Sheria inayozuwia ndoa za watu wa jinsia moja inalinda utu wa nani? ....
Wewe. Usitake hii thread ifungwe kwa mara ya pili. lolz
"Naye Katibu wa Baraza la Maaskofu nchini (TEC), Padri Antony Makunde, alisema "....Uingereza wasitumie umaskini wa Waafrika kulazimisha suala hilo. Wakitaka kutupa msaada watupe, lakini si kwa masharti hayo ya
kuunyanyasa utu wetu wa Afrika ili tukubaliane na utamaduni wao." Alisema ni heri Waafrika wakaendelea kuwa maskini na
kulinda utu na heshima waliyonayo lakini si kutaka kudhalilishwa kwa ajili ya misaada iliyojaa laana ya ushoga na usagaji.
Source:
Viongozi wa dini waionya serikali na ushoga
Mwingine anasema: "Inaonekana kama vile Uingereza na nchi nyingine tajiri bado zinaamini kwamba nchi za Kiafrika ni nchi zinazoongozwa na watu ambao uroho na tamaa yao ya misaada vinaweza kuwafanya wakubali lolote lile hata likiwa baya kwa mila, desturi, imani, utamaduni na
utu wa watu wao……Umaskini hauimanishi maskini kukubali kuuza roho, utu na imani yake kwa ajili ya kupewa misaada."
Source:
Tukubali ushoga au tuachane na misaada
Kwa mujibu wa Makamu Mkuu wa Chuo cha Mtakatifu Augustino (SAUT), Dk. Kitima, "..ushoga ni vitendo vya uovu na ukinuiwa na Serikali ni kuwaudhi wananchi wake, na kwamba kauli ya Waziri Cameron wa Uingereza ni sawa na kauli ya kutaka
kuua utu wa watu….
Ushoga unaharibu utu wa mtu. Kukubali ushoga ni sawa na kuua vizazi vijavyo…"
Source:
Chuo Kikuu cha SAUT chamuasa Kikwete kuhusu "Misaada na ushoga" | Fikra Pevu | Kisima cha busara!
Pia Bakwata imeahidi kuendelea kuunga mkono Serikali kwa misimamo yake ya kukataa kusaidiwa kwa masharti yasiyojali wala
kuheshimu utu na thamani ya Mtanzania, kwa sababu ina lengo zuri la kuutetea utaifa.
Akizungumza katika Baraza la Idd el Hajj katika Msikiti wa Masjid Al Farouq, Kinondoni, Shehe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum alisema, heri kuwa tayari kufa kwa njaa kutokana na umasikini,
kuliko kupewa misaada ya maendeleo kwa masharti ya kudhalilishwa utu.
Source:
HabariLeo | Bakwata- Bora kufa njaa kuliko kukubali ushoga
Ukisoma huko kwenye red inalinda kutonyanyasika kwa "utu wetu wa Afrika", kutokuuliwa au kutoharibiwa kwa utu wa watu, kuheshimu utu, kutokudhalilishwa, nk. Do the above shed some lights? lol. kazi ipo.