Jamani hii nchi haiishi viroja
Yaani ofisi ilijengwa Urambo? Kwa kweli hili ni jipya kabisa masikioni mwangu na bila shaka jamaa alidhani atakuwa Spika wa kudumu
Yaani ni wizio mtupu huu, hata ukipakwa rangi gani bado utabakia kuwa wizi na kushindwa kujua vipaumbele vya taifa
Rais Jakaya Kikwete atembelea Urambo na Ofisi Mpya ya Mbunge na Spika wa Bunge Samwel Sitta iliyogharimu Millioni 170
Rais Jakaya Kikwete akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuzindua rasmi Ofisi ya Mbunge wa Urambo Mashariki. Aliyesimamam ni Mbunge wa Urambo Mashariki ambaye pia ni Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta.
Rais Jakaya Kikwete akikata utepe kufungua rasmi Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Urambo Mashariki Mhe. Samuel Sitta (Kushoto) ambaye pia ni Spika wa Bunge. Ofisi hiyo imeghrarimu jumla ya Tsh 170 Million, ikiwa ni mpango wa serekali kujenga ofisi za wabunge katika kila majimbo yote nchini.
Rais Jakaya Kikwete akikagua Ofisi ya Mbunge wa Urambo Mashariki mara baada ya kuizindua rasmi mjini Urambo. Kulia kwake ni Mbunge wa Urambo Mashariki ambaye pia ni Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta. Ofisi hiyo imeghrarimu jumla ya Tsh 170 Million, ikiwa ni mpango wa serekali kujenga ofisi za wabunge katika kila majimbo yote nchini.
Mbunge wa Jimbo la Urambo Mashariki Mhe. Samuel Sitta ambaye pia ni Spika wa Bunge akiwakaribisha waheshimiwa wabunge mara baada ya kutua katika uwanja wa ndege Urambo kuhudhuria ufunguzi rasmi wa Ofisi ya Mbunge wa Urambo Mashariki. Kushoto ni Mbunge wa Mafia Mhe. Abdukarim Shah.
Ni wazi ni pesa za serikali kutoka hazina, inaweza kuwa kupitia bunge kwani hata hizo za mfuko wa jimbo ni za serikali. Kwa ufupi ni kuwa imejengwa na serikali ambayo vyanzo vyake vikuu vya mapato ni kodi inaliyopwa na wananchi na misaada kutoka njeNaomba kujuzwa ofisi hiyo ilijengwa kwa fedha zipi!...je iliwekwa kwenye bajeti ya Bunge au ni fedha za mfuko wa jimbo?
Mwishoni mwa uspika wa Samwel Sitta, serikali ilijenga ofisi ya spika wa bunge Urambo Tabora ambako ni jimboni kwa spika wa wakati huo mheshimiwa Samweli Sitta. Maswali yangu ni haya:
1. Samweli Sitaa siyo spika tena. Je anaitumia ofisi hiyo au hapana? Na kama ndio anaitumia kama nani na kwa shughuli z
zipi?
2. Spika wa sasa Anna Makinda ameshaitumia ofisi hiyo mara ngapi? Na kama haitumii ni kwanini?!
3. Je utaratibu wa kujenga ofisi kwenye kila jimbo analotoka spika utaendelea?
4. Je ilikusudiwa Sitta awe spika wa kudumu mpaka kufa kwake?
5. Kama ofisi hiyo haitumiki na spika aliyepita na aliyepo ni ya nini? Inafaa kuendelea kuwepo? kwanini isigeuzwe darasa
shule au ghala la kuhifadhia asali?
SITTA anatamani urais, hivyo akiupata "urahisi" atajenga Ikulu pembeni mwa hiyo ofisi. Kisha atatatangaza Tabora ndo Mji Mkuu wa nchi!
Sitta bado anatapatapa baada ya kuangukia pua kwenye uspika!
Rais Jakaya Kikwete atembelea Urambo na Ofisi Mpya ya Mbunge na Spika wa Bunge Samwel Sitta iliyogharimu Millioni 170
Ofisi hiyo imeghrarimu jumla ya Tsh 170 Million, ikiwa ni mpango wa serekali kujenga ofisi za wabunge katika kila majimbo yote nchini.
Rais Jakaya Kikwete akikagua Ofisi ya Mbunge wa Urambo Mashariki mara baada ya kuizindua rasmi mjini Urambo. Kulia kwake ni Mbunge wa Urambo Mashariki ambaye pia ni Spika wa Bunge Mhe. Samuel Sitta. Ofisi hiyo imeghrarimu jumla ya Tsh 170 Million, ikiwa ni mpango wa serekali kujenga ofisi za wabunge katika kila majimbo yote nchini.
Maisha Bora kwa kila mtanzania
Mahesabu yenyewe itakuwa kama hivi; 170,000,000 x239= 40,630,000,000ts
Alafu akina mama pale Muhimbili wanajifungulia wakiwa kwenye sakafu!
Wale mashabiki wa S.Siita wanatakiwa kujitambua kuwa ni mtu wa aina gani!
Focus on issue not personality