Nini hasa maana ya utajiri?

Nini hasa maana ya utajiri?

Mbelajr2023

Member
Joined
Nov 23, 2022
Posts
54
Reaction score
115
Wanajamvi nina wasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!

Nimekuwa nukijiuliza maswali mengi sana kuhusu mambo mbalimbali yanayoendelea katika taifa letu pendwa kabisa Tanzania, Je ni Taifa Tajiri au Maskini?

Mzee wetu mmoja aliwahi kuulizwa kwanini Taifa lako Maskini? Alijibu hata yeye hajui, akaja mzee mwingine ambae mtoto mtundu akamwita mwendazake, yeye akatuambia umma wa watanzania kuwa Taifa hili si Maskini hata kidogo ni Tajiri.

Mambo aliyoyafanya yako wazi yanajulikana, sasa nimebaki katika mawazo mtanziko je nini hasa maana ya UTAJIRI? Wadau naomba mnisaidie,

Rational people think at the margin.

Karibuni
 
Ngoja waje buraza. Mimi baki bencha wa la tatu dii hata sijui.
Nachojua ni kuwa inategemea na falsafa ya mtu na mtu.

Mfano
1. Wachawi huamini tajili ni kuwa na misukule mingi, wengine huamini ni kuwa na nguvu nyingi za kufanya marue rue
2. Wapo wanaoamini kuwa tajili ni kumiliki mali (dhahabu, magari, viwanja na nyumba n.k) hapa utampata mwendazake aliposema nchi hii si maskini ni tajili kwsbb ina raslimali watu wengi, wanyama, ardhi, fedha, madini, wataalamu na malighafi (resources)
3. Wapo wenye mlengo wa kutafsiri dhana ya utajili kuwa na wingi ardhi anayomiliki, watu na wanyama na watoto na wafanya kazi nyumbani kwake (watu anaowahudumia) (human resource) akina mfalme suleimani na akina Reginard Mengi, Ayubu nakuendelea. Almost watemi na wafalme ndio ilikuwa dhana yao ya utajili
4. Wapo wanaotafsiri dhana ya utajili kuwa ni wingi wa pesa wanazomiliki, hapa utakutana na akina boss, mfn Bill Gates, Elon Musk, n.k

Sasa sijui wewe unatafsiri utajili kwa dhana ipi. Hapo jiongeze mwenyewe mi darasa la 3D ndio nimeishia hapa
 
Ngoja waje wajuvi wa haya mambo waje kutuelekeza.
 
Utajiri ni fikra zako tu kila mtu ana mtazamo wake kuh dhana ya utajiri
 
Back
Top Bottom