn Gise, aliyekuwa na umri wa miaka 16. Wakapendana. Wakaanza safari ya mapenzi. Jacklyn akanasa ujauzito.

Wakati Jacklyn anashika mimba, alikuwa mwanafunzi wa high school. Ted alikuwa mcheza sarakasi aliyekuwa na ndoto za kufanikiwa kwenye mchezo huo.

Januari 12, 1964, mtoto akazaliwa. Jeffrey ndilo jina walilompa. Jeffrey alipozaliwa, Ted alikuwa ameshatimiza umri wa miaka 18, Jacklyn miaka 17. Na sababu ya mtoto na malezi, ndoto za masomo zikayeyuka. Ted na Jacklyn wakafunga ndoa.

Maisha ya ndoa yakawa magumu. Ted alikuwa mlevi kupindukia. Mara arudi nyumbani alfajiri au asirudi kabisa. Ted alikuwa na kipato kidogo lakini hakukitumia kulea familia, bali starehe zake binafsi.

Baada ya miezi 17 ya ndoa, Jacklyn akaomba talaka. Ted akakubali. Wakaachana. Jacklyn akarudi kwa wazazi wake. Miaka miwili baadaye, Jacklyn akapata mwanaume mwingine, Miguel Bezos. Wakafunga ndoa. Bezos akaomba kumuasili Jeffrey awe mwanaye kisheria. Ted akasaini nyaraka zote kuhalalisha mtoto wake atwaliwe na Bezos.

Mwaka 2012, mwandishi Brad Stone alipokuwa anakusanya taarifa ili aandike kitabu “The Everything Store” kilichohusu maisha ya bilionea mmiliki wa kampuni ya Amazon, Jeff Bezos, alimfikia Ted. Akamuuliza kama alikuwa na habari kuhusu mwanaye aliyezaa na Jacklyn mwaka 1964.

Ted akavuta kumbukumbu, kisha akajibu: “Nimekumbuka. Hivi yule mtoto bado yupo hai kweli?” Brad akamjibu: “Yupo hai. Ndio huyu bilionea mmiliki wa Amazon.” Ted akasikitika, lakini akakiri hakuwa baba bora kwa Jeffrey wala mume mzuri kwa Jacklyn.

Kuanzia hapo, Ted alianza kutafuta nafasi ya kuonana na mwanaye Jeffrey, angalau wazungumze, japo amtambue. Nafasi hiyo angeipata wapi?

Mwaka 2014, Ted aliumwa sana. Akaandika barua nyingi kwa Jeffrey, kumjulisha hali yake na kiu yake ya kumuona kabla hajaaga dunia. Hakupata majibu.

Hakuna ajuaye kama Jeffrey aliziona hizo barua na kumkaushia au hakuziona kabisa. Ila ni uhakika kuwa alitambua kuwa baba yake mzazi alikuwepo.

Mwaka 2015, Ted alifariki dunia bila kuonana na mwanaye wa damu, Jeffrey. Aliishia kumsoma na kumuona kwenye vyombo vya habari kama watu wengine.

Kuhusu maisha ya Ted; baada ya kuachana na Jacklyn, aliendelea na mitikasi yake ya kucheza sarakasi na ulevi. Miaka 10 baadaye, akagundua maisha aliyokuwa akiishi hayakuwa na kesho nzuri. Akaacha ulevi. Akafungua duka la kuuza baiskeli. Hiyo ndio ikawa kazi yake mpaka alipofariki dunia.

Ted baada ya kuachana na maisha ya ulevi, alimuoa mwanamke mwingine, jina lake Linda. Hakupata mtoto mwingine. Mkewe, Linda, alikuwa na watoto wanne.

Miaka miwili baada ya kifo cha Ted, taasisi ya utafiti wa mali na utajiri duniani ya Forbes, ilimtangaza Jeffrey kuwa tajiri namba moja duniani. Akimpita tajiri namba moja wa muda mrefu duniani, Bill Gates.

Kwa sasa, Jeffrey ana utajiri wa dola 183.6 billioni, ambazo ni sawa na Sh242.4 trillioni.

Jeffrey anatambua kuwa Ted ni baba yake, kwani cheti chake cha kuzaliwa na kumbukumbu zote za hospitali zinamtaja Ted ndiye baba yake.

Hiyo ni stori kuhusu tajiri namba moja duniani, Jeff Bezos na baba yake mzazi, Ted Jorgensen. Story kuhusu ujana na utapeli wake.

Ted angejua? Maskini hakujua. Alikufa akijuta. Angejua Jeff ndiye mwanaye wa pekee, angekubali kumwacha kwenye mikono ya baba mwingine? Angefunuliwa kuwa Jeff angekuwa tajiri namba moja duniani, unadhani angemtelekeza?

Hata hivyo usimlaumu sana Ted. Alitapeliwa na ujana. Siku zote elewa hili, ujana ni tapeli mkubwa mno kwenye safari ya maisha.
Daaah kusema kweli hi story nimesoma huku nikiwa na masikitiko makubwa sana kaka..

Hapa kuna la kujifunza aiseee daaah maisha haya kweli tujiandae snaa kwa ajiri ya kesho yetu .

Kaka asante sana kwa ushauri kama huu naimani kidogo kidogo taanza kupata mwanga na kujua ni jinsi gani ya ku tune huu ujana wangu ukawa wa faida tele hapo baadae..

Nayopitia mimi kuna mda natamani niachane nayo ila naona nishaingizwa kwenye adiabatic system no body in no body out najuta aiseeee....

Na kama ni Elastic hapa ishafika limit i turned into plasticity sijui nitarudisha lini elasticity yangu maaana......
 
Kwa kweli kuwa nice guy na kuwa selfless kumechangaia pakubwa maisha kunila kavu kavu,

kuna shortcuts unaziona za kukuondolea utu na integrity zinakuja Ila unaona hapana Ila wengine wanapiga na kutoboa.

Kuna time kuna vitu unafanya unafanikisha vitu flani, mwingine anajaribu anaangukia pua ... Vice verse is true 😁😁😁

Yes kila siku tunapambana kujua maana ya maisha lakini dhidi ninavyowaona watu wanafariki na mipango na dreams zao ndivyo najua kuwa maisha ni sasa. Maisha yako ni zao la maamuzi unayoyachukua kwa maana yenyewe ndio yanaruhusu na kuzuia vitu vyote vinavyokutokea japo vingine vichache hututokea nje ya uwezo wetu..

Maisha ni actions za kila siku
Maisha ni mjumuisho wa makosa na vitu sahihi tunayoyafanya kila siku

Maisha ni historia ambayo tunaitengeneza kila siku kwa vitu nilivyoainisha hapo juu

Hutokaa uyaelewe maisha kwani jana ishapita, Leo ndio hiyo tunaingalia na kesho hatuijui..
conclusion yako bado inabaki kuwa maisha ni Ufala.
Kwani maelezo yako bado yanamuacha mtu gizani.
Fikra kama za Atheist, wewe ni Atheist?
 
Daaah kusema kweli hi story nimesoma huku nikiwa na masikitiko makubwa sana kaka..

Hapa kuna la kujifunza aiseee daaah maisha haya kweli tujiandae snaa kwa ajiri ya kesho yetu .

Kaka asante sana kwa ushauri kama huu naimani kidogo kidogo taanza kupata mwanga na kujua ni jinsi gani ya ku tune huu ujana wangu ukawa wa faida tele hapo baadae..

Nayopitia mimi kuna mda natamani niachane nayo ila naona nishaingizwa kwenye adiabatic system no body in no body out najuta aiseeee....

Na kama ni Elastic hapa ishafika limit i turned into plasticity sijui nitarudisha lini elasticity yangu maaana......
roho hii radhi lakini mwili ni dhaifu 😮‍💨
 
Itampa faraja kuona kwamba hata kesho anaweza kujikwamua na kuendelea kupambana kuzivuka changamoto zake ili ajenge maisha mazuri kwa kiwango ambacho Mungu atambarikia kukipata.
Nikusifie kama paulo alivyowasifia waathene.. 😁
Yah unafikra nzuri za uchambuzi wa maisha na unaonekana ni mtu wa kupenda kufikiri, kuchambua na kutafuta tafuta ukweli wa mambo..

But naona unakwama sehemu moja hujui umuhimu wa mahusiano kati ya Mungu na binadamu katika maisha yake.
 
conclusion yako bado inabaki kuwa maisha ni Ufala.
Kwani maelezo yako bado yanamuacha mtu gizani.
Fikra kama za Atheist, wewe ni Atheist?
Mimi sio atheist, naamini sana katika Mungu

Kuona maelezo yangu yanamuacha mtu gizani ni kwa sababu "the most certain thing about life is uncertainity"

The fact hujui ni nini kitatokea masaa matatu au kesho inakufanya usiwe na total control ya maisha Ila tunachokifanya, ni kutengeneza mazingira ambayo yatasababisha maisha yetu yatokee katika namna flani au yatupe assurance of the future, lakini bado hatuna guarantee kuwa vitu vitabaki sawa kama tunavyitarajia..

Ndio maana watu wanawekeza sana ili tu wasije teseka uzeeni lakini haina maana kuwa wote waliowekeza hawakuishia kuteseka...

Watu wanazaa wapate familia ili uzeeni wasiishi upweke lakini haimaanishi wote wenye familia hawakutelekezwa

Hayo ndio maisha mkuu, by nature mimi nipo futuristic ila baada ya muda nikagundua maisha hayaweze kufurahiwa kama siku zote utakuwa na kiu ya kusubiri ufanikishe kitu flani ndio uyafurahie. Maisha ni kuishi kwenye moment uliyopo KWANZA, kuifurahia na kushukuru kwa ulichonacho kwanza..

Then kuenenda kwa kile unachokitarajia
 
Sawa ndio ufala wenyewe, sawa kwa sasa nina mke na watoto nakunywa na kustarehe lakini kesho yangu lolote linaweza kutokea kupoteza familia na hata mm kuwa ombaomba.
 
Exactly Ila tu tunachofanya ni kuomba Mungu lakini kufanya kazi ili mradi mambo yasiende vibaya kwa kutojiandaa kwetu.

Ila cha msingi zaidi ni kufurahia hizo family moment ulizobarikiwa mkuu
 
I looking for assurance of better tomorrow
 
Manyanza

JF-Expert Member​

AKIWA Kijana, alifanya tukio. Hakujuta. Na akasahau. Akaishi miaka 44 mingine. Ndipo akatokea mtu akamkumbusha kile alichokifanya. Akaumia. Akatamani asahihishe makosa yake. Hakupata fursa hiyo. Miaka mitatu baadaye akafariki dunia akiwa mwenye huzuni kubwa.

Zingatia, ujana ni tapeli mkubwa wa maisha. Ujana utakulaghai na kukufanya uone maisha ni hayohayo uliyonayo katika wakati uliopo. Ujana unaweza kukughilibu na kukusahaulisha ujio wa kesho. Ujana hufumba macho na huziba masikio. Si walisema ujana maji ya moto?

Ted Jorgensen, alipokuwa na umri wa miaka 17, alikutana na binti mrembo, Jacklyn Gise, aliyekuwa na umri wa miaka 16. Wakapendana. Wakaanza safari ya mapenzi. Jacklyn akanasa ujauzito.

Wakati Jacklyn anashika mimba, alikuwa mwanafunzi wa high school. Ted alikuwa mcheza sarakasi aliyekuwa na ndoto za kufanikiwa kwenye mchezo huo.

Januari 12, 1964, mtoto akazaliwa. Jeffrey ndilo jina walilompa. Jeffrey alipozaliwa, Ted alikuwa ameshatimiza umri wa miaka 18, Jacklyn miaka 17. Na sababu ya mtoto na malezi, ndoto za masomo zikayeyuka. Ted na Jacklyn wakafunga ndoa.

Maisha ya ndoa yakawa magumu. Ted alikuwa mlevi kupindukia. Mara arudi nyumbani alfajiri au asirudi kabisa. Ted alikuwa na kipato kidogo lakini hakukitumia kulea familia, bali starehe zake binafsi.

Baada ya miezi 17 ya ndoa, Jacklyn akaomba talaka. Ted akakubali. Wakaachana. Jacklyn akarudi kwa wazazi wake. Miaka miwili baadaye, Jacklyn akapata mwanaume mwingine, Miguel Bezos. Wakafunga ndoa. Bezos akaomba kumuasili Jeffrey awe mwanaye kisheria. Ted akasaini nyaraka zote kuhalalisha mtoto wake atwaliwe na Bezos.

Mwaka 2012, mwandishi Brad Stone alipokuwa anakusanya taarifa ili aandike kitabu “The Everything Store” kilichohusu maisha ya bilionea mmiliki wa kampuni ya Amazon, Jeff Bezos, alimfikia Ted. Akamuuliza kama alikuwa na habari kuhusu mwanaye aliyezaa na Jacklyn mwaka 1964.

Ted akavuta kumbukumbu, kisha akajibu: “Nimekumbuka. Hivi yule mtoto bado yupo hai kweli?” Brad akamjibu: “Yupo hai. Ndio huyu bilionea mmiliki wa Amazon.” Ted akasikitika, lakini akakiri hakuwa baba bora kwa Jeffrey wala mume mzuri kwa Jacklyn.

Kuanzia hapo, Ted alianza kutafuta nafasi ya kuonana na mwanaye Jeffrey, angalau wazungumze, japo amtambue. Nafasi hiyo angeipata wapi?

Mwaka 2014, Ted aliumwa sana. Akaandika barua nyingi kwa Jeffrey, kumjulisha hali yake na kiu yake ya kumuona kabla hajaaga dunia. Hakupata majibu.

Hakuna ajuaye kama Jeffrey aliziona hizo barua na kumkaushia au hakuziona kabisa. Ila ni uhakika kuwa alitambua kuwa baba yake mzazi alikuwepo.

Mwaka 2015, Ted alifariki dunia bila kuonana na mwanaye wa damu, Jeffrey. Aliishia kumsoma na kumuona kwenye vyombo vya habari kama watu wengine.

Kuhusu maisha ya Ted; baada ya kuachana na Jacklyn, aliendelea na mitikasi yake ya kucheza sarakasi na ulevi. Miaka 10 baadaye, akagundua maisha aliyokuwa akiishi hayakuwa na kesho nzuri. Akaacha ulevi. Akafungua duka la kuuza baiskeli. Hiyo ndio ikawa kazi yake mpaka alipofariki dunia.

Ted baada ya kuachana na maisha ya ulevi, alimuoa mwanamke mwingine, jina lake Linda. Hakupata mtoto mwingine. Mkewe, Linda, alikuwa na watoto wanne.

Miaka miwili baada ya kifo cha Ted, taasisi ya utafiti wa mali na utajiri duniani ya Forbes, ilimtangaza Jeffrey kuwa tajiri namba moja duniani. Akimpita tajiri namba moja wa muda mrefu duniani, Bill Gates.

Kwa sasa, Jeffrey ana utajiri wa dola 183.6 billioni, ambazo ni sawa na Sh242.4 trillioni.

Jeffrey anatambua kuwa Ted ni baba yake, kwani cheti chake cha kuzaliwa na kumbukumbu zote za hospitali zinamtaja Ted ndiye baba yake.

Hiyo ni stori kuhusu tajiri namba moja duniani, Jeff Bezos na baba yake mzazi, Ted Jorgensen. Story kuhusu ujana na utapeli wake.

Ted angejua? Maskini hakujua. Alikufa akijuta. Angejua Jeff ndiye mwanaye wa pekee, angekubali kumwacha kwenye mikono ya baba mwingine? Angefunuliwa kuwa Jeff angekuwa tajiri namba moja duniani, unadhani angemtelekeza?

Hata hivyo usimlaumu sana Ted. Alitapeliwa na ujana. Siku zote elewa hili, ujana ni tapeli mkubwa mno kwenye safari ya maisha.
Mkuu hii imenigusa sanaaa
 
Back
Top Bottom