Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,067
- 10,938
Habari wakuu,
Kwa wale wadau wa burudani ya muziki watakuwa washawahi kumuona au kumsikia kijana anayeitwa Karim Seleman ama kwa jina la usanii CHIBA aliyekuwa akifanya shughuli zake za kujiingizia kipato kupitia Yamoto band.
Unaweza kusoma mkasa uliopeleka kupata ulemavu hapa => Karim Seleman 'Chiba' akielezea mkasa wake ulipelekea akatwe mguu
Huyu ni mlemavu wa mguu(ana mguu mmoj), lakini pamoja na ulemavu wake hakubweteka kabisa na kuamua kuwa mnenguaji wa Yamoto Band. Kiukweli CHIBA anacheza vizuri sana kuliko wasanii wengi sana na ukimuona hutosita kutoa shilingi mbili tatu kumpatia.
Kundi lililokuwa likimpa kipato naona limekufa, kila msanii sasa afanya kazi zake kwa kujitegemea. Changamoto imebaki kwa huyu kijana. Je, nini hatma yake?
Juzi nimemuona kupitia wimbo wa Aslay ''Pusha', kuna kituko kimoja alifanya nikajikuta nacheka sana na kummiss.
Wito wangu: Kuna wasanii wakubwa hapa bongo, naomba wamuangalie huyu jamaa. Ana kipaji cha pekee sijapata kuona. Anacheza kana kwamba ana viungo vyote mwilini mwake.
Mwenyezi Mungu azidi kumbariki huyu kijana, ninamhusudu sana.