Mkupuo wa kwanza zaidi ya 300 wamekuwa mawakili binafsi, bado mikupuo mingine ya Law school. Nini hatima ya hii taaluma nyeti kwa hapa TZ??
Bongo ni matatizo kweli, kutokana na uchache wa mawakili waliokuwepo, wakafanya demand iwe kubwa, hivyo legal fees zikawa juu sana watu wa kawaida wakashindwa kumudu enzi hizo, UDSM ndio chuo pekee kikitoa LL.B, tena admission ilikuwa only 60 students tena wote ni wa Div One.
Mzumbe, Tumaini, Dodoma, Morogoro na Zanzibar, wakajoin team, sasa LL.B zinamwagwa kama njugu, na mawakili kibao. Hili ni jambo jema sasa huduma za kisheria zitakuwa more reachable na more afordable kwa kila mtu. Itafikia wakati, mawakili watabisha hodi kwako, wakiomba kukupatia huduma za kisheria bure, ukishalipwa ndipo uwalipe!. Hili ni jambo la kheri, wewe unalitilia shaka?.
Angalizo: Kusomea sheria na kupata LL.B ni jambo moja, kusajiliwa na kuwa wakili ni jambo jingine, lakini pia kuwa wakili mzuri, nalo ni jingine kabisa!. Kuna mawakili tena wengine vichwa na 1st class zao, lakini mahakamani ni sifuri wakati kuna mawakili wa kawaida tuu, mahakamani ni moto!.
Katika ya mawakili wote wa Tanzania, mfano wa Murtaza Lakha sijamuona mwingine!.