Nini hatma ya mlemavu Chiba baada ya Yamoto band kusambaratika?

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Joined
Dec 11, 2012
Posts
6,067
Reaction score
10,938
Habari wakuu,

Kwa wale wadau wa burudani ya muziki watakuwa washawahi kumuona au kumsikia kijana anayeitwa Karim Seleman ama kwa jina la usanii CHIBA aliyekuwa akifanya shughuli zake za kujiingizia kipato kupitia Yamoto band.

Unaweza kusoma mkasa uliopeleka kupata ulemavu hapa => Karim Seleman 'Chiba' akielezea mkasa wake ulipelekea akatwe mguu

Huyu ni mlemavu wa mguu(ana mguu mmoj), lakini pamoja na ulemavu wake hakubweteka kabisa na kuamua kuwa mnenguaji wa Yamoto Band. Kiukweli CHIBA anacheza vizuri sana kuliko wasanii wengi sana na ukimuona hutosita kutoa shilingi mbili tatu kumpatia.

Kundi lililokuwa likimpa kipato naona limekufa, kila msanii sasa afanya kazi zake kwa kujitegemea. Changamoto imebaki kwa huyu kijana. Je, nini hatma yake?

Juzi nimemuona kupitia wimbo wa Aslay ''Pusha', kuna kituko kimoja alifanya nikajikuta nacheka sana na kummiss.

Wito wangu: Kuna wasanii wakubwa hapa bongo, naomba wamuangalie huyu jamaa. Ana kipaji cha pekee sijapata kuona. Anacheza kana kwamba ana viungo vyote mwilini mwake.

Mwenyezi Mungu azidi kumbariki huyu kijana, ninamhusudu sana.
 
Siamini kama kweli mkuu Jose huna habari hiyo
 
Huyu jamaa n mshikaj wake aslay so hawez kuachwa na aslay ndio maana kwenye ngoma yajke mpya ya pusha kampa shavu
 
Matamanio yako kuhusu huyu kijana naamini yatafanyiwa Kazi na wadau wa music,si unajua Jf ni mtambo mkubwa?
 
Duuh maisha popote god atamsaidia.
 
Aslay kuanza kutoa nyimbo kivyake kumesababisha kundi kwenda mlama
 
Duuuh! nimesoma sababu iliyofanya akatwe mguu inasikitisha,na kilichonisikitisha sana ni jinsi alivyoshughulikiwa na huyo daktari,mimi bado naamini kuna madaktari si mahiri kabisa katika utendaji kazi zao kama alivyo huyo daktari aliyem-attend CHIBA,kamfanya apate mateso ambayo asingelazimika kuyapata wakati wakutibiwa,jinga kabisa hilo lidaktari.

Alishindwa kujua kua mguu ni wakuukata tangu mwanzo hadi mtu akavuje damu na apate maumivu yasiyokua na ulazima ndiyo anamfanyia opersheni,wajinga sana madaktari wengine.

Ndugu na jamaa zetu wengine wanapoteza maisha kijingajinga hivihivi kwasababu yakuendekeza midaktari mijinga inayosomea mitihani tu nakuondoka na GPA zao huku kichwani hawako vizuri.

Inabidi tunapopeleka wagonjwa hospitalini tusiwe tunaweka imani sana kwa madaktari,tuwe nao makini kama tunavyokua makini katika kazi nyingine zenye weledi tofauti na udaktari.Pole CHIBA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…