wanasheria naomba mnifafanunulie vitu viwili, mtu akihukumiwa kifungo jela ilihali alishakaa mahabusu lets say 6 months, ile miezi huwa inatolewa kwenye ile 2 years? la pili, hii issue ya jela asubuhi na mchana kuwa ni siku mbili tofauti is it true?
la mwisho lulu alishakaa mahabusu miezi mingapi?
Sina hakika lulu alikaa ndani miezi mingapi
swala la kwamba aliwahi kukaa ndani miezi kadhaa wakati wa upelelezi,
wakili wake alipaswa wakati wa maombolezo,amuelezee Mh Jaji
kabla hajatoa hukumu yake azingatie ya kwamba mteja wake
amekwisha kukaa ndani kwa muda fulani,....kama wakili alikaa
kimya jaji anakuchapa kifungo chake, swali la mwisho mfungwa
anatakiwa atumikie 1/3 ya kifungo chake anafanyiwa remission
ya 1/3 ya kifungo kwa mfano mtu aliyefungwa miaka miwili mathalan lulu
anapunguziwa miezi nane hivyo atatakiwa kutumikia mwaka
mmoja na miezi minne, BUT jambo la msingi la ku NOTE ni kwamba
lulu ana qualify kuomba kifungo mbadala community service
atumikie adhabu yake akiwa nje akifanya shughuli za kijamii
atakazopangiwa ...kwa hivyo miezi mitatu minne ijayo akiwa nje
msishtuke....kuna baadhi ya makosa likiwepo lake ukifungwa
chini ya miaka mitatu sheria inakuruhusu kuomba uitumikie
jamii.